Kikwete: Uamuzi wa Dodoma kuwa Makao Makuu na Ujenzi wa Ikulu haukuwa wa mtu mmoja!

Kuna uzi uletwa humu ukiwa na picha la jengo wakisema ile ndio ikulu, watu wakamtukana sana Magu sasa leo wanaumbuka tena.
Kiukweli chadema ni fungu la kukosa
Walichokosoa ni design ya jengo! BTW kuna faida gani ya kuhamia Dodoma ukilinganisha na gharama zote tunazoingia nchi maskini kama yetu? Hebu nielimisha kwa kuni-orodheshea faida za kuhamia Dodoma.
 
Heshima kwenu Wakuu wangu,

Leo Taifa tumeweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.

Ikulu ambayo itafanana na ile iliyopp Dar Es Salaam kwa kila kitu hadi upana wa ngazi. Tofauti ni moja tu kwamba ile ya Dodoma ina underground.

Lakini katika waliohutubia, Makongoro Nyerere na Jakaya Kikwete ndo wamefanya watu kusahau machungu ya maisha na hasira za Corona kwani wamechangamsha Ukumbi japo hata ambaye hakucheka alitabasamu kwa furaha.

Rais Mstaafu Kikwete alipo simama kuhutubia alianza na neno "Mambo"? Nikaona kila mtu hata wale Maafande wa JKT wanaojenga Ikulu wakavua kofia na kuepeperusha hewani kwa shangwe na Vifijo.

Kwenye hotuba ya rais Mstaafu Jakaya Kikwete nimegundua hili:

1. Kikwete ameshangiliwa sana na vijana wa JKT kuliko rais yoyote mstaafu

2. Kikwete amezungumzia kuwa Mwalimu hakuamua tu Makao Makuu yahamie Dodoma yeye mwenyewe, Ulikuwa ni uamuzi wa kidemokrasia na uamuzi shirikishi. Hapa aliweka msisitizo wa uongozi shirikishi na demokrasia (collective decision-making)

3. Alieleza uamuzi wake kuwa Makazi ya Rais na ofisi zijengwe Chamwino. Mawazo ya zamani ni kuwa Ikulu ijengwe Chamwino halafu ofisi ya Rais iwe Chimwaga, hiyo isingekuwa salama Rais asafiri 40km kila siku kutoka Chamwino kwenda Chimwaga na kurudi. Hii imedhihirisha kuwa uamuzi wa kuhamia Dodoma ni mchakato ambao kila Rais alikuwa na mchango wake, siyo maono ya kiongozi mmoja peke yake.

Wasubiri MATAGA waje na kipeperushi kua masterplanner wa kuwa na ikulu dodoma ni mzee wa chattle!
 
Zile kelele, vifijo na nderemo zilizosikika alipokuwa akienda kusema neno inaonesha ni kwa jinsi gani alivyokuwa akikubalika hata Rais msataafu Benjamin Mkapa katikati ya hotuba yake alisema JK ni kati ya viongozi wanaopendwa sana...
IMG_20200531_081824.jpg
IMG_20200531_081828.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikwete n Rais anayependwa kuliko wote hii haipingiki n mtu mwenye nyota ya watu ILA KWA RAIS Magufuli atabaki kuwa Rais bora kuwahi kutokea na mwenye uthubutu mkubwa ambaye hajatokea Tanzania vitabu vitamwandika na atakuja kukumbukwa milele
 
Amefika hapo alipo kwa sababu hatuna mfumo thabiti wa kuandaa na kuchuja viongozi.

Tungekuwa nao mfumo huo, asingefika hapo.
Ni kweli. Halafu Tanzania kwa mwananchi wa kawaida kujua tabia na vipaji halisi vya kiongozi ni ngumu sana kwani wengi ni wanafiki. Wanapokuwa ngazi za chini huficha makucha yao na maamuzi mengi wanayotoa husoma kwanza upepo unaelekea wapi. Hapa ndipo tulitakiwa tuwe na idara ya usalama wa Taifa imara ili iwasome viongozi kwa ukaribu.

Nakumbuka wakati wa Kikwete wakati watu wanalaumu sana aliwezaje kuingia Ikulu, wewe ukasema tusishangae tukaja kupata rais mwingine mbovu kuliko Kikwete.

Wengi tulikupinga na kusema Kikwete alikuwa kilele cha rais mbovu na hatutarajii atokee mwingine kumzidi. Kinachotokea leo kinaonyesha ulikuwa sahihi.

Mpaka sasa nashangaa Magufuli aliwezaje kuvuka mpaka kuwa na PhD wakati kichwani ni mwepesi namna hiyo. Mazungumzo na hotoba zake zote hazionyeshi kama ni mtu mwenye elimu.

Kama unavyosemaga jamaa kweli ni mzinga wa country pumpkin ila kinachonishangaza zaidi mbona elimu haikuweza kuondoa hiyo hali ya u-country pumpkin au n angalau kuipunguza?
 
Veeeery true. Kikwete is the best among the worst. Katikati ya CCM yetu iliyooza Kikwete ndio ana afadhali kidogo.

Yeye alimnunua Dr. Slaa tu kwa kuwa alikuwa ni Asset. Hawa vilaza kina Meko wananunua mpaka kina Mbatia, Selasini, Juakali na madiwani..

Huku ni kuchezea kodi za wananchi.
Vipi CHADEMA waliponunuliwa na Lowassa, alikuwa asset au liability?
 
Kikwete n Rais anayependwa kuliko wote hii haipingiki n mtu mwenye nyota ya watu ILA KWA RAIS Magufuli atabaki kuwa Rais bora kuwahi kutokea na mwenye uthubutu mkubwa ambaye hajatokea Tanzania vitabu vitamwandika na atakuja kukumbukwa milele
Yes mzee hatosaulika atabaki kwenye kumbumbuku za nchii hii hizo legacy zake za SGR,na kule stigila zitambakisha kwenye kumbukumbu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikulu dodoma lilikuwa ni wazo la kizazi cha wakati ule na si tija kwa kizazi na mazingira ya Sasa halijazingatia suala la vipaumbele vya kiuchumi
 
Heshima kwenu Wakuu wangu,

Leo Taifa tumeweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.

Ikulu ambayo itafanana na ile iliyopp Dar Es Salaam kwa kila kitu hadi upana wa ngazi. Tofauti ni moja tu kwamba ile ya Dodoma ina underground.

Lakini katika waliohutubia, Makongoro Nyerere na Jakaya Kikwete ndo wamefanya watu kusahau machungu ya maisha na hasira za Corona kwani wamechangamsha Ukumbi japo hata ambaye hakucheka alitabasamu kwa furaha.

Rais Mstaafu Kikwete alipo simama kuhutubia alianza na neno "Mambo"? Nikaona kila mtu hata wale Maafande wa JKT wanaojenga Ikulu wakavua kofia na kuepeperusha hewani kwa shangwe na Vifijo.

Kwenye hotuba ya rais Mstaafu Jakaya Kikwete nimegundua hili:

1. Kikwete ameshangiliwa sana na vijana wa JKT kuliko rais yoyote mstaafu

2. Kikwete amezungumzia kuwa Mwalimu hakuamua tu Makao Makuu yahamie Dodoma yeye mwenyewe, Ulikuwa ni uamuzi wa kidemokrasia na uamuzi shirikishi. Hapa aliweka msisitizo wa uongozi shirikishi na demokrasia (collective decision-making)

3. Alieleza uamuzi wake kuwa Makazi ya Rais na ofisi zijengwe Chamwino. Mawazo ya zamani ni kuwa Ikulu ijengwe Chamwino halafu ofisi ya Rais iwe Chimwaga, hiyo isingekuwa salama Rais asafiri 40km kila siku kutoka Chamwino kwenda Chimwaga na kurudi. Hii imedhihirisha kuwa uamuzi wa kuhamia Dodoma ni mchakato ambao kila Rais alikuwa na mchango wake, siyo maono ya kiongozi mmoja peke yake.

JK ni mtu wa kupiga madongo live ila utakuja kuelewa baadae kwamba kumbe alinipiga DONGO tofauti na Vijembe vya "MTU FURANI" analenga hapo hapo na ni Direct.
 
Ni kweli. Halafu Tanzania kwa mwananchi wa kawaida kujua tabia na vipaji halisi vya kiongozi ni ngumu sana kwani wengi ni wanafiki. Wanapokuwa ngazi za chini huficha makucha yao na maamuzi mengi wanayotoa husoma kwanza upepo unaelekea wapi. Hapa ndipo tulitakiwa tuwe na idara ya usalama wa Taifa imara ili iwasome viongozi kwa ukaribu. Nakumbuka wakati wa Kikwete wakati watu wanalaumu sana aliwezaje kuingia Ikulu, wewe ukasema tusishangae tukaja kupata rais mwingine mbovu kuliko Kikwete...
Kwanza shukurani sana kwa kukumbuka maneno yale. Sikutegemea kama kuna watu wanakumbuka.

Nilisema vile kwa kuangalia kwamba kila utawala mbovu unavyokuja, unashusha standards za commonly accepted behavior. Wanaofuata wanashusha zaidi.

Hebu fikiria uje upate rais Makonda au hao watu wa caliber yake.

Tutarudi kulekule kusema "bora hata Magufuli".

Siyo kwa sababu Magufuli ni mzuri sana.

Bali kwa sababu quality ya uongozi ikizidi kushuka, hata mbaya anaonekana afadhali akilinganishwa na mbaya zaidi.
 
Amefika hapo alipo kwa sababu hatuna mfumo thabiti wa kuandaa na kuchuja viongozi.

Tungekuwa nao mfumo huo, asingefika hapo.
Kwa upande mwingine, unapoona mtu kama Trump alifanikiwa kuwa Rais na kuendelea kuwa licha ya kashfa nyingi zilizomwandama baada ya kuteuliwa, ndipo mtu unapoweza kuhitimisha - hakuna mfumo wa kiutawala uliothabiti na hata kuwa mfano.

Hebu fikiri tu kwa mtu kama Boris Johnson kuwa PM , ama kwa Putin kuendelea kuwa Rais wa kudumu... Lililo bora na nono kwa huyu, kwa mwingine sumu!

Watu wengi wanapenda kudanganywa.

Hapo ndipo mwanzo wa tatizo.
 
Pia ndiye Rais anayejua kuongea na kupangilia maneno yake kuliko wote hadi kimuonekano wa urais Kikwete bado anampiga bao Meko
Huyu si aliitwa rais dhaifu haijawahi kutokea tena
Ni vasco da gama
Leo lulu
 
Back
Top Bottom