Hivi ni kweli kusoma vitabu kunaweza kubadilisha maisha ya mtu? una ushahidi wowote?

hermanthegreat

JF-Expert Member
Mar 2, 2021
861
2,050
Wakuu habari,

Kwanini watu waliowahi kufanya makubwa hawakufanikisha hayo kupitia kusoma vitabu.

Unakuta mtu anasoma kitabu cha How to influence people lakini hadi anakimaliza hana influence yoyote.

Mtu anaandika kitabu cha how to get rich fast afu pesa ya kuchapisha hicho kitabu amekopa.

Kiufupi nawaza hivi , huenda watu wengi wanaopenda kusoma vitabu huwa ni kwa lengo la kujifariji tu.

Ila mwalimu mzuri wa maisha yako ni uzoefu wako mwenyewe.

Kusoma vitabu ni sawa na kujaribu kujifunza kupitia maisha ya watu wengine huku ukijua maisha ya mwanadamu hayajirudii.

Kitabu kimewahi kubadilisha maisha yako kwa kiasi gani.
 
Kuna namna fulani fikra zangu zilibadirika baada ya kukiri na kufuata mafundisho ya mwalimu wangu Marcus Aurelius.
Soma kutabu chake utaelewa
FB_IMG_17085009307596772.jpg
 
😂😂maisha hayana formula in actuality ,mengi ni Mungu and bieng at the right place at the right time.
utakuta dogo ni domo zege anasoma kitabu kuhusu kuapproach madem, akimwendea Mariamu wazee wazima wanachomoa vile vikaratasi vina sura ya nyerere vya 10k , nguvu ya hela na milaini ya poem ipi itashamiri???
Knowledge has its place na maisha na mafunzo yake yana nafasi yake
 
Watu wasichoelewa ni kuwa
Vitabu vina umuhimu kama ukiwa level flan hivi ya economy.

Sio mwenzangu na mimi ndo kwanza unajitafuta unataka kusoma vitabu.
Hutoelewa utaona mambo ya hovyo tu.
Sisi wa kujitafuta vitabu vyetu kama hivi.
Raisi na mke wangu
Dereva taxi
Penzi la kipofu
Na vingine vingi kama hivo😂😂😂😂

Ila hivi vya sijui
Miracle of subconscious mind waachieni kina mshana na kiranga.
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Soma vitabu kwa ajili ya kupata technical skills tu(ujuzi wa kiufundi) mfano jinsi ya kupiga vinanda nk

Ushauri wa kimaisha(mahusiano, ndoa, uchumi) tafuta wenye uzoefu au ambao wameshaweza

Vitabu vya ushauri wa kimaisha vina ushauri wa jumla tu havikuongezei chochote. Mfano utaambiwa ili utajirike, weka akiba, sasa nani hajui?

Mwishoni unaingia kwenye mtego wa kusoma kitabu baada ya kitabu, ukitafuta kile kitu flani kitakachosisimua akili yako na kufanya upige hatua....

Na utakua unachukulia kama kusoma mavitabu ni sehemu ya kufanikiwa, yaani unasoma huku unavuta picha unafanya unayosoma(mental masturbation)
 
Elon Musk alikuwa na interests na masuala ya rockets na anga.
Alinunua vitabu vingi kuhusu rocket science akasoma akaelewa mengi.

Inaanza na interests, waandishi wa vitabu hufanya research ya muda mrefu, vitabu ni njia nzuri kujifunza kwa sababu vinakuwa deep sana kuliko video tutorials.

Kama unapenda mechanics soma vitabu vya mechanics.... Kama unapenda ujenzi tafuta vitabu vya ujenzi na hapo utaona msaada wa vitabu.
 
Back
Top Bottom