Jifunze silaha kuu tano (5) za ulimwengu wa kiroho ili upate ushindi kwenye kila jambo

Nawasalimu wote wanajukwaa,leo nataka tujifunze silaha kuu tano zinazotumika katika ulimwengu wa kiroho.

Kama wengi tunavyojua kuwa katika ulimwengu wa kiroho kuna falme kuu mbili,falme ya kwanza ni ufalme wa nuru na falme ya pili ni ufalme wa giza.

Falme zote hizi zina muundo na uongozi na mamlaka kamili.Katika viumbe vyote binadamu ndiyo kiumbe pekee mwenye sifa ya kuweza kuishi katika ulimwengu wa kiroho na ulimwengu huu wa kimwili kwa wakati mmoja.Inawezekana umesoma vitabu vingi sana na kufanya jitihada nyingi sana ili ufanikiwe katika maisha yako lakini bado umeshindwa.

Nakushauri fuatilia darasa hili kwa umakini na siku ukimaliza Lazima ufanikiwe kwa kuwa manbo yote huanzia katika ulimwengu wa kiroho na ndicho utakachojifunza hapa.

Zifuatazo ni silaha kuu tano za ulimwengu wa kiroho.
1. Damu
2. Jina
3. Kiti
4. Maneno
5. Ardhi na Mbingu

Ukiweza kujifunza silaha hizi kwa umakini,utaweza kujua ulimwengu wa kiroho unavyofanya kazi,utapata nguvu za kuingia katika ulimwengu wa kiroho,utashinda vita vya kiroho na kimwili kwa urahisi na utafanikiwa kimwili na kiroho katika mambo yako.

Somo hiki litakuwa na jumla ya vipande kumi (10),yaana tutajadili silaha moja moja inavyotumika katika ulimwengu wa kiroho upande wa ufalme wa giza na moja moja inavyotumika katika ulimwengu wa kiroho upande wa ufalme wa nuru.

Naomba maoni yenu ya tuanze kuijadili silaha ipi, na tuanze na falme ipi kati ya falme ya nuru au ya giza au somo liishie hapa maana watu wengi hawaamini kama kuna ulimwengu wa kiriho.
an
silaha pekee ni mbili tu, Jina la Yesu, na Damu ya Yesu. Jina la Yesu kwa kutoa mamlaka na kufukuza au kukemea chochote, na Damu ya Yesu kwa kukiri kama ushuhuda wa ile ilikifanya na kuamuru vifungo na takataka zote ziondoke kwasababu Damu ya Yesu ilimaliza kila kitu. Shetani hufuata sheria, na akiona kisheria hana haki kwako, ukimfukuza kwa kutumia mamlaka iliyomshinda, hana namna ila kuondoka.

ukianza kutumia maji, ardhi n.k, ni uganga kama uganga mwingine tu na ni uongo mkubwa sana ambao kanisa la siloamu limedanganya wengi hadi kufikia hatua kusema Damu ya Yesu na Jina la Yesu vimepungua nguvu. Mungu awasaidie.
Ndo umemaliza au!
 
Wachawi, mapepo yoote wanaogopa sana JINA LA YESU
 
Back
Top Bottom