Hivi kwanini sisi binadamu tukipata mafanikio kidogo tunavimba sana?

Top gun maverick

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
2,032
2,633
Habari za asubuhi wana JF poleni na majukumu ya kutafuta mkate wa kila siku ilimradi njia ya kwenda msalani isiote nyasi.

Husika kwenye mada iliopo hapo juu sijui ni kwanini sisi binadamu hasa tuliotokea maisha magumu yaani mtu kanunua gari tu, kajenga nyumba au kapata kazi basi ni vurugu huko mtandaoni yaani ni kero zile show off.

Mfano mzuri kuna rafiki yangu kasota sana mtaa kapata bahati ya kwenda polisi sasa kamaliza juzi aisee anavyovimba huko what's up status ni balaa mpaka nasema hivi ni nature ya binadamu wote au?

Nawasilisha wakuu.
 
Habari za asubuhi wana Jf poleni na majukumu ya kutafuta mkate wa kila siku ilimradi njia ya kwenda msalani isiote nyasi.

Husika kwenye mada iliopo hapo juu sijui ni kwanini sisi binadamu hasa tuliotokea maisha magumu yaani mtu kanunua gari tu,kajenga nyumba au kapata kazi basi ni vurugu huko mtandaoni yaani ni kero zile show off.
Mfano mzuri kuna rafiki yangu kasota sana mtaa kapata bahati ya kwenda polisi sasa kamaliza juzi aisee anavovimba huko what's up status ni balaa mpaka nasema hivi ni nature ya binadamu wote au?

Nawasilisha wakuu.
Naona wewe ndo una tatizo.
Tafsiri yako ya mafanikio ni hovyo na una wivu ila hujui ka unao. Fanya kazi mkuu na zingatia mambo yako huyo unaemuita rafiki sidhani kama ni rafiki yako. Wewe ni mnafiki!
 
Mwache avimbe aiseeh maana kipindi anapitia msoto hukua nae na pengine alitengwa na ndugu na jamaa na kumwona si lolote si chochote. Lakini Mungu si athumani kapata ndoto zake Mwache tena mtu kama huyo mpongeze kabisa.
Ni nature ya kiafrika kufurahia mtu akipitia changamoto.

NB; mimi mwenyew hapa sasa hivi nime LAY LOW siku nikija kufumuka mara leo nipo Sychelles, China, Bangkok, Scandnavian countries Aiseeh mbona wale waliosema jamaa hatoboi watakoma..🤣🤣🤣

Amini nakuambia kwa jamii zetu za kiafrika zinafurahia sana ukiwa matatizon kuliko kuyafurahia mafanikio yako. Hata hapo wewe unapoona umefika kuna kundi kubwa la watu wanapenda ushuke.

Mwache jamaa afurahi kipindi yupo kwenye msoto alikimbiwa na watu.
 
Mwache avimbe aiseeh maana kipindi anapitia msoto hukua nae na pengine alitengwa na ndugu na jamaa na kumwona si lolote si chochote. Lakini Mungu si athumani kapata ndoto zake Mwache tena mtu kama huyo mpongeze kabisa.
Ni nature ya kiafrika kufurahia mtu akipitia changamoto.

NB; mimi mwenyew hapa sasa hivi ni LAY LOW siku nikija kufumuka mara leo nipo Sychelles, China, Bangkok, Scandnavian countries Aiseeh mbona wale waliosema jamaa hatoboi watakoma..🤣🤣🤣

Amini nakuambia kwa jamii zetu za kiafrika zinafurahia sana ukiwa matatizon kuliko kuyafurahia mafanikio yako. Hata hapo wewe unapoona umefika kuna kundi kubwa la watu wanapenda ushuke.

Mwache jamaa afurahi kipindi yupo kwenye msoto alikimbiwa na watu.
Duu basi nimeelewa
Doto magari anasema.. "asiye faa kafaa
 
Habari za asubuhi wana Jf poleni na majukumu ya kutafuta mkate wa kila siku ilimradi njia ya kwenda msalani isiote nyasi.

Husika kwenye mada iliopo hapo juu sijui ni kwanini sisi binadamu hasa tuliotokea maisha magumu yaani mtu kanunua gari tu,kajenga nyumba au kapata kazi basi ni vurugu huko mtandaoni yaani ni kero zile show off.
Mfano mzuri kuna rafiki yangu kasota sana mtaa kapata bahati ya kwenda polisi sasa kamaliza juzi aisee anavovimba huko what's up status ni balaa mpaka nasema hivi ni nature ya binadamu wote au?

Nawasilisha wakuu.
Ni ulimbukeni tu kwa baadhi ya watu.

Najua watu wengi waliohustle na kutusua ila hawajioneshi kupitia mafanikio yao
 
Back
Top Bottom