Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana...

Eehe yamekuwa haya.....!
kila baya likitokea ni upinzani tu
hivi wananchi kwani hatuna akili? au kwani tumeridhika?
 
Kumwagiwa Tindikali kwa Saed Kubenea
Kifo cha Horace Kolimba - inasemekana ni kwa njia ya sumu.
Kifo cha marehemu Prof. Juan Mwaikusa
Kuchinjwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA arumeru siku kadhaa baada ya uchaguzi
Kifo cha marehemu Imran Kombe
Kuvamiwa na Kupigwa kwa mpendazoe kipindi yupo na chama cha CCJ.
Jaribio la kutaka kumuua mbunge wa Ilemela Ndg. Highness Kiwia.
Kupotea kwa Shabiki wa Chadema kule igunga siku chache baada ya uchaguzi.
Kuuawa kwa wazanzibar kabla ya muafaka wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Haya yote ni baadhi ya mambo ambayo yanamtizamo hasi kwa umma dhidi ya serikali ya chama cha mapinduzi, wahanga wote wa haya matukio wana kitu kimoja common - kupigania mabadiliko kwa uwazi pamoja na kuikosoa serikali kwa baadhi ya mambo mbalimbali ambayo hawakuridhishwa nayo.

Hili na ulimboka na lenyewe lina tafsiri nyingi sana.
....niko kwenye kifo cha horace kolimba....taarifa ya uchunguzi wa kitaalam iliyofanywa na wataalam, waliochaguliwa na familia ya marehemu haikusema lolote juu ya sumu...!
 
Haya ni mawazo ya wana CCM ili kujivua na uovu waliomtendendea Dr. Ulimboka
Katika pitapita zangu, nimedokezwa kuwa mfululizo huu wa migomo na maandamano ni kufanikisha mpango wa ki haini wa kutaka kuiangusha serikali iliyoko madarakani. Tulianza kushuhudia maandamano na kuambiwa kama nchi haitatawalika, nadhani ilitakiwa iwe kama yale ya arab spring. Lakini Mungu bariki mbinu hii ikabuma.

Ikaja mgomo wa wafanyakazi, nao ukabuma. Ukaja mgomo wa madaktari kupitia interns...huu ulisumbua kiasi mpaka ukang'oa vigogo kule wizarani lakini ukapita. Sasa mgomo huu mwingine kwa kisingizio kile kile cha hali bora za madaktari. Cha kushangaza wanaoshabikia zaidi migomo yote hii ni wale walioanzisha maandamano.

Nashawishika kuamini jamaa yangu aliyenin'gata sikio kuwa mpango huu unalenga kutaka kuifanya nchi isitawalike, nimedokezwa kuwa waalimu nao wameshawishiwa kugoma.

Sasa kama nadharia hii ni kweli, basi masikini dr. Uli jamaa zako wenyewe ndio wamekutia jiti. Na jamii iaminishwe kama ni jeshi la polisi and so serilkali ili umma woote uanze kuichukia serikali na kuiangusha. Dr. Uli adui yuko chumbani kwako, usimtafute mchawi.

I was just thinking very loud, sitaki nkuamini hata kidogo kam serikali kupitia jeshi la polisi could be dare to do this.

Kuna silku ukweli utadhihiri.

K.
 
Ana habari gani huyo?

Habari awe nayo Ritz; ni kitu gani kama si UBUNIFU wa tangu leo asubuhi kumtafutia Dr Ulimboka 'Mbaya Mpya Mwenye Uwezo wa Kuteka Kijeshi' ili mhusika halisi aliyefanya mambo bila kutafakari apate kubaki salama.

Too late na narudia kwamba ni TOO LATE for any cover-up in this instance. DNA info zote zilishachukuliwa saa nyiiiiingi ajabu.

Na satelite pictures and voice signals za ndani y wiki mbili hadi leo are SO DAMNING if not overwelming!!! Ehe, hebu endelea kutuletea theories nyinginezo za kule CCM Barabara ya Lumumnba hapa tukasome.

ritz mwaga habari
 
Katika pitapita zangu, nimedokezwa kuwa mfululizo huu wa migomo na maandamano ni kufanikisha mpango wa ki haini wa kutaka kuiangusha serikali iliyoko madarakani. Tulianza kushuhudia maandamano na kuambiwa kama nchi haitatawalika, nadhani ilitakiwa iwe kama yale ya arab spring. Lakini Mungu bariki mbinu hii ikabuma.

Ikaja mgomo wa wafanyakazi, nao ukabuma. Ukaja mgomo wa madaktari kupitia interns...huu ulisumbua kiasi mpaka ukang'oa vigogo kule wizarani lakini ukapita. Sasa mgomo huu mwingine kwa kisingizio kile kile cha hali bora za madaktari. Cha kushangaza wanaoshabikia zaidi migomo yote hii ni wale walioanzisha maandamano.

Nashawishika kuamini jamaa yangu aliyenin'gata sikio kuwa mpango huu unalenga kutaka kuifanya nchi isitawalike, nimedokezwa kuwa waalimu nao wameshawishiwa kugoma.

Sasa kama nadharia hii ni kweli, basi masikini dr. Uli jamaa zako wenyewe ndio wamekutia jiti. Na jamii iaminishwe kama ni jeshi la polisi and so serilkali ili umma woote uanze kuichukia serikali na kuiangusha. Dr. Uli adui yuko chumbani kwako, usimtafute mchawi.

I was just thinking very loud, sitaki nkuamini hata kidogo kam serikali kupitia jeshi la polisi could be dare to do this.

Kuna silku ukweli utadhihiri.

K.
Vichipkizi VGA TISS Bwana...Viko kizamaaaani? Utafikiri vimezaliwa Aldeia Msumbiji?
 
Ww v...na huyo aliyepigwa pale muhimbili na kujitambulisha km mkuu wa police pale salender baada ya kugundulika kuwa alikuwa anaongea na cm siniliwaambia tumchome sindano ya sumu ili afe' ni nani,c o serikali?...au hujui kinachoendelea ww!km hujui uliza uckurupuke

KOva alimsafisha eti yule askari alitumwa kwenda kumlinda Dr Ulli pale muhimbili... too late...
 
Kumwagiwa Tindikali kwa Saed Kubenea
Kifo cha Horace Kolimba - inasemekana ni kwa njia ya sumu.
Kifo cha marehemu Prof. Juan Mwaikusa
Kuchinjwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA arumeru siku kadhaa baada ya uchaguzi
Kifo cha marehemu Imran Kombe
Kuvamiwa na Kupigwa kwa mpendazoe kipindi yupo na chama cha CCJ.
Jaribio la kutaka kumuua mbunge wa Ilemela Ndg. Highness Kiwia.
Kupotea kwa Shabiki wa Chadema kule igunga siku chache baada ya uchaguzi.
Kuuawa kwa wazanzibar kabla ya muafaka wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Haya yote ni baadhi ya mambo ambayo yanamtizamo hasi kwa umma dhidi ya serikali ya chama cha mapinduzi, wahanga wote wa haya matukio wana kitu kimoja common - kupigania mabadiliko kwa uwazi pamoja na kuikosoa serikali kwa baadhi ya mambo mbalimbali ambayo hawakuridhishwa nayo.

Hili na ulimboka na lenyewe lina tafsiri nyingi sana.

...hilo la kuuawa kwa wazanzibar kabla ya muafaka ulioleta serikali ya umoja wa kitaifa ....tuseme bila ya kutafuna maneno...ni matokeo ya "kujifanya wanajua kumbe wanaungua na jua"....mzee mwenye hekima na mwenye kuzijua siasa za zanzibar, nje ndani, aliwaambia mapema...mwaka 1995, mara tu baada ya uchaguzi, kuwa ili pawepo na amani na utulivu wa kisiasa ktk zanzibar, basi na iundwe serikali ya mseto...wakajifanya ati mafundi....!
 
Huyo hana habari zozote ni uzushi tuu ...si hao hao hana lolote wanahangaika sasa kutunga story zao ili kujaribu kupoteza ukweli !! kmnn zao .......mmeumbuka na sasa ndiyo kila kitu mwaaa.... !! Safari hii lazima mdondoke airport kwa mawazo...!
 
Kwa mtazamo wangu binafsi huyo mama hata kama anaumafia wake hawezi kuwa na ujasiri wa kupanga mauaji kwa njia ya jinsi hiyo.
Naungana na wachangiaji wengine kwamba mipango ya kumpoteza DR. itakuwa ni mipango kutoka juu zaidi. Nina mashaka sana kwamba Mr Pinda anahusika moja kwa moja katika hili.
Mtazamo binafsi "HUENDA" Amiri Jeshi mkuu amebariki tendo hili na vijana waliotumwa kufanya kazi hiyo Roho zao zimekuwa za kibinadamu zaidi kwani hawakupenda kumtoa roho DR badala yake wameamua kumnyanyasa na kumwacha akiwa hai ili kuwaumbua wahusika wakuu wa jambo hilo.
Subira yavuta heri na siku ya kufa nyani mti yote huteleza..TUTAPATA MAJIBU..!!

Naomba tulejee wiki ambayo watanzania walikuwa wanajadili matokeo ya uchaguzi wa arumeru je nini kilitokea.

Tulipatwa na habari za msiba wa marehemu kanumba

Sasa tuko tunajadili mgomo wa madaktari na implication zake kwa maisha yetu,guess what we end up with,another beautiful headline.

SIASA NI MCHEZO MCHAFU
 
Katika pitapita zangu, nimedokezwa kuwa mfululizo huu wa migomo na maandamano ni kufanikisha mpango wa ki haini wa kutaka kuiangusha serikali iliyoko madarakani. Tulianza kushuhudia maandamano na kuambiwa kama nchi haitatawalika, nadhani ilitakiwa iwe kama yale ya arab spring. Lakini Mungu bariki mbinu hii ikabuma.

Ikaja mgomo wa wafanyakazi, nao ukabuma. Ukaja mgomo wa madaktari kupitia interns...huu ulisumbua kiasi mpaka ukang'oa vigogo kule wizarani lakini ukapita. Sasa mgomo huu mwingine kwa kisingizio kile kile cha hali bora za madaktari. Cha kushangaza wanaoshabikia zaidi migomo yote hii ni wale walioanzisha maandamano.

Nashawishika kuamini jamaa yangu aliyenin'gata sikio kuwa mpango huu unalenga kutaka kuifanya nchi isitawalike, nimedokezwa kuwa waalimu nao wameshawishiwa kugoma.

Sasa kama nadharia hii ni kweli, basi masikini dr. Uli jamaa zako wenyewe ndio wamekutia jiti. Na jamii iaminishwe kama ni jeshi la polisi and so serilkali ili umma woote uanze kuichukia serikali na kuiangusha. Dr. Uli adui yuko chumbani kwako, usimtafute mchawi.

I was just thinking very loud, sitaki nkuamini hata kidogo kam serikali kupitia jeshi la polisi could be dare to do this.

Kuna silku ukweli utadhihiri.

K.

I am sorry to say your argument is baseless,based on hearsay. And this line of thinking is totally misguided

Kama serikali kuangushwa inajuangusha yenyewe kwa madudu inayofanywa. Je unamfahamu nani mwenye kampuni ya Kagoda? Nani walifaidi kwenye michongo kama Meremeta,Radar,Ndege ya Rais, Deep Green? Kwa nini watu wanaendelea kuiba rasilimali fedha wapo na hawachukuliwi hatua? Je mwalimu anayedai 2,000,000/= akaandikiwa hundi ya laki mbili(200,000), huku serikali ikilipa 2,000,000/= na 1,800,000/=(inakwenda tumbo street) aliyetayarisha bado yupo hapo vipi?

Kiongozi kashiriki kwenye rushwa ya radar pesa imeonekana kule Jersey Islands na anaendelea kupeta hapo vipi? Je matumizi mabovu ya rasilimali fedha yanayoendelea ndani ya serikali yamesababisha na hao wanaofanya mgomo au maandamano? Mambo yanayofanywa na serikali ni machafu sana na hayana uzalendo na mchanganyiko wa hayo yote ndio yanayozaa haya tuonayo sasa. Haya hayakutokea kwa bahati mbaya. Kwa nini? Kwa sababu zama zimebadilika,watu wanaelewa zaidi sasa kuliko miaka ya nyuma.Watu wanajiuliza,kwa nini yeye akiumwa akatibiwe Appolo India,lakini mimi ugonjwa uleule nitibiwe Mwananyamala? Kwa nini rasilimali za nchi zinagawanywa au wanagawana wachache tu,ila sisi tukidai haki yetu tunaambia serikali haina fedha? Kwa nini yeye anaweza kumpeleka mwanae shule kule Canada,Uingereza nk lakini mimi uwezo ni kumpeleka shule ya kata? Maswali yapo mengi na haya ndio yanayoleta kizaazaa chote hiki.

Serikali inachoweza kufanaya ni kutengeneza utaratibu wa kuwageuza watu wenye kujiuliza maswali haya wawe na fikra kama za zamani kwa kutengeneza teknologia itakayorudisha muda nyuma. Au serikali ijirudi iseme wizi,ubadhirifu,u-mungu mtu, kiburi cha viongozi,ubabaishaji, naizesheni sasa basi. Je lipi kati ya haya mawili ni rahisi?
 
Back
Top Bottom