Kampuni ya Farmbase, Farmers Center wanoa wafugaji na wakulima, matumizi ya bidhaa zilizosajiliwa yasisitizwa kuepusha madhara

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
130
218
Suleiman Msellem ambaye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni za Farmbase, Farmers Center, ambazo ujihusisha na uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa dawa za mifugo na pembejeo za kilimo nchini na nje ya mipaka ya Tanzania amewahasa wafugaji pamoja na wakulima kununua bidhaa za kilimo na mifugo kutoka kwa watu ambao wamesajiliwa na Serikali ili kuepuka madhara yanayoweza kuwakumba.
IMG_20240502_160152_127.jpg

Akizungumza katika mkutano mkubwa ambao umeandaliwa na wadau hao kwa kuwakutanisha wafugaji na wafugaji zaidi ya 500 kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Posta Jiji Dar es Salaam, Mei 1, 2024, Mkurugenzi huyo amesema kuwa kununua dawa mikononi kwa watu ambao hawajasajiliwa na kutambulika rasmi na Serikali kunaweza kuambatana na madhara mbalimbali kwa wanunuzi.

"Niendelee kutoa wito kununua bidhaa za kilimo na mifugo kutoka kwa watu ambao wamesajiliwa na Serikali, ukinunua dawa ambayo imesajiliwa sehemu ambayo imesajiliwa hiyo dawa ubora wake utakuwa umeaminika na umethibitishwa na kuacha kabisa tabia ya kununua dawa mikononi kwa sababu dawa utakayonunua kwenye mikono ya mtu huna uhakika wa ubora wake na uthibi wake inaweza ikisababisha madhara au isifanye kazi inayokusudiwa badae"

Mkurugenzi huyo akieleza juu ya mkutano huo amesema "Kwetu Farmbase na Farmcenter tumekuwa tukifanya hivi kwa zaidi ya miaka 15 tukiwashirikisha wafugaji na wakulima wa maeneo ya Dar es Salaam na karibu yake na mpaka sasa tumepata washiriki kutoka Nchi mbalimbali za jirani, mfano safari hii tuna washiriki kutoka Congo, Zambia, Comoro na Nchi nyingine mbalimbali wanakuja kushiriki hizi semina zetu lengo kutoa elimu sahihi ya ufugaji na kilimo pia matumizi sahihi ya Dawa za kilimo na dawa za mifugo"
IMG_20240502_160200_106.jpg

Kufuatia ushiriki wa wadau kwenye semina hizo amewapongeza huku akisisitiza kuwa Farmbase, Farmers Center wamejenga imani kupitia huduma zao ambazo wamekuwa wakizitoa.

"Tunashukuru kwa ushirikiano ambao tunaupata kwa wafugaji na wakulima kwamba wanatumia sasa dawa zetu toka zamani na wanaamini zimeaminika vizuri."amesema Mkurugenzi huyo

Ameongeza "Ni mshukru Mh. Rais Samia kwa kuendelea kuweka misingi mizuri ya biashara na kufungua njia mbalimbali kama hizi za BBT kuweza kuwasaidia vijana katika uchumi wa kilimo na mifugo"

Pia amese Serikali kuwa licha ya kukutana na changamoto mbalimbali katika utekelejazi wao wa majukumu lakini wamekuwa wakiigeukia Serikali kama mlezi jambo ambalo limekuwa msaada kwao kwa changamoto zao kupatiwa ufumbuzi.

"Tunaishukuru Serikali kila tukipata changamoto hatukimbilii kuzitangaza bali tumekuwa tukienda kwao kama walezi kwamba kuna moja mbili tatu, na tumekuwa tukishirikana hivyo kila wakati na changamoto zimekuwa zikitatuliwa"amesema Mkurugenzi huyo
IMG_20240502_160213_506.jpg

'Wafugaji na wakulima wanazidi kunufaika'

Aidha ameeleza kina kwamba "Kwa sasa hivi wakulima na wafugaji wameboreka, ambapo kipimo chake mfano tulianza baadhi ya wafugaji wakiwa wana kuku 100 wengine 200 sasa utawakuta wana mabanda makubwa yenye kuku wengi zaidi na wanafuga kitaalumu"

Ameendelea kueleza"Na ukienda kwa wakulima waliokuwa wadogo wengi wao wameendelea kuwa bora na wakubwa zaidi, wengine mpaka wamefungua biashara ya kuuza dawa za kilimo huko waliko na tumekuwa tukiwasaidia wanaofanya ujasirimali huu kwa kuwaelekeza na kuwashika mkono"

Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuna watu tokea mwaka 1994 wakati kampuni inaanzishwa ikiwa changa wamekuwa nao mpaka nyakati hizi jambo ambalo linaonesha wazi kuaminika kwa kampuni ambayo ina miaka 30 tokea ilipanzishwa, lakini amesema kuwa Farmbase, Farmers Center imekuwa ikiwafikia wadau wake kwenye mikoa mbalimbali kupitia njia tofauti ikiwemo kuendesha semina kwenye baadhi ya mikoa na kushiriki maonesho ya nane nane.

"Kila siku tumekuwa tukiongeza wigo mwaka hadi mwaka kwa mfano tulianzia Dar es Salaam peke yake badae tukaenda mikoani leo tuna matawi zaidi ya 20 Nchi nzima maana yake tumefika kila sehemu ni rahisi kuwasiliana na watu wetu ambao wapo Nchi nzima, sisi wenyewe pia tumekuwa tukishiriki maonesho mbalimbali"amesema Mkurugenzi huyo
IMG_20240502_160204_219.jpg

Anasema kuwa wamevuka mipaka hadi Nchi jirani

"Sasa hivi tumetoka hadi nje ya Tanzania ukienda kwenye Nchi za jirani zote Comoro Zambia, Malawi, Msumbiji, Congo, Uganda, Kenya , Zimbabwe hata Afrika Kusini utakuta watu ambao wanatumia dawa zetu kwa namna moja au nyingine nasisi pia tumesajili huko katika Nchi mbalimbali" ameeleza Mkurugenzi huyo

Kufuatia hatua hiyo amesema kuwa wanajivunia kukua kwao hali ambayo inaenda sambamba na wateja na washiriki wao ambao wamekuwa nao pamoja nao kupiga hatua.

Amesema mafanikio yamekuwa yakitokana na bidhaa wanazozalisha na kusambaza pamoja semina za kuwaongezea ujuzi wakulima na wafugaji hususani matumizi ya dawa ambazo wamekuwa wakizipata kwenye kampuni hiyo.

Amesema kupitia semina hizo na maonesho hayo wamekuwa pia wakiwasikiliza wateja wao kuhusu mafanikio wanayoyapata pamoja changamoto wanazokumbana nazo kisha kuzipokea na kuzipatia suluhu kupitia ujuzi na huduma mbalimbali.

Anaeleza walipotoka, walipo sasa na matarajio yao

"Moja kati ya jambo muhimu kabisa kwamba tulianza kama wauzaji na badae tukawa wasambazaji wa makampuni ya nje na badae tukaamua kuzalisha vitu ndani ya Nchi, kwahiyo sasa hivi tunadharisha dawa za mifugo ambazo ni za kuua wadudu na vimelea za kutibu pamoja na kuua minyoo pamoja na 'vitamins' na virutubisho mbalimbali, zaidi ya aina 80 ya dawa tunazalisha hapa ndani ya Nchi"anaeleza Mkurugenzi huyo
IMG_20240502_160146_504.jpg

Amesema kuwa jambo hilo ni mafanikio na hatua kubwa sana kwa Tanzania, ambapo ameweka wazi kuwa na kiwanda chao kina cheti cha ubora katika uzalishaji.

Suleiman anaendelea kueleza kwamba "uzalishaji unazidi kuongezeka zaidi ambapo amesema kuwa wakati wanaanza uzalishaji mwaka 2001 walikuwa wanazalisha aina moja ya bidhaa lakini mpaka sasa wanazalisha aina zaidi ya 80."

Amesema kuwa wanaendelea kuongeza uzalishaji na kuwa kwa sasa wapo kwenye mchakato wa ujenzi wa kiwanda kipya kikubwa ambapo amedai kuwa kitakapokamilika kitakuwa kiwanda kikubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki kwenye bidhaa za mifugo na kilimo hatua ambayo anasema kuwa itaongeza wigo wa uzalishaji zaidi.

Ambapo ametaja baadhi ya tija au matokeo chanya yanayoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na kupungua kwa gharama ya bei ya bidhaa mbalimbali za kilimo na mifugo ambazo uzalisha na kusambaza, kukuza na kuchochea shughuli za ufugaji na kilimo nchini sambamba na kuongeza wigo wa ajira, ambapo amedokeza kuwa kwa sasa wanao wafanyakazi zaidi ya 500 ambao wapo katika vitengo mbalimbali, ikiwemo wataalamu wa masuala ya mifugo
IMG_20240502_160230_709.jpg

Mgeni rasmi na washiriki wanapongeza

Aidha kwa upande wa wanufaika wa semina hiyo ambayo imeudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini ikiwemo Naibu Mkurugenzi Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye amemuwakilisha Kaimu Mkurugenzi, Dr. Benezet Lutege ambaye alikuwa mgeni rasmi, ambaye amepongeza jitihada zinazofanywa na kampuni hizo.

Ambapo amesisitiza kuwa milango na masikio ya Serikali yapo wazi katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo wanaweza kukutana nazo katika utendaji huku akidai kuwa Serikali imekuwa ikiendelea kuweka mazingira rafiki kwa watu kuwekeza pamoja kuchochea mazingira rafiki kwenye kilimo.

Eva Lwabona mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni kati ya wanufaika wa huduma hizo amewapongeza wadau hao kwa kuandaa semina hiyo akidai kuwa inawaleta kwa pamoja na kutoa nafasi ya kueleza changamoto zao kwa wataalamu kisha kupata suluhu.
IMG_20240502_160156_867.jpg

Lakini ametoa wito kwa Serikali kuwawekea mazingira rafiki zaidi wananchi kuingia kwenye fursa za kilimo na mifugo ikiwemo kutumia nyaraka mbalimbali mfano NIDA kuwakopesha baadhi ya watu ambao tayari wameonesha nia ya ufugaji na kilimo ili waweze kukuza mitaji yao.

Nae John Kilo raia Congo DRC amepongeza wadau hao akisema kuwa kupitia semina hizo amejifunza mambo mbalimbali ambayo anaamini yatamsaidia katika uwekezaji wake.

Amesema wazi kuwa Congo ni imekuwa ikinufaika na bidhaa za Farmbase, Farmers center jambo ambalo ametoa wito kwa wadau hao kuendelea kuwasogezea huduma zaidi kwa uharaka ili kuwafikia zaidi watu wengi ambao wanatamani kupata huduma hizo.
IMG_20240502_160234_646.jpg

Semina hiyo ambayo iliongozwa na kauli mbiu isemayo 'Boresha mifugo na kilimo kuongeza kipato binafsi na kwa Taifa" imeambatana na mada mbalimbali zilizowasilishwa na wataalamu kutoka waandaaji, maswali na maoni kutoka kwa washiriki pamoja na maonesho ya baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kusambazwa ikiwemo madawa ya kuku, dawa za kuua kufukuza wadudu kwenye mazao, sambamba na zana mbalimbali za kuwekea dawa hizo kwa ajili ya kunyunyizia kwa mifugo na kwenye mazao.
 
Back
Top Bottom