Jumla ya ada ya kusoma degree ya udaktari katika chuo kikuu cha Kairuki kwa miaka yote mitano ni milioni 32, swali langu is it worth it ?

Mkuu,

Yeye alichouliza je hiyo ada ina worth na elimu inayotolewa pale?

Inawezekana ikawa ni gharama nafuu ukilinganisha na mataifa mengine hilo hata mimi sipingi na ni shahidi kabisa..

Lakini je tabibu wa hapo ana kitu gani cha ziada ukilinganisha na tabibu wa MUHAS, CUHAS, MUCHAS au vyuo vingine vya Afya?
Is it worth it kwa muktadha gani? Kwa nani?

Swali la is it worth it halijakamilika, kwa sababu halina muktadha.

Tukiwa na genius anayekuja kugundua dawa ya kutibu saratani, ambaye kakosa nafasi kwingine kote, hiyo ada ni cheap sana, kwa sababu huyu genius ukimpa lift kidogo tu ya formal education, anakwenda kugundua dawa itakayokuja kuwa na thamani ya mabilioni ya dola za Kimarekani na kuokoa maisha ya watu wengi sana.

Hapo ada hiyo ni rahisi sana, kwa sababu tutajiunga watu wachache na kuweka scholarship huyo genius asome, tukijua kuwa miaka michache atazalisha faida kubwa sana kwa jamii. Faida ambayo ukiilinganisha na hiyo ada, hiyo ada ni peanuts tu.

Ukiwa na mtu mbumbumbu kwenye kusoma ambaye hawezi kuelewa kitu medical school, hata ada ikiwa bure, huyo it is not worth it kusoma chuo bure, kwa sababu atapoteza muda tu, inawezekana kipaji chake ni soka si medical school. Waliosoma uchumi hapo watajua kuwa hata ukisoma bure bado kuna "opportunity cost".

Sasa, kwa nini tunaishia gia ya kwanza kuuliza swali la "is it worth it" bila muktadha?

Is it worth it for whom? For the right candidate, hiyo ada is very cheap. For the wrong candidate, hata ada ikiwa bure, medical school is not worth it.

Vyuo vya serikali vingi vinakuwa subsidized na serikali na huduma ni mbovu sana. Juzi nilikuwa nasoma uzi unaelezea mtu alivyopata shida ya kunguni, wakaja watu wanatoa ushuhuda kunguni walivyojaa UDSM kwenye vyumba wanavyolala wanafunzi.

Ukitaka huduma standard, ni kazima ulipie hela standard. Watanzania wengi tumelemazwa na Ujamaa, ni hodari wa kudai huduma standard lakini hatutaki kulipia.
 
Jibu zuri. Je elimu inayotolewa kairuki ina worth kulipiwa hiyo ada ?

Value for money ipo kairuki ?

Nashindwa kujibu moja kwa moja swali lako.

Japo kuna wadogo zangu wanasoma pale kairukii na hivyo hivyo kwa MUHAS hakuna utofauti mkubwa sana japo Kwa Mhimbili wapo competent zaidi na elimu inasimamiwa kindakindaki..

Kairuki sana sana ni learning facilities za kutosha hospital nzuri yenye usimamizi mzuri lakini madaktari wanaozalishwa pale ni wa kawaida sio wa kutisha.
 
Hata hujaeleweka unamanisha nini madakitari wa kawaida na sio wakutisha. Hivi unajua kozi ya udakitari kwote kwote duniani inafanana? Kinacha beba mtu ni indivifual intelligence au talent sio chuo.
Kwa swali la mleta mada is it worthy that Amout? Money is not comparablr to education whatsoever ever stuation or course. If you think education is expensive afford ignorance and see.
 
Is it worth it kwa muktadha gani? Kwa nani?

Swali la is it worth it halijakamilika, kwa sababu halina muktadha.

Tukiwa na genius anayekuja kugundua dawa ya kutibu saratani, ambaye kakosa nafasi kwingine kote, hiyo ada ni cheap sana, kwa sababu huyu genius ukimpa lift kidogo tu ya formal education, anakwenda kugundua dawa itakayokuja kuwa na thamani ya mabilioni ya dola za Kimarekani na kuokoa maisha ya watu wengi sana.

Ukiwa na mtu mbumbumbu kwenye kusoma ambaye hawezi kuelewa kitu medical school, hata ada ikiwa bure, huyo it is not worth it kusoma chuo bure, kwa sababu atapoteza muda tu, inawezekana kipaji chake ni soka si medical school.

Sasa, kwa nini tunaishia gia ya kwanza kuuliza swali la "is it worth it" bila muktadha?

Is it worth it for whom? For the right candidate, hiyo ada is very cheap. For the wrong candidate, hata ada ikiwa bure, medical school is not worth it.

Vyuo vya serikali vingi vinakuwa subsidized na serikali na huduma ni mbovu sana. Juzi nilikuwa nasoma uzi unaelezea mtu alivyopata shida ya kunguni, wakaja watu wanatoa ushuhuda kunguni walivyojaa UDSM kwenye vyumba wanavyolala wanafunzi.

Ukitaka huduma standard, ni kazima ulipie hela standard. Watanzania wengi tumelemazwa na Ujamaa, ni hodari wa kudai huduma standard lakini hatutaki kulipia.

Kiranga,

Binafsi nimekuelewa sana japo embu tujaribu kutengeneza mazingira ya kufanya factors zote zibaki constant.

Kisha tu subject wanafunzi wawili wenye level moja kwenye IQ labda wote wana 80% kwenye vyuo viwili mmoja MUHAS kisha mwingine Hubert Kairuki je Ada ya Kairuki ina worth na yule mtaalam tutayempata After 6 years ( 1 year for intern)..?

Wakati huo huo turudi na MUHAS tukijaribu kufanya comparison kwa yule ndugu yetu mwingine mwenye 80% pia...

Ni nini cha zaida kwa Hubert Kairuki?
 
View attachment 2893856

Jumla ya Ada kwa Miaka yote mitano: 32,769,250​

tukumbuke hiyo ni ada tu haijajumlisha gharama za chakula, hostel, stationary, na mengineyo

swali langu kwa mliosoma ama kusomesha watoto wenu degree ya udaktari Kairuki Is it worth it ?
Si Bora hio pesa umpe kijana aanzishe biashara!? na anaweza kuwa tajiri mkubwa kuliko hata, itakacho msaidia hio degree!!
 
Muuza chips tu kwa siku akikosa anakunja elfu 30, faida, kwa mwezi laki ,9
Muuza chips anapata faida ya laki tisa kwa mwezi ukimaanisha anamzidi daktari, basi taja muuza chips aliyefungua chuo au hoteli nami nikutajie madaktari waliofungua hospitali.

Kairuki yenyewe yenye mjadala hapa ni zao la daktari unayedai anazidiwa na muuza chips, tena ana na hospitali ukiachana na chuo. Au wauza chips nao wana vyuo
 
Umesema unadhani wakati data zipo, kwanini usiache kudhani ukauliza ndio useme. Au kama hujui ukanyamaza wanaojua waseme. Ona sasa umepotosha

Wewe toka uzaliwe hujawahi kudhani jambo lolote?

Huwa upo accurate katika kila kitu?

Kama unajua fee structure ya kila chuo precisely kwanini usiweke mpaka usubirie kunikosoa mimi ninayedhani?

Kuwa muungwana.
 
Kiranga,

Binafsi nimekuelewa sana japo embu tujaribu kutengeneza mazingira ya kufanya factors zote zibaki constant.

Kisha tu subject wanafunzi wawili wenye level moja kwenye IQ labda wote wana 80% kwenye vyuo viwili mmoja MUHAS kisha mwingine Hubert Kairuki je Ada ya Kairuki ina worth na yule mtaalam tutayempata After 6 years ( 1 year for intern)..?

Wakati huo huo turudi na MUHAS tukijaribu kufanya comparison kwa yule ndugu yetu mwingine mwenye 80% pia...

Ni nini cha zaida kwa Hubert Kairuki?
Unalinganisha chuo cha private ambacho hakipati direct au indirect subsidies za serikali na chuo cha serikali ambacho kimepata direct na indirect subsidies za serikali.

Hizo ada za MUHAS si ada zinazoakisi gharama halisi, kwa sababu ni ada zilizopunguzwa sana kwa kusaidiwa na ruzuku za serikali kwenye chuo cha serikali.

Mpaka hapo hujalinganisha vitu viwili vilivyo sawa.

Pia, unaweza ku prefer elimu ya ada ndogo bila kujua hiyo ada ndogo inakuwekea costs nyingine nyingi tu, mfano nimeongelea habari za wanafunzi wa UDSM wanavyolalamika kuwa na kunguni vyumbani mwao. Hii si elimu ya kwenye mazingira standard.

Kuhusu Kairuki wana nini cha zaidi kulinganisha na Muhimbili, hilo si swali zuri la kuuliza, kwa sababu Muhimbili wanapata ruzuku kubwa sana.

Ma Profesa wa Muhimbili hawategemei ada za wanafunzi, wale wanalipwa mishahara na serikali bila kujali ada za wanafunzi, gharama za kuendesha chuo Muhimbili hazitegemei ada za wanafunzi, hizi nibsehemu ya bajeti ya Wizara ya Afya.

Huko private universities hawana hiyo privilege ya ruzuku za serikali kihivyo, inawabidi wategemee ada za wanafunzi.

Swali zuri kabisa, ni, je, gharama za uendeshaji wa private universities, mishahara ya ma profesa, gharama za majengo, labs, huduma nyingine kama za malazi kama zipo (habari za usafi kuepuka kunguni zinaingia hapo) research facilities etc, standard, zinaendana na hizo ada?
 
Muuza chips anapata faida ya laki tisa kwa mwezi ukimaanisha anamzidi daktari, basi taja muuza chips aliyefungua chuo au hoteli nami nikutajie madaktari waliofungua hospitali.

Kairuki yenyewe yenye mjadala hapa ni zao la daktari unayedai anazidiwa na muuza chips, tena ana na hospitali ukiachana na chuo. Au wauza chips nao wana vyuo
Mkuu,

Hii hoja ya watu fikra zao kuishia kwenye mshahara mdogo wa Tanzania inasikitisha sana.

Yani watu washakubali kabisa kwamba daktari Mtanzania hawezi kugundua dawa akaifanyia international patent na kusaidia watu wengi sana na hapo hapo kupiga hela katika biashara kubwa sana ya hiyo dawa?

Au hata asipogundua dawa, hapo hapo kwenye mshahara tu, hawajui kwamba daktari anaweza kusoma Tanzania akaona mshahara mdogo Tanzania akaenda nchi nyingine yenye mshahara mkubwa kufanya kazi huko?
 
Hata hujaeleweka unamanisha nini madakitari wa kawaida na sio wakutisha. Hivi unajua kozi ya udakitari kwote kwote duniani inafanana? Kinacha beba mtu ni indivifual intelligence au talent sio chuo.
Kwa swali la mleta mada is it worthy that Amout? Money is not comparablr to education whatsoever ever stuation or course. If you think education is expensive afford ignorance and see.

Covax,

Individual intelligence kama unavyozungumzia wewe pekee bila nafasi ya chuo haitoshi.

Kama mazingira ya kujifunzia yana walakini bado hiyo intelligence yako ni bure.

Kama kuna wahadhiri wa viwango, vifaa, na mazoezi ya kutosha hivi vina add sehemu kubwa hata kwenye hiyo intellegence unayoongelea.

Na medicine sio kama degree zingine hii imekaa kimazoezi zaidi na kupata ustadi kunahitaji sehemu ya walimu na mazingira wezeshi..

Na ndomana kuna clinical rotations sasa huku huwezi kutoboa kama msingi wako huku chini ni butu.

Mimi nimesema Kairuki ni njema zaidi kwenye kusaidia mwanafunzi kwa ku provide learning facilities za kutosha maana ni chuo cha private hilo unatakiwa utambue.

Lakini sio kwamba tabibu wa Kairuki ni bora zaidi kuliko wa chuo cha Muhimbili au Bugando. Madaktari tunawajua, tunawaona na wanatueleza hivyo tunatambua.
 
Walioanzisha biashara wot ni matajiri?
Daktari atatibu watu huo ni utajiri tosha.
Hivi lazima wote tuwe matajiri?
Kuishi maisha standard ndio muhimu.
Watu masikini (nakusudia umasikini wa akili zaidi, umasikini ulio mbaya kuliko wote) siku zote hawawezi kufikiri zaidi ya mshahara na pesa.

Yani ukiwaambia habari za maisha standard, kitu cha kwanza wanachofikiria ni gharama za ki fedha za kufikia maisha hayo standard.

Hawajui kabisa kuhusu the power of ideas na jinsi ideas zinavyoweza kufanya mambo makubwa kuliko hata fedha.
 
Unalinganisha chuo cha private ambacho hakipati direct au indirect subsidies za serikali na chuo cha serikali ambacho kimepata direct na indirect subsidies za serikali.

Hizo ada za MUHAS si ada zinazoakisi gharama halisi, kwa sababu ni ada zilizopunguzwa sana kwa kusaidiwa na ruzuku za serikali kwenye chuo cha serikali.

Mpaka hapo hujalinganisha vitu viwili vilivyo sawa.

Pia, unaweza ku prefer elimu ya ada ndogo bila kujua hiyo ada ndogo inakuwekea costs nyingine nyingi tu, mfano nimeongelea habari za wanafunzi wa UDSM wanavyolalamika kuwa na kunguni vyumbani mwao. Hii si elimu ya kwenye mazingira standard.

Kuhusu Kairuki wana nini cha zaidi kulinganisha na Muhimbili, hilo si swali zuri la kuuliza, kwa sababu Muhimbili wanapata ruzuku kubwa sana.

Ma Profesa wa Muhimbili hawategemei ada za wanafunzi, wale wanalipwa mishahara na serikali bila kujali ada za wanafunzi, gharama za kuendesha chuo Muhimbili hazitegemei ada za wanafunzi, hizi nibsehemu ya bajeti ya Wizara ya Afya.

Huko private universities hawana hiyo privilege ya ruzuku za serikali kihivyo, inawabidi wategemee ada za wanafunzi.

Swali zuri kabisa, ni, je, gharama za uendeshaji wa private universities, mishahara ya ma profesa, gharama za majengo, labs, huduma nyingine kama za malazi kama zipo (habari za usafi kuepuka kunguni zinaingia hapo) research facilities etc, standard, zinaendana na hizo ada?

Hapa nimekuelewa nimejifunza kitu pia chief.
 
Mkuu,

Hii hoja ya watu fikra zao kuishia kwenye mshahara mdogo wa Tanzania inasikitisha sana.

Yani watu washakubali kabisa kwamba daktari Mtanzania hawezi kugundua dawa akaifanyia international patent na kusaidia watu wengi sana na hapo hapo kupiga hela katika biashara kubwa sana ya hiyo dawa?

Au hata asipogundua dawa, hapo hapo kwenye mshahara tu, hawajui kwamba daktari anaweza kusoma Tanzania akaona mshahara mdogo Tanzania akaenda nchi nyingine yenye mshahara mkubwa kufanya kazi huko?

Watanzania bado wapo kwenye zama za ujima ya kwamba wagunduzi ni wazungu.

Lakini huwa najiuliza tuna MDs, Biotechnologists, Microbiologists, Pharmacists etc kweli wameshindwa kutengeneza patentable subject matter yoyote na kupasua anga?

Sema Juzi kati hapa nimeona Prof mmoja wa Microbiology pale UDSM anaitwa Tibuhwa ni mmama fulani hivi wamepata patent kwenye issues za mycology nadhani.

Hii inatakiwa iwe na muendelezo hasa kwenye Afya na life science in general.
 
Kwahiyo inakuwa around 45 millions.
Ni mjinga pekee atatoa hiyo pesa ili mwanae aajiriwe kwa shida na kulipwa milioni 1.
Ikumbukwe pia mtaani kuna madaktari waliokosa ajira , wamekwenda private wanalipwa laki 6 , laki 7 au pungufu. Na kupata huko private mpaka uunganishwe.
Mgambo miezi 5 bure Mwembeyanga ukipata ajira Bandari kama mlinzi mshahara wako unamzidi Daktari.
Vijana machaguo ni yenu
Hivi daktari fresh from Kariuki (medical doctor) akiajiliwa private,mfano pale TMJ analipwa shingapi?
 
Back
Top Bottom