NADHARIA Kevin Carter alijiua baada picha ya kusikitisha aliyompiga mtoto akiwindwa na Tai kumpatia tuzo ya Picha bora (Pulitzer Prize)

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Kevin Carter alikuwa ni mpiga picha, sasa katika kazi zake alifanikiwa kufika Sudan na alikuta eneo fulani nchini Sudan likikabiliwa na njaa kali sana.

Wakati anaendelea kuchukua matukio katika picha, alikutana na mtoto dhoofu mwenye utapiamlo aliyekuwa akikabiliwa na njaa kali pamoja na kiu, cha kusikitisha zaidi nyuma ya mtoto huyo dhoofu kulikuwa na ndege hatari aina ya TAI akimuwinda huyo mtoto ili kujipatia kitoweo.

Inadaiwa Kevin Carter alipiga picha na kusepa. Inasemekana huko nyuma mtoto yule kutokana na kuwa dhoofu aliweza kuuawa kirahisi na TAI yule.

Inasemekana picha ile ya Kevin Carter ilipata umaarufu sana mpaka kupata tuzo ya Pulitzer iliyoanzishwa na Joseph Pulitzer.

Inadaiwa Kevin Carter umaarufu aliopata haukumsaidia, na alijikuta mwenye hatia kwa kushindwa kumsaidia mtoto yule dhoofu japo kwa chakula na maji badala yake aliona picha pekee ndio jambo la msingi. Tukio lile la huzuni inadaiwa lilimsumbua sana, kumsababishia mgogoro na nafsi hadi kufikia tamati kwa kujiondoa uhai duniani.

KC.jpg
 
Tunachokijua
Kevin Carter alikuwa mpiga picha wa habari kutoka Afrika Kusini na mwanachama wa Klabu ya Bang-Bang Mwaka 1994, alizaliwa Septemba 13, 1960 na kufariki Julai 27, 1994). Miongoni mwa mafanikio yake katika kazi ya upigaji picha aliweza kuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer iliyotokana na picha yake ya mwaka 1993 alipokuwa anadhihirisha athari ya njaa katika nchi ya Sudan.

Carter alipiga picha ambayo inaonekana kama msichana mdogo aliyekuwa amedondoka chini kutokana na njaa, huku Tai akionekana anamvizia kwa karibu. Ambapo wa mujibu wa vyanzo Kelvin anadai baada ya kupiga picha alimfukuza ndege huyo ili asimdhuru mtoto. Tazama picha hiyo hapa Chini:

1694038044607-png.2741531

Picha hiyo ilinunuliwa na The New York Times na kuchapishwa mara ya kwanza mnamo Machi 26, 1993, na kusambazwa ulimwenguni kote. Mamia ya watu waliiwasiliana na gazeti hilo kuuliza hatima ya mtoto huyo. Gazeti lilisema kwamba kulingana na Carter, "Mtoto alipona kwani ndege huyo alifukuzwa na mtoto aliendendelea na safari yake. Mnamo Aprili 1994, picha hiyo ilishinda Tuzo ya Pulitzer kwa Uchanganuzi wa Picha. Mwaka 2011, baba wa mtoto huyo alifichua kwamba mtoto huyo alikuwa ni mvulana, Kong Nyong, na alikuwa amechukuliwa na kituo cha msaada wa chakula cha Umoja wa Mataifa.

Je, Carter alijiua baada picha aliyompiga mtoto kumpatia tuzo ya Picha bora (Pulitzer Prize)
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali ambavyo vyote vinakiri kwamba Mpiga picha Kelvin Carter alijiua kwa sumu mnamo Julai 27, 1994 akiwa na miaka 33

Mathalani, katika Jarida la The New York Times na The Guardian wote wakieleza kifo cha Kevin Carter wanaandika kuwa Mpiga Picha huyo alikutwa amejiua mwaka mmoja baada ya kupokea Tuzo ya Pulitzer. Taarifa za Polisi zilifafanua kuwa uchunguzi ulionyesha Carter alikufa kutokana na sumu ya kaboni monoksidi. Zaidi ya hayo, Polisi walieleza kuwa walikuta barua kadhaa kwa marafiki na familia zilipatikana katika gari lake la kubebea mizigo, lililopakiwa katika mtaa wa Johannesburg.

Zaidi ya hayo, majarida hayo yanaeleza kuwa katika harakati zake za kupiga picha Kelvin Carter alikutana na changamoto nyingi ikiwamo kufungwa na kusumbuliwa na Polisi. Majarida hayo yanasimulia pia namna rafiki mkubwa wa Carter, aliyeitwa Ken Osterbroek, alivyouawa mbele yake wakati wakiripoti mapigano ya bunduki katika mji wa Thokoza nje ya Johannesburg. Pia yanasimulia namna Mahusiano ya muda mrefu yalivyovunjika mambo mbayo yalimsababishia kuwa na mawazo na masononeko kwa muda mwingi.

Pamoja na kuwa majarida hayo yanatupa picha kuwa Kelvin Carter alifariki mwaka mmoja baada ya kupata Tuzo iliyotokana na Picha ya mtoto na ndege tai nchini Sudan lakini maelezo ya moja kwa moja yanayobainisha kuwa picha hiyo ndiyo ilimfanya Carter kujiua. Aidha majarida hayo ya The New York Times na The Guardian yanatupa picha namna Carter alivyopitia wakati mgumu na kusongwa na mfululizo wa matukio mabaya siku za mwisho za uhai wake.

Hivyo, JamiiForums inaona kwamba hoja inayodai kuwa Kevin Carter alijiua baada picha ya kusikitisha aliyompiga mtoto akiwindwa na Tai kumpatia tuzo ya Picha bora (Pulitzer Prize) ni ya kinadharia isiyo na uthibitisho.
Sijui alikuwa na akili gani kumwacha huyo mtoto katika mazingira hayo!
Kwa miaka ya 90 wazungu afrika kusini walikuwa na ubaguzi mbaya sana , hata kumgusa huyo mtoto kwake ilikuwa kama jinai, wachilia mbali kumbeba
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom