Kataa ndoa. Leo wamepata point 3 ugenini, ilikuwa hivi...

Asilimia kubwa ya ndoa zenye makelele hua hazidumu. Ndoa sio Movie Premier ya kufanyia maonyesho, na ni ishara walioona sio mapenzi bali ulimbukeni ndio unaowafanya wayafanye hayo i.e not suitable for family building. Cha pili, hata msipofunga ndoa, Kama mali mmechuma pamoja, mtagawana tu.
 
Mkuu, wanasema you can not solve modern problems with old methods.

Amka, kumekucha, la sivyo utalia muda si mrefu, modern problems need modern solutions.
Hakikisha haujipumbazi na huo umodern.

Hata ulimwengu uwe modern kiasi gani, laws hazitakaa zibadilike hata kidogo. Laws zinazogovern huu ulimwengu ni nne tuu. Marriage is in one of the laws.

Hakuna jaribio la kutemper na hizi laws lililoiacha dunia salama.

Najua this is heavier than most of heads
 
Haya masuala ya kukwepa majukumu yetu sijui tunawaandalia Mfumo Gani wa maisha watoto wetu.

Umefilisika, alafu unaamua kumfungulia mke biashara, kwanini hukumfungulia wakati ukiwa vizuri?

Na kikawaida Mwanaume akishafilisika saikolojia yake inabadilika, hajiamini tena, na hapohapo unampa mke kitu Cha kumfanya ajiamini mara dufu...

Unategemea Nini?
 
Mzee huyo mwanamke alishaniacha akaenda hadi mahakamani, ustawivwa jamii kazunguka ila yakamshinda, alipichoka nikamwambia rudi ndani, akarudi. Sabab ni mara mia kukaa na kajini unakokajua na kanakokufaham kwamba ww si wa mchezo mchezo.

I'm faced with legal issues on daily basis, nikikwambia hio sheria ya kukaa na dem eti miezi sita ndo nimemuoa ina loopholes naelewa ninachokisema.
Taja hizo loopholes, au hutaki wanaume wenzako tufaidikie tusioe kama Wewe?
 
Nina mwanamke mwaka wa saba huu nakaa nae na sijamuoa, kila mtu anaenijua physically anajua ni mke wangu. Kuna kipindi alileta kelele lkn akaja kugundua mimi ni mafia, ametulia anakula ugali na samaki.
Usijisifie Mkuu, kabla ya yote kasome kifungu cha 160 cha sheria ya ndoa. Alafu endelea kuomba huyo mwanamke asije kukijua au kuambiwa.
 
Haya masuala ya kukwepa majukumu yetu sijui tunawaandalia Mfumo Gani wa maisha watoto wetu.

Umefilisika, alafu unaamua kumfungulia mke biashara, kwanini hukumfungulia wakati ukiwa vizuri?

Na kikawaida Mwanaume akishafilisika saikolojia yake inabadilika, hajiamini tena, na hapohapo unampa mke kitu Cha kumfanya ajiamini mara dufu...

Unategemea Nini?
Point
 
Matatizo mnajitakia wenyewe. Unatumia fedha kumshawishi mwanamke akupende ili umuoe! Hii inaonyesha kabisa jamaa yako alitumia ''misuli'' ya fedha ili kumvuta huyo demu. Na mara nyingi unakuta ni hawa ''wenzangu'' na mimi wenye elimu ndogo na pengine washamba na ulimbukeni hapo hapo, wanapofanya biashara na kupata fedha za ghafla wanakimbilia kuoa wanawake ''wavaa vimini'' ili nao waonekane ni wajanja.

Hoja yako sio ya kweli.. binadamu tunabadilika. Na upendo huwa unaisha.

Naweza nikakupenda leo. Kesho nisikupende.

Na pia nikikupenda wewe leo haimaanishi sitaweza kumpenda mwingine mbeleni

Women are loyal to their feelings.

Pale temeke mahakama ya ndoa.. kila siku za kazi mahakama inavunja ndoa kibao Je wote hao walikuwa hawapendani zamani
 
Usijisifie Mkuu, kabla ya yote kasome kifungu cha 160 cha sheria ya ndoa. Alafu endelea kuomba huyo mwanamke asije kukijua au kuambiwa.
Hahahaha

Sijui niseme mara ngapi.

Kuna siku nitafungulia uzi kesi yangu na yy iliomuamsha.

Hv ushajiuliza kwa nn vicky kamata alinyimwa hata mia? Kimada ni kimada tu mzee, hio sheria inawala maboya.

Leo ukienda kulala jua kwamba almost kila by-laws zina counter-part yake.

Ndoa ni law, hio ya kukaa na mwanamke ndani ni by-law
 
Mambo mengine yanahitaji kufanyiwa ''update'' kila baada ya muda ili kuenda na wakati, sheria za ndoa ni mojawapo. Imefika muda, sheria za ndoa za Tanzania zifanyiwe maboresho haraka sana, ili kuwe na uwezekano wa kufunga ndoa zenye makubaliano maalum kulingana na wanandoa wanavyokubaliana. Kwa mfano wanaweza kukubaliana kuwa wakiwa kwenye ndoa kila mtu atachuma na atamiliki mali zake na ikitokea kuna kutengana, kila mmoja anaondoka na ''mbao zake''.
Hii haizuiwi hata kwa sheria iliyopo. Ukiweza andikishana tu na mkeo.
 
Usijisifie Mkuu, kabla ya yote kasome kifungu cha 160 cha sheria ya ndoa. Alafu endelea kuomba huyo mwanamke asije kukijua au kuambiwa.
Mkuu mgeni.

Mimi nimemwbia hivi aendele kuomba kapata Mke ambaye hafahamu, Nina muhakikishia hawezi kuchukua raundi akikutana na wanasheria wanaojua hasa wale wamama wanaoshusha miwani kwenye pua.

Halafu kuhusu prenuptial hili ni janga.
Sababu kama kila mtu ana mali zake hapo hakuna ndoa. Mke ataamka alfajiri awahi kazini atasema tutafute mfanyakazi tuchangie kumlipa sababu hapa kila mtu anatafuta maisha yake.

Inapunguza upendo wote, yaani unamwambia mwanamke wewe chako ni chako changu ni changu.

Hiyo sheria inatumiwa na matajiri sana sana.
 
Mzee huyo mwanamke alishaniacha akaenda hadi mahakamani, ustawivwa jamii kazunguka ila yakamshinda, alipichoka nikamwambia rudi ndani, akarudi. Sabab ni mara mia kukaa na kajini unakokajua na kanakokufaham kwamba ww si wa mchezo mchezo.

I'm faced with legal issues on daily basis, nikikwambia hio sheria ya kukaa na dem eti miezi sita ndo nimemuoa ina loopholes naelewa ninachokisema.
Mkuu kwanza kabisa hakuna sheria inayosema kukaa na mwanamke miezi 6 anakuwa ni mkeo, hiyo sheria haipo.

Ila kuna sheria inayosema ukiishi na mwanamke kwa miaka miwili kunakuwa na dhana kuwa ni mkeo.

Huyo mwanamke ni vile hajakutana na wakili amsetie mambo sawa chomoka yako itakuwa ni nyembamba sana Mkuu na pengine isiwepo kabisa.

kama haufahamu sheria na yeye hafahamu sheria basi usijigambe Mkuu, jipe muda tu uanze kutenga mali zako, zake na zenu ili uwe salama ila vinginevyo hautoboi.
 
Back
Top Bottom