SoC03 Kipi kinaizuia Serikali kunitangaza kuwa binadamu kivuli?

Stories of Change - 2023 Competition

EDOGUN

JF-Expert Member
Jul 9, 2023
256
298
Ni saa tatu za asubuhi, nikiwa nafua nguo nje ya nyumba yangu. Nashitushwa na ujio wa ghafla wa askari mgambo wanne wenye nyuso za shari shari wakiwa wameambatana na mwenyekiti wa mtaa. Japokuwa mimi ni kiziwi. Askari mgambo hawa wanalazimisha kuzungumza na mimi kwa amri tu kama vile wanaongea na mtu mwenye masikio mazima kama yao.

Najaribu kujieleza kwa lugha ya ishara lakini hakuna anaetaka kunielewa. Nahisi kama vile hawa mgambo wanafikiri nimejigeuza kuwa kiziwi ghafla ili nikwepe kulipa hicho wanachotaka nikilipie, naona isiwe kesi, nawapatia pesa, elfu kumi na tano, wananiandikia stakabadhi ya mkono, isiyokuwa na maelezo ya kueleweka na wanaondoka kuendelea na zoezi hilo tata kwenye nyumba za majirani zangu wengine.

Ninakosa hata hamu ya kuendelea kufua, narudi ndani nikiwa na masikitiko makubwa mno kama mtu aliyefiwa na mke, hii pesa nimeilipa lakini hata sijui nimelipia kitu gani jamani.

Nimeamua tu nilipe maana hawa viongozi wetu wa mitaa huwa hawana jambo dogo kabisa, sijui kama wana elimu yoyote ya uongozi, unaweza kugomea kulipa elfu tano wakakupatia kesi ya kuvunja na kuiba ukakaa gerezani miaka saba.

Hii pesa niliyoporwa leo inanikumbusha mwaka juzi, wakati naishi mtaa wa Kilimahewa, nilipolazimishwa kulipa faini ya shilingi elfu hamsini, eti kwa kosa la kutokuhudhuria matukio matatu ya misiba yaliyotokea kwenye mtaa wetu. Yaani yule mwenyekiti wa mtaa ule alishindwa kabisa kuelewa kuwa nilishindwa kuhudhuria matukio hayo kwa sababu matangazo yote ya msiba mtaani hutangazwa kwa poromondo (vipaza Sauti), sasa mimi haya masikio yangu mfu yatasikia nini.

Hii pesa niliyopokonywa leo inanikumbusha siku nilipopigwa na polisi kwa kosa la kuingilia msafala wa mkuu wa mkoa, wale polisi walinitwanga kweli kweli, mpaka walipogundua mimi ni kiziwi tayari damu zilikuwa zinachuruzika kila kona ya mwili wangu.

Sijui kwa nini haya matukio ya uonevu ninayofanyiwa yamegoma kabisa kufutika kwenye kumbukumbu zangu, na kibaya zaidi yanazidi kuongezeka kadri ya umri wangu unavyoongezeka.

Mara nyingi najiuliza hivi mimi ni binadamu kamili kweli kama binadamu wengine, mbona sishirikishwi kwa jambo lolote lile, sipewi taarifa ya vikao na mikutano, kwenye mtaa ninaoishi.

Hebu tizama jamani, ni kama hakuna anaejali kabisa uwepo wangu hapa Duniani, sio wananchi wenzangu wa kawaida, sio serikali. Hata kampuni kubwa zinazoheshimika Duniani kwa utengenezaji wabidhaa maarufu, nazo
hazina muda kabisa na mimi.

Hebu tazama kampuni za kutengeneza magari, wameweka honi kwenye kila gari wanayotengeneza kuwatahadharisha binadamu kamili na wanyama wengine ili wasigongwe na magari lakini wameshindwa kujali kabisa kuhusu mimi, inaonekana mimi hata nikigongwa na gari zao, kwao ni sawa tu, hakuna shida.

Hebu tazama kampuni za kutengeneza baiskeli, wameweka kengere za kuwatahadhalisha binadamu na wanyama wengine ili wasigongwe na baiskeli lakini wameshindwa kujali kabisa kuhusu mimi, inaonekana mimi hata nikigongwa na baiskeli zao, kwao ni sawa tu.

Hakuna anaejali kabisa uwepo wangu, nimesahaulika hadi kwenye nyumba za ibada. Hebu zitazame kengere kwenye makanisa, hebu tazama adhana msikitini, hawajali lolote kuhusu uwepo wangu, inaonekana hata nisiposikia milio ya kengere au adhana, kwao ni sawa tu.

Hebu tazama mahubiri mpaka kwenye makanisa ya mitume na manabii, hawajishughulishi kabisa na uwepo wangu, wanaweka wakalimani hadi wa lugha za kiingereza na kifaransa lakini hawajishughulishi kuweka wakalimani wa lugha ya ishara.

Hebu tazama jamani, namba za huduma kwa wateja za makampuni ya simu, zote ni simu za mdomo, maana hawajui kama mimi pia ni mteja wao na ninakutana na changamoto kama wanazopata wateja wao wengine.

Hebu tazama simu za dharura ya moto, gari la wagonjwa, polisi, TANESCO nk. zote ni simu za mdomo, ina maana hawajui kama na mimi nipo Dunia wanayoishi wengine, majanga yanayowapata wengine ndiyo yanaweza kunipata na mimi.

Wameamua kuniletea jehanamu Duniani kabla hata sijafa. Ona sasa, mpaka natamani ningebadilishana ulemavu wangu huu na maalbino, maana wao kidogo serikali inawajali, ingawa serikali ilianza kuwajali baada ya kuibuka matukio ya kuuwawa.

Tazama, licha ya uzalendo wangu kwa nchi yangu siruhusiwi kujiunga hata na jeshi la kujenga taifa.

Tazama, hata siku nikinunua gari sitaruhusiwa kupewa leseni ya udereva.

Hivi ni kweli, watu, hawajui kipi wafanye ili kunisaidia na mimi niishi kama binadamu wengine wanavyoishi.

Hivi katika karne hii ya sayansi na teknolojia wanashindwaje kuvumbua vifaa sawa na honi, kengere, ving'ora nk vya kunisaidia ili niishi maisha ya kawaida kama binadamu wengine;

Hivi Bunge linashindwaje kutunga sheria za kuwalazimisha watoa matangazo kutoa matangazo kwa kuwajumuisha wakalimani wa lugha ya ishara;

Hivi Bunge linashindwaje kutunga sheria za kulazimisha uwepo wa wakalimani wa lugha ya ishara kwenye matukio kama vile harusi, kampeni, misiba nk;

Hivi Bunge linashindwaje kutunga sheria za kulazimisha uwepo wa wakalimani wa lugha ya ishara kwenye vituo vya kutolea ushauri nasaha;

Hivi Bunge linashindwaje kutunga sheria za kulazimisha uwepo wa wakalimani wa lugha ya ishara kwenye vituo vyote vya mabasi;

Hivi Bunge linashindwaje kutunga sheria za kulazimisha kwepo kwa wakalimani wa lugha ya ishara kwenye vituo vyote vya polisi;

Hivi watunga mitaala wanashindwa nini kuzifanya lugha ya ishara ifundishwe kuanzia shule za msingi;

Hivi Bunge linashindwaje kutunga sheria za kuwataka watumishi kwenye taasisi za umma kufundishwa lugha ya ishara.

Hivi serikali inashindwa vipi kutoa ufadhili kwa watu au kampuni zinazotengeneza vifaa vya kunisaidia kuishi kama wanavyoishi binadamu wengine.

Mbona haya yote yako ndani ya uwezo wa serikali, sasa kwa nini hawataki kuyatekeleza, au labda wananiona mimi kutokuwa binadamu kamili.

Basi naiomba serikali initangaze, tena kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la serikali, mimi sio binadamu kamili au kama wanaona ugumu sana kutangaza hivyo,wanitangaze kuwa mimi ni binadamu kivuli.
 
Sawa bwana tutakutangaza kuwa wewe ni kivuli
 
Gh
 
Back
Top Bottom