Katika ndoa kuna wajibu, haki, majukumu na utaratibu wake katika maisha

USSD

Member
Sep 19, 2021
21
55
UMUHIMU WA KUJIANDAA NA MAISHA YA NDOA

Katika kumuumba kwake mwanadamu, Mungu aliweka utaratibu wa kuwepo mahusiano kati ya mwanamume na mwanamke , ili kuendeleza

uzao kwa wanadamu,

kuwaondolea upweke na kuwatunukia utulivu, faraja, huruma, mapenzi, upendo na ushirikiano.

Kutokana na Mwenyezi Mungu kuwajengea wanadamu mahusiano hayo ya jinsia mbili tofauti, aliweka sharti na utaratibu wa mahusiano hayo, nao ni utaratibu wa ndoa kati yao.

Kimsingi ndoa kwa wanadamu ni uhalalishaji adilifu wa mahusiano ya mume na mke.

Mahusiano ambayo yamewekewa utaratibu mahususi ya kukubalika nakutambulika rasmi.

Kusudio la kuwepo utaratibu huu wa ndoa ni kuweka mipaka ya kimahusiano miongoni mwa wanadamu na kuondoa vurugu za watu kuingiliana hovyo.


Hii ina maana ya kudhihirisha kwamba mke au Mume wa mtu anaheshimiwa kwakuwa kwake katika mafungamano ya ndoa.

Na atakayejaribu kuingilia mahusiano hayo ambayo yamekuwepo kwa utaratibu huo, huyo anatizamwa kuwa mwasherati, mzinzi na asiye na utu.

Kutokana na umuhimu wa ndoa katika maisha ya mwanadamu, tumeona kuna haja ya kukumbushana, hasa vijana jinsi ya kujiandaa na maisha ya ndoa kabla ya kuona.

inapofikia hatua ya kutaka kuoa au kuolewa, pande zote mbili hukabiliwa na mawazo mengi ni vipi atampata mchumba sahihi.

Tatizo kubwa ni katika kumchagua mwenza sahihi na mwenye sifa, ambaye utakapompata na kumuoa/kuolewa, atakuwa ndiye mshirika wako wa maisha.

Vile vile hutizamwa ni vigezo gani atumie muoaji au muolewa katika kufikia lengo lake la kumpata anayestahili na kukidhi.

Ikumbukwe kwamba pamoja na kwamba kuna dhana kwamba mwanamke hawezi kuchumbia na hana nafasi ya kuchagua mume anayetaka aolewe naye, lakini ukweli ni kwamba kwa utashi wake mwanamke ana haki ya kumkubali au kumkataa mchumba anayekuja kwake.

Kwa ujumla mambo ya ndoa huwasumbua watarajiwa huku kila mmoja akiwa na mitazamo tofauti katika chaguo.

Kila upande ukiwa umekua na kulelewa katika mazoea, desturi na tamaduni tofauti, mambo ambayo yana athari kwa namna moja au nyingine katika makuzi.

Baadhi ya wenye dhamira ya kuoa au kuolewa, wanakuwa hawafahamu wanahitaji mke au mume wa aina gani. Wakati mwingine wanajikuta wanaingia katika hamu ya kuwa katika ndoa, lakini bila kujua wanataka kuwa na wenza wa namna gani.

Wengine hujikuta wakijiingiza katika ndoa bila ya kuwa na ufahamu wa kutosha au taaluma yoyote inayohusiana na maisha hayo ya mahusiano na hatimayake hukosa uwezo wa kuziendesha ndoa zao.

Lakini pia wapo ambao hawana kabisa uelewa wa misingi ya kuoa na kuolewa zaidi ya kusukumwa na fikra finyu ya kutamani kuwa na mwenza kwa ajili ya kukidhi tu matamanio ya nafsi na hususan tendo la ndoa na kurahisishiwa baadhi ya majukumu kama vile kupika, usafi wa nyumba, kufua nk.

Wapo wanaotamani kuingia katika mahusiano ya ndoa kwa lengo moja tu,la kupata wepesi wa kupata mali na maisha ya anasa na starehe.

Kwa ujumla wengi wanaotaka kuoa au kuolewa, mara nyingi hawana fikra halisi na pana ya kusudio la ndoa.

Hata maandalizi katika kuliendea jambo hilo wakati mwingine hayafanyiki vya kutosha na kwa kiasi kikubwa.

Uchaguzi wao hautizami sekta za msingi kama dini na maadili kwa ujumla wake.

Siku hizi sehemu kubwa ya jamii yetu imezoea kuyafanya masuala ya ndoa kuwa ni mambo ya kiutamaduni

Kwa mtazamo huo, ndoa nyingi zimekosa uvumilivu na kuendelea kuporomoka na kusababisha utengano wa kifamilia na magomvi kwa kasi ya kutisha.

Matokeo yake, badala ya kuunganisha familia kama ilivyokusudiawa na kujenga udugu, ndoa zimekuwa chachu ya utengano wa kifamilia, kuporomoka udugu na kuwa chanzo cha huduma mbovu za kijamii katika familia na wanaoathirika zaidi ni watoto.

Katika kufanya uchaguzi wa mtarajiwa, iwe ni mume au mke,kuna mambo mawili yanaweza kujitokeza, nayo ni kuwa na ndoa iliyojaa matarajio ya watarajiwa (kama yalikuwepo kabla) au kuwa na ndoa iliyokosa matarajio ya watarajiwa na hivyo mwisho wake kuwa ni balaa badala ya raha, dhiki badala ya faraja.

Anaweza mtu kuoa au kuolewa na akafurahia uamuzi wake huo kwa jinsi ndoa ilivyotimiza matakwa ya kuitwa ndoa.

Lakini mwingine akajutia uamuzi wake kutokana na kukithiri maudhi mpaka kufika kuhasimiana na kuachana.

Ili kuepukana na hali hii, kuna haja ya kuwa na utaratibu mahususi kwa wazazi, wazee na viongozi wetu wa dini katika jamii yetu, kujenga mazoea ya kutoa mafunzo na miongozo kwa vijana wetu ili kujaribu kutoa mwongozo kujaribu kuokoa janga hili la kasi ya kuharibika mahusiano ya ndoa.

Utulivu katika ndoa ni moja katika mambo muhimu yanayodumisha maisha ya ndoa kwa wanandoa.

Haina maana kosa kidogo tu, au kosa moja likamfanya mtu mara moja akakosa uvumilivu wa kutoa nafasi ya mwenzake kuonywa au kujirekebisha, yeye kashaamua.

Ndoa huunganisha koo kufikia kuweza kurithiana kati ya mume na mke.

Ndoa huzuia zinaa.

Ni jambo la msingi kwa kila mwana ndoa au anayetarajia kuingia katika ndoa, afahamu kwamba ndoa ni kati ya riziki ambazo Mwenyezi Mungu amewapa wanadamu

Katika ndoa kuna wajibu, haki, majukumu na utaratibu wake katika maisha.

Kabla ya kuoa au kuolewa na kufunga ndoa, kuna haja ya kujiuliza kwanini unaliendea jambo hilo.

Hili ndio swali la kwanza muhusika anapaswa kujiuliza ndani ya moyo wake na kupata majibu yake.

Ndoa humpa mtu heshima katika jamii, kupata watoto,kutafuta stara, kujenga familia bora, kuwaridhia wazazi wawili, kukidhi hamu za kijinsia.

Lakini wapo pia ambao kufikia maamuzi ya kuoa kwakufuata marafiki, kusaidiana majukumu

Ni lazima yawepo malengo ya kuoa kabla ya tendo lenyewe.

Lakini malengo yenyewe lazima yawe sahihi na siyo ya kinafsi na ya matamanio tu.

MWANAMKE NA MAFANIKIO YA MWANAUME​


SUALA la ndoa katika maisha ni jambo lenye heshima, hadhi na furaha. Lakini zaidi ya yote, ni sehemu muhimu ya mchakato wa kawaida katika maisha ya binadamu.

Hapa namaanisha kuwa, kuingia kwenye ndoa ni sehemu ya maisha ya binadamu hivyo basi inahusika moja kwa moja hata katika mambo ya mafanikio kimaisha.

Ukweli ni huu.

Walio kwenye ndoa, hasa zenye masikilizano wana nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa maishani mwao kuliko wale ambao hawana ndoa.

Kuna uhusiano wa karibu sana katika kujenga familia na mafanikio ya kimaisha na ndoa.

siku hizi vijana wengi ni kama hawaoni umuhimu sana wa suala la kuoa au kuolewa.

Zipo sababu kadhaa ambazo zinawafanya vijana kuchelewa au kupuuzia kuoa, mwisho wanakuja kushtuka tayari umri unakuwa umekwenda. Yapo madhara makubwa yanayotokana na kuchelewa kujenga familia.


FAIDA ZA KUOA

Faida kubwa zaidi katika kuoa, ukiacha mengine yote ni

kupata muda wa kutosha wa kulea watoto wakati ukiwa na nguvu.

Watoto wa kuwazaa ukiwa na umri mkubwa, mara nyingi huwa wanadhulumiwa malezi na mahitaji sahihi.

Mfano, ikiwa baba atazaa mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 40, maana yake hi hii: Mtoto akiwa na umri wa miaka sita, ambao ndiyo huanza darasa la kwanza, baba atakuwa na umri wa miaka 46. Atamaliza darasa la saba akiwa na miaka 13 huku baba akiwa na 51.

Ongeza miaka sita ya kidato cha kwanza hadi cha sita, mtoto atakuwa na miaka 20 (ukiweka kipindi cha kusubiri matokeo) baba atakuwa na miaka 58 – huo ni muda wa kijana kujiunga na Chuo Kikuu.

Hapo sijazungumzia watoto wengine wanaofuata.

Maana yake, mzee huyu mwenye miaka 58 bado atakuwa na mzigo wa kusomesha.

Katika umri huo ambao wengi wanakuwa wameshastaafu kazi, uwezo wa ubunifu wa biashara au usimamizi wa biashara unakuwa mdogo, haiwezi kuwa rahisi kwake kuwaendeleza sawasawa watoto wake kielimu.

Lakini ukioa mapema, unakuwa na uwezekano pia wa kupata watoto mapema, ambao utakuwa na uwezo wa kuwasomesha ukiwa na nguvu na kuwafuatilia vizuri kwenye elimu yao ambayo kimsingi ndiyo msingi wa maisha.


MISINGI YA NDOA.


Kuna mambo mengi sana muhimu ya kufanya katika ndoa ili ndoa iwe imara na yenye mafanikio,


Je, ni Misingi ipi hiyo?

1. MUNGU KUWA KIONGOZI WA NDOA.


Ndoa ambayo inaendeleza, ongeza, imarisha na kufurahia mahusiano na Mungu itakuwa na picha kamili ya Mungu.
Kila mwanandoa atakuwa na uhusiano mzuri na Mungu na atajitahidi kuishi katika maadili ya dini na matokeo yake dhambi itakaa mbali na dhambi kukaa mbali basi upendo wa kweli wa kimungu huongoza ndoa.

Ndoa yenye msingi wa Dini huwa na maombi na maombi ni mawasiliano ya wanandoa na Mungu, hivyo kwa kuwa na connection kati ya Mungu na wanandoa, Mungu atakuwa anaipa stabilization ndoa yao kila wanapokutana na tatizo, shida au jaribu.

Unajua kuna siku shetani huwa anaamua kumpaka matope mmoja ya wanandoa ili asipendwe (unajisikia kutovutiwa na mwenzako), ni kwa maombi tu unaweza kuharibu kazi za aina hii za shetani si pesa, wala elimu wala ujanja.

Kwenye ndoa kuna good times na bad times na Mungu huweza kuwapitisha wanandoa vizuri kama wanamtegemea yeye, hilo halina ubishi ni amini na kweli.

2.UPENDO WA KUJITOA.

Maisha ya binadamu ni safari ndefu, si sahihi kwamba siku zote ndoa itakuwa na mapenzi yaleyale ya motomoto, au kupendana kule kule kama mwanzo, kiwango cha mahaba kupanda tu graph kila iitwapo leo; si kweli, kutokana na kuwa na malezi tofauti na mambo mengine inawezekana ndoa kupita kwenye wakati mugumu sana, kuna stress, kuna kukata tamaa, kuna business kufilisika, na kuna wakati tu inatokea mume na mke kila mmoja hampendi mwenzake bila sababu, hivi vyote vinahitaji watu wenye Upendo wa kujitoa ili kurudi kwenye mstari.
Katika ndoa conflict na disagreement hutokea bila upendo wa kujitoa basi ndoa haiwezi kufika popote.
Kwenye ndoa hakuna mtu perfect wote bado tuna tumia Learner driving license kwa maana kwamba tunaendelea kujifunza na kutoa efforts za kuhakikisha ndoa inakuwa na afya na inaendelea kudumu na kudumu na kudumu.

Kuna utafiti ulifanywa kwa wanandoa waliopata talaka, asilimia 40 walisema wanatamani kurudi kwenye uhusiano wao wa kwanza, hii ni kuthibitisha kwamba wangekuwa na upendo wa kujitoa basi wasingeamua kuomba talaka zao kwani kuna watu ambao conflict kidogo tu, tuachane!

Hawana dogo na wengine sasa kuoa na kuolewa ni kama shopping!

3. MAWASILIANO.


Utafiti unaonesha kwamba watoto wadogo wa kike wamebarikiwa sana (talented) na uwezo wa kuongea na lugha kwa ujumla , huweza kuongea haraka na mapema kuliko watoto wadogo wa kiume.
Hiyo tabia huendelea hadi wanapokuwa watu wazima na kwa maana hiyo wanawake na wanaume lipokuja suala la kuongea na mawasiliano kwa ujumla kuna tofauti kubwa.

Hivyo basi wanawake ni viumbe wanaohitaji mwanaume kuuongea ili na yeye aongee hayo maneno yake, ndiyo maana kwa mfano kama umetoka kazini basi mwanamke anapenda sana umwambie mambo mbalimbali kama vile unafikiri kitu gani, nini kilitokea kazini, watoto wameshindaje, unajisikiaje kuhusu yeye mwanamke nk.
Wakati huohuo wanaume hujisikia sawa tu hata asipoongea chochote akifika nyumbani kutoka kazini matokeo yake mke anakuwa bored na hayo ni mawasiliano mabovu.
Wanaume kushindwa kuelezea hisia zao kwa wake zao ni kitu kinachowaumiza sana.

Panga muda maalumu kwa ajili ya maongezi ya maana na mke wako hata kwa kuwa na matembezi au outing.
Hata hivyo wanawake wanapaswa kufahamu kwamba kuna wanaume ambao hawawezi kuwa kama wanavyotaka wao kwani ndivyo walivyo.
Mume wako hataweza kukutimizia mahitaji yako yote kwani hakuna mwanaume duniani ambaye anaweza kumpa mwanamke vyote anavyohitaji, ndiyo maana hata wewe mwanamke mwenyewe hupo perfect mia kwa mia.

Kumbuka

Unapowasiliana na mume au mke;
Badilisha kile ambacho kinaweza kubadilishwa
Elezea kile ambacho anaweza kukielewa
Fundisha kila ambacho anaweza kujifunza
Patanisha kile ambacho anaweza kukubaliana
Rudia kile ambacho anaweza kukiimarisha.
 

Attachments

  • DOC.docx
    29.3 KB · Views: 24
Si ruhusa kisheria na kibinaadamu pia
Lakini watu wengi wamekua wakitumia kama mbadala wa kujinasua pindi wake zao wanapokua katika hali hiyo
 
Back
Top Bottom