Kifanyike kipi kuboresha Mikopo kausha damu iwe na manufaa kwa wakopaji?

Half american

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
27,684
72,138
Habari wakuu, nmeona kipindi cha ripoti maalum ITV kuhusu mikopo kausha damu.

Malalamiko ni mengi sana licha ya kuwepo kwa uhitaji wa mikopo na wengine kufikia hatua ya kuomba hii mikopo isitishwe.

Dhamana zinazowekwa na kiasi cha mkopo haviendani kabisa.

Kwa maelezo ya wanawake wengi wanaochukua mikopo wanadai ina madhara makubwa kuliko faida, na wengi wanachukua bila kuwashirikisha waume zao, hii ni hatari zaidi.

Serikali inajinadi kutoa mikopo kwa makundi mengi ya kijamii hasa kwa wanawake lakini ina mlolongo mrefu na ndio chanzo cha wengi kukimbilia kausha damu kupata mkopo kwa haraka.

Kipi kifanyike kuboresha hii mikopo inayoonekana inawaumiza wengi na uhitaji wake bado ni mkubwa?

Taasisi za fedha kama mabenki hamuoni hii fursa kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwafikia watu wa matabaka ya chini kupitia vikundi? (tatizo hapa ni mlolongo mrefu mpaka kupata mkopo)

Wanawake wanadhalilika sana na hii mikopo ya kausha damu. Mtu una mikopo zaidi ya minne kausha damu lazima utadhalilika tu, huwezi kutoka shimoni kwa kuendelea kuchimba shimo.

NB: DAWA YA DENI NI KULIPA.

Screenshot_20240222_113558.JPG
 
waache tu kukopa utakuwa mwishonwake tatizo lipo Kwa wakopaji wakibanwa na matatizo wanaenda kimyakimya BAADA ya kutuma vibaya wanaanza kuitaka serikali ikomeshe mikopoo hiyo
 
Huko ni kufeli Kwa serikali Kuna mikopo ya halmashauri wengi hawaijui hata mashari yake pia lazima yazingatie hali ya wakopaji. Lakini vipi taasisi za serikali zinazo simamia mambo ya fedha
 
Wakati wa kukopa watu huwa very anxious; hata kujiridhisha huona kama vile wanapoteza muda hivyo kujikuta wanakopa hata kwenye maeneo ambayo hayana usajili na hayako kisheria.

Pia kuna hulka ya wakopaji kukopa hovyo-hovyo. Unakuta mtu ana mikopo sehemu zaidi ya moja bila sababu ya msingi kulingana na aina ya biashara anayofanya. Hii upelekea kuelemewa na mikopo na hivyo kufanya marejesho inavyotakiwa (Na hapo ndipo kelele na malalamiko huwa mengi wakati tatizo ni mkopaji).

Wako pia wanaodhani wanaenda kukopa kwenye NGO (Hawa ni wale wapenda vya mteremko). Ukikopa ni sharti ulipe. Hili utaliona pia hata kwa baadhi ya wakopaji wanaopata mikopo ya Halmashauri (Kurudisha huwa ni changamoto).
 
Tatizo kubwa la mikopo ya Kausha damu ni shida zinazo wakabili wananchi na haswa watumishi wa umma ambao ndio wahanga wakuu wa kukaushwa damu.

ushauri wangu kwa serikali ni.
wizara ya Fedha/Hazina itoe mikopo nafuu kwa watumishi wake ili ijikwamue kimaisha.

Benki ya NMB ambayo ndio Benki pekee inayo hudumia mishahara ya watumishi hivyo haina budi kupunguza riba za mikopo.
 
Mbona mwigulu na nape wanarukaruka hoja. Mikopo kausha damu ipo, sio ya kwenye simu tu hata wale wenye ofisi za mikopo uchochoroni wapo. Hao wa uchochoroni ukiacha makampuni ya simu wana leseni ya kutoa mikopo?
 
Riba 50% mtu anashida anakubali tu shida ikiisha ndio ubishi unaanza wa kulipa, wengine wanafikia kudhalilishwa
 
Jasho linawatoka waziri wa fedha na waziri wa TEHAMA, wamejibu hoja kwa kurukaruka viunzi, majibu yao hayajaridhisha na hakuna azimio bunge lililopitisha kuhusu kadhia ya mikopo kausha damu. Spika kaamua ngoma hii ijadiliwe tena mwezi wa tisa, labda serikali itakuja na majibu ya kuridhisha. Kumbe hawa jamaa wakibanwa mbavu kidogo wanakosa cha kujibu na kuanza kurukaruka, ujanja unawaaishia.
 
Habari wakuu, nmeona kipindi cha ripoti maalum ITV kuhusu mikopo kausha damu.

Malalamiko ni mengi sana licha ya kuwepo kwa uhitaji wa mikopo na wengine kufikia hatua ya kuomba hii mikopo isitishwe.

Dhamana zinazowekwa na kiasi cha mkopo haviendani kabisa.

Kwa maelezo ya wanawake wengi wanaochukua mikopo wanadai ina madhara makubwa kuliko faida, na wengi wanachukua bila kuwashirikisha waume zao, hii ni hatari zaidi.

Serikali inajinadi kutoa mikopo kwa makundi mengi ya kijamii hasa kwa wanawake lakini ina mlolongo mrefu na ndio chanzo cha wengi kukimbilia kausha damu kupata mkopo kwa haraka.

Kipi kifanyike kuboresha hii mikopo inayoonekana inawaumiza wengi na uhitaji wake bado ni mkubwa?

Taasisi za fedha kama mabenki hamuoni hii fursa kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwafikia watu wa matabaka ya chini kupitia vikundi? (tatizo hapa ni mlolongo mrefu mpaka kupata mkopo)

Wanawake wanadhalilika sana na hii mikopo ya kausha damu. Mtu una mikopo zaidi ya minne kausha damu lazima utadhalilika tu, huwezi kutoka shimoni kwa kuendelea kuchimba shimo.

NB: DAWA YA DENI NI KULIPA.

View attachment 2912031
Watu wafanye ibada sana na kufuata mafundisho ya dini ili waogope yote waliyokatazwa ikiwemo riba haramu nyoookoooniiinaaa.
 
Kwakweli umasikini wa fikra mbaya sana, sijui niseme ni tamaa za kutaka kunufaika Kwa haraka zinawafanya watu waingie mikopo kausha damu, sijui nisemeje mpk watumishi nao wanaingia mkenge huo. Siku moja Niko kwenye ATM nataka nitoe pesa basi kunamdau tayari yupo ndani anatoa pesa, aisee nilisubiri karibia dakika ishirini haitoki ikabidi nimwambie mlinzi aliyekaribu huyo mdau hebu msaidie kama hawezi kutoa pesa watu tunaharaka. Cha kunishtua ni pale niliposikia mlinzi anamwambia bado Kadi ngapi hujatoa pesa? Ikajibiwa bado Kadi 13 tu. Du ikabidi hata ule uharaka wa kutaka kutoa pesa ukapungua ikabidi nimhoji mlinzi mdau Kadi zote anamiliki yeye, nikajibiwa hizo ni Kadi za watumishi waliokopa kwahiyo aliyekopesha Huwa anabaki na Kadi kazi yake kusosomora pesa tu mshahara unapotoka
 
Back
Top Bottom