JKCI yatambulisha huduma maalum itakayowezesha baadhi ya wenye matatizo ya moyo kutibiwa wakiwa nyumbani

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
133
225
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imetambulisha rasimi huduma maalumu inayotambulika kama 'home-based care' ambayo itawawezesha wagonjwa wenye changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakishughulika nazo kupatiwa huduma wakiwa majumbani kwao.

Akizungumza wakati akitambulisha huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dr. Richard Kisenge amesema kuwa huduma hiyo inaanza kutolewa hususani wahitaji ikiwalenga wagonjwa ambao utibiwa kwenye hospitali hiyo, ambapo amedai kuwa wagonjwa hao wakiwa majumbani kwao wanaweza kuendelea kunufaika na matibabu kupitia utaratibu wa huduma majumbani (home-based care).

"Hii ni huduma ambayo sisi Taasisi ya JKCI tutakuwa tunawahudumia wagonjwa pale walipo nyumbani hususani wagonjwa ambao walikuwa wamelazwa hapa hospitalini na wameruhusiwa kwenda nyumbani lakini bado wanahitaji uangalizi maalumu. Kwahiyo wale wagonjwa wakiwa nyumbani sisi tunaweza kuendelea kuwahudumia"

Pia Dr. Kisenge ambaye ni Daktari bingwa wa maswala ya moyo amesema kuwa wanatarajia kutumia vifaa mbalimbali vya teknolojia, akitolea mfano kuwa wataweza kutumia kitambaa ambalo mtu atakuwa anakilalia kwenye kitanda chake, ambapo kupitia kitambaa hicho ambacho kitakuwa kimeunganisha na nyenzo nyingine watagundua mapigo ya moyo, presha na oxygen kwa muhusika kupitia kwenye mifumo wao wakiwa ofisini.

Ameongeza kuwa kupitia teknolojia hiyo mgonjwa akiwa nyumbani, wao wataweza kubaini hali ya mgonjwa kama presha yake imepanda au imeshuka pamoja na masuala mengine ambayo ameyabainisha ikiwemo mapigo ya moyo.

"Hii ni teknolojia mpya ambayo hipo nchini India lakini tumeileta kwenye Taasisi yetu kwamba mgonjwa anakuwa na kitanda chake tunamuwekea hicho kitambaa, hicho kitambaa kitakuwa kinapima mapigo yake ya moyo, kinapima presha yake na oxygen yake akiwa nyumbani" amesema Dr. Kisenge

Amesema kuwa wamejipanga kwa huduma hiyo ambayo itakuwa na vifaa maalumu vitakavyowezesha huduma hiyo kutekelezeka kama inavyokusudiwa.

Aidh daktari bingwa wa masuala ya moyo, Smita Bhalia amefafanua zaidi huduma hiyo itakavyokuwa, huku akidai kuwa hata kama haujawai kutibiwa kwenye hospitali hiyo unaweza kunufaika na huduma hiyo katika mazingira tofauti.

"Kwenye Home-based Care tunachokifanya ni kwamba mgonjwa ahitaji kuja hospitali au mgonjwa ambaye hali yake ni mbaya amesharuhusiwa hospitalini lakini akawa anahitaji uangalizi wa karibu sana wa Madaktari au Nesi tunaweza kumfuata mgonjwa popote alipo nyumbani kwake" ameeleza Daktari huyo

Ameongeza kuwa " Kama anahitaji huduma ya masaa 24 tunaweza tukatoa Nesi akawa anamuangalia muda wote au kama mgonjwa ameshafanyiwa upasuaji na bado ana kidonda ila anaendelea vizuri, anaweza akaenda nyumbani wahudumu wetu wakawa wanamfuata nyumbani wanamuangalia kidonda, wanaweza wakamsafisha kidonda ili aendelee kukaa katika mazingira ya nyumbani lakini bado anaendelea kupata huduma nyumbani."

Anasema kama inapoweza kutokea ngonjwa amebadilika ghafla kupitia utaratibu huo utawezesha Daktari kwenda kumuona mgonjwa ili kuona yupo katika hali ya aina ipi ili kushauri hatua za kuchukuliwa kulingana na hali ambayo atamkuta nayo.

Katika kufanikisha hilo Mkurugenzi wa JKCI, Dr. Peter Richard Kisenge amesema kuwa tayari wanayo magari ya huduma za dharura (ambulance) zaidi ya matano ambayo yatakuwa sehemu ya kuwesha huduma hiyo ambayo inaratibiwa kwa utaratibu maalumu.

Screenshot_20240424-093047_1.jpg
Screenshot_20240424-093021_1.jpg
Screenshot_20240424-093112_1.jpg
 
Back
Top Bottom