JKCI yashirikiana na wataalamu kutoka Muntada Aid kuwafanyia upasuaji watoto 40 wenyewe matatizo ya moyo

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
133
225
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) inaendesha kambi maalumu ya siku tano ambayo inaokoa zaidi ya Bilioni moja kwa Watoto 40 ambao wangetakiwa kulipia matibabu ya upasuaji wa mshipa ya moyo kwa kupasua kifua pamoja na tundu dogo.

Akizungumzia Kambi hiyo ambayo imewakutanisha wataalamu kutoka taasisi ya Muntada Aid wanaotekeleza mradi wa 'Little Heart', Mkurugenzi JKCI, Dr. Peter Richard Kisenge April 25, 2024 amesema kuwa wataalamu hao ambao wamekuja kwenye hospitali hiyo kutokea mataifa mbalimbali, tayari wamewafanyia upasuaji watoto 24 kati ya 40 ambao wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo ndani ya siku tano.

Amesema kuwa lwataalamu hao kupitia taasisi yao wamewezesha vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Bilioni moja, ambavyo amesema kuwa vitabakia kwenye hospitali hiyo.

Sambamba na tija hiyo amesema kuwa kambi hiyo inawawezesha wataalamu wenyeji kuendelea kupata ujuzi ambao unaendelea kuboresha uwezo wao wa utoaji huduma.

Ambapo amesisitiza kuwa kati ya sababu zilizowavutia wadau hao wadau hao ni uwekezaji uliofanywa na Serikali katika miundombinu ya vifaa pamoja na kukuza utaalamu wa wafanyakazi wa taasisi hiyo kupitia programu mbalimbali.

Kwa niaba ya wengi hao, Dr. Kabiri Miah ambaye ni Mkuu wa programu kutoka Muntanda Aid United Kingdom amesema kuwa kambi hiyo inaendelea vizuri na kuwa wamekuwa wakishirikiana na JKCI katika masuala mbalimbali ya kitaalumu.

Hata hivyo wamepongeza taasisi hiyo ikiwemo Mkurugenzi wa JKCI kwa kuendeleza mashirikiano yenye tija kwa kuwasaidia wananchi wenye matatizo hususani ya moyo.

Kabir Miah amesema shirika hilo lenye makazi yake London linatekeleza miradi mingi ikiwemo afya, elimu na maji na linafanya kazi katika mataifa mbalimbali ambapo kwa Afrika linafanya kazi katika nchi 30 ikiwemo Tanzania.

Aidha kwa Dr Sulende Kubhoja ambaye ni Dakitari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, amewahasa wazazi na walezi kuwa msatari wa mbele kuwawesha watoto kupata chanjo mbalimbali ambazo uratibiwa na Serikali, ambapo amedai kuwa chanjo hizo zina tija kuwalinda watoto na magonjwa mbalimbali.
 

Attachments

  • images - 2024-04-26T125512.693.jpeg
    images - 2024-04-26T125512.693.jpeg
    30.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom