Kanusho la kuwepo kwa Mayai ya Kuku kutoka nje ya Nchi yaliyosababisha kushuka kwa bei ya Mayai Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,884
12,133
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dodoma, Juni 17, 2021


A: UVUMI KUHUSU TAARIFA ZINAZOZUNGUKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA) JUU YA UWEPO WA MAYAI YA KUKU KUTOKA NJE YA NCHI YALIYOSABABISHA KUSHUKA KWA BEI YA MAYAI NCHINI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki.JPG

Ndugu waandishi wa Habari,

Tarehe 14/06/2021 Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliona ujumbe unazunguka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuingia kwa mayai mengi nchini kutoka nje ya nchi kiasi cha kusababisha kushuka kwa bei ya mayai mpaka kufikia shs 4,000= kwa trei. Ujumbe huo ulikuwa na kichwa cha habari kinachosomeka “SOKO LA MAYAI DSM KITENDAWILI”.

Baada ya kuona ujumbe huo, Tarehe 15/06/2021 Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilifanya uchunguzi kwenye makao makuu ya mikoa yote 26 nchini na baadhi ya Wilaya ili kujiridhisha juu ya upatikanaji wa mayai, bei ya trei ya mayai na soko lake kwa ujumla.

Njia zilizotumika kukusanya taarifa ni pamoja na:
Kuongea na wafugaji wakubwa wa kuku wa mayai;
Kuongea na wafanyabishara wakubwa na wadogo wa mayai;
Kufika sehemu za masoko kunakouzwa mayai na kujionea hali halisi ikiwa ni pamoja na kujua bei ya trei ya mayai, upatikanaji wake na hali ya soko kwa ujumla;
Kuongea na Maafisa Mifugo wa Mikoa, Majiji, Manispaa na Halmashauri ili kupata taarifa juu ya bei ya trei ya mayai, upatikanaji wake na hali ya soko la mayai kwenye maeneo yao ya kiutawala.

Matokeo ya uchunguzi huo yanaonesha kwamba:


  • Mayai yanayozalishwa nchini ni kidogo kiasi kwa sababu ya uhaba wa vifaranga wa kuku wa mayai;
  • Tatizo la uhaba wa vifaranga limekuwepo tangu mwaka 2020 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 duniani uliopelekea uingizaji nchini wa vifaranga wa kuku wazazi kupungua sana;
  • Hali hii imesababisha idadi ya kuku wa mayai wanaotaga kwa sasa kuwa wachache na kusababisha kuwepo na uhaba wa mayai nchini;
  • Matokeo zaidi ya uchunguzi yanaonesha kwamba bei ya trei la mayai katika ngazi ya mfugaji ni kati ya shs 6,500 mpaka shs 9,000.
  • Vilevile bei ya trei la mayai sokoni ni shs 6,800 katika baadhi ya mikoa mpaka shs 12,000 kwa mikoa ya Katavi;
  • Aidha bei ya yai moja sokoni au madukani ni kati ya shs 250= mpaka shs 500=.
Maoni ya Wizara Juu ya Ujumbe Kuhusu Kuingia Kwa Mayai Nchini

Kutokana na ujumbe uliosambazwa kwenye mitandao (social media), Wizara ya Mifugo na Uvuvi ina maoni yafuatayo:

Hakuna uwingi wa mayai uliosababisha kushuka kwa bei ya mayai katika ngazi ya mfugaji na sokoni;
Kinachoonekana zaidi ni kuwa kuna upungufu mkubwa wa mayai nchini uliopelekea bei kupanda mpaka kufikia hadi shs 12,000=;

Taarifa zilizosambazwa ni uzushi mtupu na hazina ukweli wowote;
Serikali ilishazuia uingizwaji wa kuku na mazao yake kutokana na uwepo wa tishio la ugonjwa wa Mafua Makali ya Ndege Duniani. Aidha, Wizara imekuwa ikitoa vibali maalum vya kuingiza vifaranga na mayai ya kutotolesha ya kuku wazazi;
Kumekuwa na matukio machache ya uingizaji wa mayai nchini kwa njia za panya lakini Wizara imekuwa ikidhibiti hali hiyo;
Mwezi wa Aprili, chama cha wafugaji wa kuku kiliomba makampuni ya kuku yaruhusiwe kuingiza vifaranga wa kuku wa nyama, vifaranga wa kuku wa mayai na mayai ya kutotolesha kutokana na uhaba mkubwa wa vifaranga nchini na Serikali imeruhusu kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Juni mpaka Agosti 2021;
Tayari makampuni kadhaa yameshaanza kuingiza nchini vifaranga na mayai ya kutotolesha na hivi karibuni tatizo hili litafikia ukomo.

Mapendekezo ya Wizara

Uzushi uliojitokeza kutokana na kusambazwa kwa ujumbe wenye taarifa za kupotosha kuhusu kuingizwa kwa mayai nchini kutokea nchi jirani unapaswa upuuzwe;
Mtu aliyezusha taarifa hizi za uongo ana nia ovu na tasnia ya ufugaji kuku Tanzania na ameleta taharuki kubwa kwa wafugaji wetu;
Kwa wafugaji wetu wa kuku na jamii yote ya Tanzania, suala la uhaba wa vifaranga linafanyiwa kazi na kufikia mwezi wa Septemba, 2021 hali itakuwa imesharudia kama kawaida.

B: HALI YA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE NA JITIHADA ZINA ZOCHUKULIWA KUKABILIANA NA TATIZO HILI

Ndugu waandishi wa Habari,

Tarehe 23, Januari 2021 nilitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya Habari juu ya kuwepo kwa mlipuko wa Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe (African Swine Fever) katika maeneo ya mikoa ya Mwanza, Kagera, Shinyanga na Dodoma. Katika taarifa yangu hiyo, niliwaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa masharti ya karantini zilizokuwa zimewekwa na wataalamu wa mifugo hasa kwa vile ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Nawashukuru sana kwa jinsi walivyosimamia zoezi hilo.

Aidha Wizara yangu imekuwa ikifanya juhudi kubwa kudhibiti ugonjwa huu na mpaka kufikia mwishoni mwa Mwezi Aprili, 2021 sehemu nyingi za nchi hakukuwa na matukio ya ugonjwa huo.

Mnamo tarehe 01/06/2021 katika Manispaa ya Morogoro kulijitokeza matukio ya nguruwe 14 kufa na uchunguzi wa kimaabara ulionesha ugonjwa wa Homa ya Nguruwe. Tayari juhudi kubwa za kuudhibiti zinaendelea ambazo ni pamoja na kuweka zuio (karatini) ya kuingiza na kutoa nguruwe na mazao yake katika Manispaa ya Morogoro tangu tarehe 03/06/2021 na elimu kwa wafugaji na wadau wengine wa nguruwe njia za kukinga ugonjwa usiingie kwenye mabanda ya nguruwe. Mpaka kufikia jana tarehe 17/06/2021 hali ya ugonjwa katika Manispaa ya Morogoro imedhibitiwa na hakuna kifo tena kilichotokea kwa nguruwe.

Tarehe 09/06/2021, Wizara ilipata taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe katika Jiji la Dar es Salaam. Baada ya kufanya uchunguzi katika mashamba ya nguruwe, tulibaini uwepo wa taarifa za nguruwe 298 kufa katika mashamba mawili kwa kile kilichodhaniwa ni ugonjwa wa Homa ya Nguruwe. Baada ya kuchunguza kwa kina kwa wanyama waliokuwa wamebaki kwenye mashamba hayo pamoja na kuchukua sampuli na kuzipima katika maabara, ilibainika kuwa ilikuwa sio ugonjwa wa homa ya nguruwe. Ufuatiliaji zaidi ulifanyika kwenye sehemu zote za machinjio ya nguruwe Dar es Salaam na kuchunguza nguruwe wanaochinjwa, hapakuwa na viashiria vyovyote vya ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inaendelea na juhudi za kudhibiti kabisa ugonjwa huu nchini.

Asanteni kwa kunisikiliza

Imetolewa na

Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (MB)

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI


 
Huenda mada hii inahusu biashara, ndiyo maana haipati wachangiaji wa mambo ya siasa.; lakini ni taarifa muhimu sana iliyotolewa na wizara.

Nawashauri wWizara ya Mifugo na Uvuvi, wasiwe wanasubiri kujibu taarifa za uzushi ndipo wafuatilie na kujuwa hali ya soko za bidhaa zinazozalishwa na wizara yao ikoje.

Inafaa sasa wawe na utaratibu wa kukusanya na kuweka kumbukumbu ya mambo kama haya ili wanaohitaji kutumia taarifa hizo wazipate kwa uhakika bila ya kusubiri kuzuka kwa uzushi kama huu walioujibu hapa.
 
Kijana, magufuli kashajiozea chini ya ardhi, Tanzania imebakia, kwaiyo chagua kubaki na Tanzania au jiue mfuate msukuma mwenzio,

TANZANIA itaendelea kuwepo, wenye akili tulijua mbio za dikteta zitaishia ukingoni,na Nchi itabakia salama tu
 
Kijana, magufuli kashajiozea chini ya ardhi, Tanzania imebakia, kwaiyo chagua kubaki na Tanzania au jiue mfuate msukuma mwenzio,

TANZANIA itaendelea kuwepo, wenye akili tulijua mbio za dikteta zitaishia ukingoni,na Nchi itabakia salama tu
Ok!

Sasa mbona unahangaika namna hiyo?
 
Huenda mada hii inahusu biashara, ndiyo maana haipati wachangiaji wa mambo ya siasa.; lakini ni taarifa muhimu sana iliyotolewa na wizara.

Nawashauri wWizara ya Mifugo na Uvuvi, wasiwe wanasubiri kujibu taarifa za uzushi ndipo wafuatilie na kujuwa hali ya soko za bidhaa zinazozalishwa na wizara yao ikoje.

Inafaa sasa wawe na utaratibu wa kukusanya na kuweka kumbukumbu ya mambo kama haya ili wanaohitaji kutumia taarifa hizo wazipate kwa uhakika bila ya kusubiri kuzuka kwa uzushi kama huu walioujibu hapa.
Haipati wachangiaji sababu inataka wenye akili kubwa ili kuichangia.
 
WANAKANUSHA NINI wakati rais alienda kenya kufungua fursa, arusha kilombero yako kibao yanaingia kwa njia za panya.
 
Nashindwa kuelewa ....

Kama wao wanaweza kufuga na kupata mayai ambayo bei ni nusu ya kwetu basi tuende tujifunze kwao na sisi tujue tufanye kama wao...

Na kama vipi tuone jinsi ya ku-process hayo mayai na ku-add value na kutafuta masoko pengine..., haya mambo ya kulalamika kwamba tunakosa masoko sababu bei za nje ni za chini, kwenye soko huria mnalopigia kelele ni vigumu kuwa maintained...

You can Not have your Cake and Eat it....
 
Waaaoooh!! Hii ni furaha kwa ndugu zangu wa Dar maana huko vibanda vya wauza chipsi ni vingi kuliko vya mamantilie ndo mana wanasumbuliwaga sana na hawa watoto wa panya road kwa ajili ya kuendekeza chipsi mayai kuku broila
 
Ok!

Sasa mbona unahangaika namna hiyo?
Nyinyi ndio bado mnahisi marehemu atazinduka Tena aje awaulize kwann hamumtetei !!

Dikteta kafa,hatorudi Tena mkuu,
Rais now Ni Samia, hupende au usipende, utaki Hama nchi mzee baba
 
Unahangaika sana na mtu ambaye ni marehemu!

Just move on.
Nyani Ngabu Magufuli kashakufa hatorudi tenaaa, Umchukie Samia, usimchukie , yeye ndio Rais Hadi #2040,

Kwaiyo wewe siulikuwa hodari kusapoti kila kitu wakati wa ndugu yako msukuma, Sasa izo sapoti mpe Samia, na uyu sio kama yule dikteta asiyetaka kukosolewa, yeye Samia amesema mumkosea , ila ukosoaji wa kujenga sio wa chuki Kama zenu
 
Nashindwa kuelewa ....

Kama wao wanaweza kufuga na kupata mayai ambayo bei ni nusu ya kwetu basi tuende tujifunze kwao na sisi tujue tufanye kama wao...
Mkuu 'KeyserSoze', inawezekana kweli "unashindwa kuelewa", kwa mfugaji anayefuga kuku 100,000 huko Marekani, anavyoweza kumshinda mfugaji wetu hapa Tanzania mweye vikuku 1,000 kwa sababu haya mambo huyafahamu vizuri.

Hilo siyo kosa lako; kosa ni huko kudhani kwamba huyo wa kuku 1,000 ataweza kuhimili ushindani kwa mazingira ya hapa nyumbani.

Kwani huko ku-process' haya mayai, unadhani huko pia hakuna ushindani na wenye ujuzi zaidi yetu? Hayo tunayo'process' tutayauza wapi!

Na hayo masoko watakaokubali sisi tuwauzie kwa bei ya juu, ambako hao washindani waliotukimbiza kwenye soko letu la nyumbani hawapo tutayapata wapi kwenye dunia hii?

Wakati mwingine ni bora kutumia akili kidogo kuwazia jambo, badala ya kurukia tu mradi tunalisemea.
 
Back
Top Bottom