Jumla ya ada ya kusoma degree ya udaktari katika chuo kikuu cha Kairuki kwa miaka yote mitano ni milioni 32, swali langu is it worth it ?

Kwa hiyo hamtaki kuwa na madaktari wa kutosha?

Hamtaki kugundua mambo katika utabibu?

Mnaishia kufikiria mshahara tu?

Kwani lazima mtu mwenye ujuzi wake afanye kazi Tanzania?

Kwa taarifa yenu hiyo ada ukiiweka katika viwango vya kimataifa ni ndogo sana, tatizo uchumi wenu mdogo tu.

Kwenda medical school kwa ada ya milioni 6.4 kwa mwaka itakuwa ni kati ya ada rahisi kabisa duniani. Kuna watu wanalipa zaidi ya ada hiyo kusomesha watoto shule ya msingi tu. Hapo hapo Tanzania.

Kuna nchi hiyo ni ada ni robo ya ada ya mwaka mmoja tu.
Nilitaka ku-comment nilipoona umemjibu nikasema nisome kwanza kwa kuwa nilikuwa na uhakika utakuwa umempa jibu sahihi. Tatizo la Tanzania ni kuwa watu wanachukulia elimu kama njia ya kupata ajira tu. Yaani watu wankwenda shule ili waajiriwe sehemu nzuri, basi. Ndiyo maana elimu yetu imekuwa na ya kukariri na kusomea kushinda mitihani ili tupate vyeti. Hili limefanya tuwe na ''wasomi'' wengi ambao hawaajiriki popote kwa sababu licha ya kuwa na vyeti, lakini hawana knowledge ya kutosha.
 
View attachment 2893856

Jumla ya Ada kwa Miaka yote mitano: 32,769,250​

Tukumbuke hiyo ni ada tu haijajumlisha gharama za chakula, hostel, stationary, na mengineyo

Swali langu kwa mliosoma ama kusomesha watoto wenu degree ya udaktari Kairuki Is it worth it ?
hii 32,769,250 ikiwa kama mtaji wa biashara kwa form4 failure anaanza nayo, nina uhakika ndani ya miaka miwili huyu mtu akiwa na bidii ya kazi atakua na mtaji wa 100M
 
Nilitaka ku-comment nilipoona umemjibu nikasema nisome kwanza kwa kuwa nilikuwa na uhakika utakuwa umempa jibu sahihi. Tatizo la Tanzania ni kuwa watu wanachukulia elimu kama njia ya kupata ajira tu. Yaani watu wankwenda shule ili waajiriwe sehemu nzuri, basi. Ndiyo maana elimu yetu imekuwa na ya kukariri na kusomea kushinda mitihani ili tupate vyeti. Hili limefanya tuwe na ''wasomi'' wengi ambao hawaajiriki popote kwa sababu licha ya kuwa na vyeti, lakini hawana knowledge ya kutosha.
Ni tatizo kubwa sana. Kuna jamaa mmoja anafanya kazi serikalini alikuwa anasema yeye kaenda kusoma ili aongeze mshahara.

Ameenda kusoma, kahitimu, mshahara wake ukaongezeka kwa sababu kahitimu, kazi yake ile ile, cheo kile kile, lakini kwa sababu kasoma na kahitimu, mshahara wake umeongezeka.
 
13,000$ Kwa maarifa ya udaktari ni sawa kabisa sema tuliowengi hata kula yetu ni shida tunaiona ni ukwasi mkubwa.
 
Hiyo hela unampa kijana unamnunulia mzigo mkubwa wa kutosha wa dawa na vifaa Tiba na usajili wa Phamarcy mbili akizisimamia vizuri miaka miwili anatoboa nawakikishia lakn zaidi ya hapo ataenda kusoma atakuja kuambulia mshahara wa 900k kama take home mpka 700k kwa mwezi jitafakarini wazazi,walezi na ndgu zangu wa JF
 
Back
Top Bottom