Jinsi ya kujenga tabia ya kusoma vitabu kwa mafanikio

Call me GHOST

Member
Jan 18, 2019
53
95
Umekuwa ukitamani kuwa na tabia ya usomaji vitabu kila siku lakini kila ukijaribu unashindwa USIJALI ngoja nikupe mbinu nzuri unayoweza itumia kwa mafanikio makubwa.

Anza leo kutumia 'Pomodoro Technique' kwa kusoma kitabu kwa dakika 25 kisha pumzika kwa dakika 5 na ndani ya dakika hizo 5 jaribu kutafakari yale yote uliyoyasoma kwa dakika 25 kuna mtu mmoja aliwahi kusema kwamba "If you never stop and think when you read a book, You aren't learning" ikiwa na tafsiri isiyo rasmi kwamba "Kama haujawahi kupumzika na kutafakari wakati unasoma kitabu basi jua kwamba haujifunzi hapo".

Changamoto nyingine inayowakuta watu wengi ni kutaka kusoma kila kitabu kinachotumwa humu au wanachokutana nacho mahali pengine bila kujua kwamba sio kila kitabu ni kwa ajili yako rafiki vingine viache vikupite tu lakini ngependa kukushauri utumie hii mbinu ambayo mimi binafsi naitumia kama itakufaa ichukue na uanze kuitumia leo.

Mbinu hii inaitwa 2C's kwa kirefu ni 'CURE and CURIOSITY' yenye maana kwamba unachagua kitabu kutokana na hizo sababu mbili yaani cure na curiosity.

Mosi, Chagua kitabu ambacho unaona kitakuwa CURE kwenye tatizo ulilo nalo au hali unayoipitia kwa wakati huo kwa mfano kama una tatizo la kiuchumi,kimahusiano,kitabia n.k unalohitaji kulitatua au kupata mawazo mbadala juu ya hali hiyo basi bila shaka kitabu kinachohusu masuala ya uchumi, mahusiano, Self growth n.k kitakufaa kutokana na changamoto uliyonayo ambayo unahitaji kuitatua au kupata mawazo mapya na fikra tofauti za namna ya kukabiliana nayo.

Ukiwa unataka kuacha tabia kadhaa na kutengeneza tabia kadhaa mpya lazima utafute vitabu vinavyoweza kutatua shida yako hii

Ukiwa hauna matumizi mazuri ya kipato chako na unatamani uanze kuweka akiba n.k bila shaka kitabu kitakachokufaa kwa wakati huu ni kile kinachoweza kukupa elimu ya namna ya kukabiliana na hali uliyonayo.

Ukiwa unapitia changamoto za kimahusiano either ya kimapenzi au ya kijamii bila shaka vitabu vinavyoweza kutatua changamoto yako vipo vitafute kwa kifupi ni kwamba unasoma kitabu ambacho unahisi kitakubadili mtazamo au kuponya matatizo yako baada ya kumaliza kukisoma.

Pili, Chagua kitabu unachoona kinaendana na CURIOSITY uliyonayo kwa wakati huo. Kama unahisi ndani yako upo willing kujua jambo fulani au topic fulani kiundani basi tafuta vitabu vinavyohusu hiyo topic na usome kiundani sana(In-depth learning) lakini kadri unavyosoma utakutana na baadhi ya mawazo au concept zinazofanana na ulizosoma either kwenye kitabu kingine au mahali pengine hivyo basi kuwa mtu wa kufanya kitu kinaitwa "Joining of knowledge trees" kwa kuunganisha hizo concept kutokea kwenye vyanzo tofauti tofauti itakusaidia sana.

Kama unatamani kujua kiundani kuhusu biashara bila shaka vitabu unavyotakiwa usome vinatakiwa vihusiane na biashara

Kama unahitaji kujua histori za watu waliofanikiwa bila shaka vitabu vya biographies zao vipo unaweza vitafuta ukavisoma

Kama unatamani kubadilika kwenye masuala fulani bila shaka vitabu vinavyohusiana na eneo unalohitaji kubadilisha vipo vya kutosha

Chagua kitabu cha kusoma kutokana na sababu maalum unayohitaji kujifunza kwa wakati huo usisome tu ilimradi uonekane na wewe unasoma vitabu

Ukijiwekea utaratibu wa kusoma wastani wa kurasa 10-25 kwa siku kwa mwezi utakuwa na uhakika wa kusoma kurasa 300-750 wastani wa kitabu kimoja mpaka vitatu kwa mwezi hivyo kwa mwaka utakuwa umesoma wastani wa kurasa 3600-9000 sawa na wastani wa zaidi ya vitabu 10-30 ambavyo vinaweza kuyabadili maisha yako kabisa kama utakuwa unayafanyia kazi yale unayoyasoma na sio kuishia tu kuyasoma.

Mwisho kabisa nikuache na hii kauli "You don't learn when you read it, You do when you use it" ikiwa na maana kwamba "Haujifunzi kwa kusoma pekee bali unapokifanyia kazi kile ulichokisoma hapo ndio unakuwa umejifunza".

•READ ->APPLY ->READ AGAIN

Ghost..! (ciao)

IMG_20210706_210308.jpg
 
Sawa Mkuu.! Mie niko nasoma kitabu changu cha Napoleon Hill. Na nitaanza kutumia hiyo mbinu yako
 
Back
Top Bottom