dr namugari
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 9,779
- 16,582
Mwaka 2014 nilishawishika kwa mara kwanza kuekeza kwenye biashara za hisa, Basi nikapata abcd za namna gani na faida za za kuekeza kwenye masoko ya hisa na nikafanya maamuzi ya kununua hisa katika kampuni moja ya uchimbaji na utafutaji wa mafuta inayoitwa Swala energy.
Basi nikapewa list ya kampuni zilizo listed katika soko la hisa Dar es Salam stock exchange ndipo nikachagua kampuni hiyo kwa vile ndio ilikuwa inafanya IPO yaani initial public offer kwa Mara ya kwanza, na mimi nikashawishika na nikaamua kununua hisa za milioni mbili kila hisa Moja iliuzwa 500 hivyo nikafanikiwa kununua hisa za 2m sawa na hisa elfu 4000.
Basi baada tu ya kununua hisa ktk kampuni hyo baada ya week mbili hisa zikapanda value kutoka 500 Hadi 1000 kwa kila Moja nikataka kuuza nikaambiwa na jamaa angu kuwa nisubiri kwa vile itaendelea kupanda Kweli baada ya Kama miezi miwili hivi hisa ktk kampuni hyo ikashuti Hadi kufika 2100 nikaona wacha niuze.
Jamaa yangu ambae ni mzoefu akaniambia nisiwe na haraka zitaendekea kupanda zaidi na tutapiga pesa ndefu za maana.
Wakati nikitamani kuuza hisa zangu nikaanza kuona zikistak ikibakia palepale kwa muda wa kama mwezi nzima bila kupanda wala kushuka.
Ajabu ghafla bin vuu nikaanza kuona inaporomoka Tena Bei zake nikaanza kutafuta dalali aniuzie, mimi kipindi hicho niko Tabora ikawa kama simuamini dalali yule kwani yeye alitaka nimtumie dcm zangu zote nikaona nikipata chance nikimbie Dar faster nikaziuze.
Kadri siku zinavyozidi kwenda na mimi kubanwa na kazi nilishutukia hisa zimeporomoka kwa kasi ya kutisha na kumpata mteja ikawa ngumu pia 😂 aise hyo ni biashara kichaa sana yaani una hisa zako ila kupata mteja wa kuzinunua hupati.
Kuna wakati nimecheki mwenendo wa hiyo kampuni nikakuta hisa Moja Ni 234, hisa zimeporomoka Sana nikakata tamaa kabisa nimetulia na Sina pa kupeleka kesi hiyo.
Kama kuna wazoefu nipeni mbinu nifanye nini ili niweze kurescure hicho hisa zangu hata Kama zimeporomoka Bei, kampuni haijawi kunipa gawio Wala kuitwa mkutano mkuu wa mwaka kwa kifupi ni matapeli wa enz za JK ndio waliniingiza mjini for the first time
Kweli sina hamu kbsa kwenye masoko ya hisa na mamlaka zake za mitaji na dhamana hi biashara imekaa kitapeli sana.
Na mbaya zaidi Magu alivyoingia madarakani masoko ya hisa likawa Kama kaburi wazi.
Niwaonye vijana kuweni makini na hayo Mambo ya hisa Kuna utapeli Sana unaendelea sana.