Jifunze silaha kuu tano (5) za ulimwengu wa kiroho ili upate ushindi kwenye kila jambo

4B; MANENO KAMA SILAHA YA KIROHO KATIKA UPANDE WA UFALME WA NURU. Kama tulivyoona silaha hii katika ufalme wa giza, hivyohivyo na katika ufalme huu wa nuru silaha hii inakuwa na nguvu zaidi ikiambatana na silaha ya Kiti. Maneno mtu anayozungumza yanakuwa na uhusiano mkubwa sana na kiti alichokalia, pia unapaswa kujua kila mtu ana kiti cha maisha yake (unatawala maisha yako), hivyo unapaswa kuwa makini na maneno unayojitamkia na unayotamkia wengine. Namna ya kupata ushindi na silaha hii; Kwanza unapaswa kujinenea/ kujitamkia maneno mzuri na kusikiliza kwa umakini maneno unayotamkiwa na watu wengine, kama wanakutamkia maneno mazuri unapaswa kuyatia uhai (maneno ni roho) kuulinda uhai huo hadi maneno hayo yatimie kwako kwa kuyapiga muhuri kwenye kiti cha ufalme wa nuru. Kama umetamkiwa maneno mabaya ya kukukwamisha unapaswa kuyatoa uhai kwa haraka kabla maneno hayo hayajaleta matokeo kwako, unayatoa uhai kwa kuyakataa na kuyafuta kabla hayajafika kwenye kiti cha ufalme wa nuru. Jifunze muundo huu ukusaidie; katika ulimwengu wa kiroho kuna kiti cha Mwenyenzi Mungu (Mungu Mkuu) na chini yake kuna kiti cha wazazi wako, chini yake kuna kiti cha maisha yako na mwisho ndipo vinafuata viti vyote (nafasi zote za mamlaka/ uongozi). Kwakupitia muundo huu unaweza kukalia viti vyote ila kamwe hutaweza kukalia au kuwa juu ya kiti cha wazazi wako!. Na hapa ndipo tunapata neno "laana ya wazazi". Laana ya wazazi inatokana na matumizi mabaya ya maneno anayoyatoa mzazi dhidi yako akiwa amekalia hiki kiti chake mbele ya kiti kikuu cha Mwenyenzi Mungu. Maneno hayo ya mzazi yanakuwa na nguvu sana kuliko maneno yanayotolewa na mtu mwingine yeyote au na kiti chochote. Hivyo chunga sana maneno unayotamkiwa na wazazi wako au unayomtamkia mtoto wako. Baraka ya wazazi ni matumizi mazuri ya kiti anachotumia mzazi / wazazi kukunenea maneno mazuri mbele ya kiti cha Mwenyenzi Mungu na akaweza kuulinda uhai wa maneno hayo. Kwakusikiliza maneno ya mtu kunakusaidia kujua malengo yake, makusudi yake, kiti alichokalia, roho iliyopo ndani yake na kusudi la yeye kuishi. Hivyo silaha hii ni muhimu sana kuijua vizuri. Mwisho kwa leo, unapaswa kujua kuwa kila kitu katika dunia hii kama wanyama, ndege, mawe, miti, upepo nk vyote vina maneno (sauti) na vinauwezo wa kukunenea maneno mazuri au mabaya ni wewe tu kutumia hekima yako kutafsiri na kujua chakufanya na chakutokufanya ili vikunenee maneno mazuri mbele ya kiti. Nb; sauti ni tafsiri ya maneno. Na usiogope sana maneno ya mtu bali ugopa zaidi kiti anachokalia anapotamka maneno hayo, maana maneno ya mtu ni tofauti na maneno ya kiti lakini yote yanapitia kwenye kinywa cha aliyekalia hicho kiti.
Mzazi alikutamkia Maneno ambayo ukiwa mtoto ulichukulia kawaida...! Bila elimu ya kiroho bila kujua namna ya kuzuia Uhai wa hayo maneno mabaya kama unavyofundisha hapa...!

Sasa nimekuwa nimekutana na Uzi wako nimerudi nyuma utotoni kukumbuka maneno ambayo Mzazi aliwahi kutamka....!

Naweza kuyafuta....!?
Nayafutaje...!?

Naweza kuyabadirisha yakaleta Maana..!?
Nayabadirishaje....!?
 
KUINUKA KWA ROHO YA MAUTI.
Hii inasababishwa na mambo mengi sana ambayo kwa kujibu swali lako ni ngumu kuyaorodhesha yote hapa.

Ila sababu kubwa zaidi ambazo hupelekea yote haya ni MADHABAHU,MAAGANO,MAMLAKA na UTAWALA wa huyo mtu aliyekusudiwa hiyo roho ya mauti.

Ndoto zote zinazohusiana na watu waliokufa siyo nzuri,wawe ni wazazi,ndg,jamaa na marafiki,au hata watu wasiojulikana.Hizi siyo ndoto nzuri hata kidogo.

Kwasababu roho ya huyo mtu inakuwa na mahusiano na roho za hao waliokufa ambao wao wako katika ulimwengu mwingine; huku aliye hai yuko katika ulimwengu wa mwili.Haitakiwi kuwepo mawasiliano ya watu waliokufa na walio hai,kwa kuwa waliokufa hawajui chochote kinachoendelea hapa duniani.

MTU ATAULIZA KWANINI SASA IWE HIVYO.

Tazama hapa.MUHUBIRI 9:5

"Kwasababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa;lakini wafu hawajui neno lolote,wala hawana ijara tena;maana kumbukumbu lao limesahauliwa."

SASA HUWA NI AKINA NANI TUNAWAOTA KWA SURA TUNAZOZIJUA?

"Mtu anaweza kumuona mzazi wake, mume/mke wake,mtoto wake,rafiki yake n.k,akizungumza naye mambo ya kawaida au hata mambo ya siri na yote hayo yasemwayo ni hakika ,yaani kweli kabisa." Hii isimpe uhalali kwamba yuko katika njia za haki.

Ndio maana unaweza kukuta mtu anasema yeye akiota ndoto huwa ni za kweli,akimuotea mtu hutokea hivyo hivyo kama alivyoota, na wakati huo huo ni mtenda dhambi kama zote.

Hapa kinachofanyika ni mapepo ambayo huvaa sura za hao wahusika na kuja kwa huyo mtu,mara nyingi sehemu za namna hii ni zile zenye chimbuko la kuabudu mizimu,familia za kichawi,kishirikiana,za waganga wa kienyeji, kutambikia mizimu na makafara ya kila aina.

KIUFUPI,ni familia zenye madhabahu ya miungu zilizo hai,mapepo na mizimu ipo mahali hapo,inawaongoza na kuwapa maelekezo ya jinsi ya kuendelea kuitunza hiyo madhabahu ili iendelee kupata huduma, hasa katika KUABUDIWA.

Madhabahu zina mambo mengi,sasa ikiwa katika familia kuna mtu anatembelewa na hiyo roho ya mauti kwa kuota watu waliokufa, kuota sana makaburini,anaota anazikwa, jeneza,sanda, au amekufa. Hapo kuna uwezekano ametumiwa hiyo roho ili imvae na iharibu afya yake,mambo yake na hata uhai wake.Haiji hivi hivi mpaka awepo mtu mwingine wa kuituma.

Ikishatumwa itaamua imuondoe kwa ajali,kuumwa sana,au muda mfupi,kifo cha ghafla, kujiua, kuua na kisha kujiua.

Na hii roho ikiingia kwenye familia itawasumbua sana,inaweza kuua hata ndg watano mpaka mshtuke. Ikiingia ofisini inaweza ikawamaliza Wakurungenzi, Mameneja, Viongozi wakubwa,wafanyakazi wa kawaida mpaka wafanyakazi wengine wakaanza kuikimbia Ofisi kwa kuacha kazi ili wazinusuru roho zao.

Hii roho inawezekana ikaja kwa njia ya laana, yaani ndani ya familia,kazini au nchi kuna dhuluma iliwahi kutendeka kwa mtu aliyekuwa na haki ,akadhulumiwa aidha kiwanja,shamba,nyumba,pesa,cheo chake,au nafsi yake ikafa (mauti).

Sasa ile nafsi inarudi kulipa kisasi, au kuna aliyejua huo mchezo kisha akatamka kwamba hata kama mmemuua huyu mtu kwa kosa ambalo hakulitenda ipo siku yatawarudia.

Kwahiyo ardhi ilisikia, ikayatunza. Sasa anatokea mtu anataka cheo cha huyo muhusika, au ushindani wa kazi na biashara; sasa huyu mtu anataka amshushe chini mpinzani wake,hapa hawezi kwenda kwenye ulimwengu wa nuru maana anajua hakuna maombi ya hila,ataenda gizani.

Akifika.Wataangalia kwenye matunguri yao,nayo yataiona hiyo laana,hapo hapo ndipo watapitia.Hapo hapo ndipo palipo na njia ya kupitishia pigo. Ataanza kudondoka mmoja mmoja mpaka waishe. Labda neema ya Kristo iingie ndani yao ndipo watapata nafasi ya kutengeneza.

Ikiwa roho ya mauti inatembea ndani ya familia Ebu chunguzeni hapo ndani au kwenu kuna mlango gani usio wa haki na uko wazi,angalieni kazini kwenu,angalieni kwenye uko wenu huko nyuma kuliwahi kutokea nini?

Na huyo anayetembelewa muangalieni machoni pake anaangalia kwa namna gani,?

1.Anaona aibu isiyo ya kawaida?
2.Anakuwa ni mtu wa mawazo hana furaha tena?
3.Amejikatia tamaa anasema bora afe tu maana hana thamani?
4.Macho yake ni kama yana Ukungu haoni vizuri?
5.Amekosa nuru ,uso wake umefifia?
6.Rangi ya uso wake ni kama mtu aliyekufa, yaani mfu?
7.Hapendi ushauri, anajitenga na hataki tena maombi?

"Iwapo utagundua dalili kama hizi ujue huyo mtu ameshavishwa roho ya mauti kupitia jini maiti."

Ikiwa upo katika kundi la watu,au sehemu ukasikia watu unaowafahamu wanazungumza mambo ya vifo,yaani wao kila wakikuona ni mambo ya kufa kufa tu,shtuka kwamba wameshapatana na mauti ili wakutupie, mara nyingi hii huitafutia sababu ya wivu, ugomvi usio wa lazima,ila hasa ni 'WIVU WA MAENDELEO.'

Wanaweza kusema hivi,yaani mtaani kwetu kuna mtu kagongwa na gari ghafla akafa muda huo huo,tena alikuwa amevaa nguo za rangi hii na ile( wakati huo huo wewe umevaa hivyo hivyo).

Au kazini kwa rafiki yangu kuna mama kapigiwa simu na mumewe kwamba mtoto wao ameumwa ghafla wakati wanampeleka hospitali wakakuta amekufa tayari jamani,yaani Amelia huyo hadi huruma.Wanafiki sana wanajifanya kujisikitisha.

Au kuna mwenzetu nasikia kafukuzwa kazi kwasababu ya kuchelewa kufika kazini!

SASA UTAJUAJE NI WEWE?

Kila wakiongea maongezi ya hivi mara nyingi hujikuta wewe moyo wako unauma, na kweli saa nyingine unaweza kurudi nyumbani na kukuta vitoto vyako vyote vimejikunyata eti vinaumwa, hapa shtuka.

Kama ni kazini bosi wako anakuazishia bifu, anakuchukia ghafla,anakugombeza pasipo sababu za msingi,kwenye ndoa hivyo hivyo mnaanza kugombana kwa vitu vya kijinga. Mambo ni mengi siwezi kuyaandika yote nikayamaliza.

SASA UFANYEJE ILI ROHO YA MAUTI ISIKUFUATILIE?

Kwanza wao wamepatana na kuzimu ili wakutimie hiyo roho na kukupata.Kwa kuwa ndio hivyo,Kumbuka imeandikwa kwamba mapatano yenu na kuzimu mliyopatana na mauti hayatafanikiwa, nayakataa, mimi sitakufa bali nitaishi ili niyasimulie matendo makuu ya Mungu.

Wewe ndugu msomaji unayo nguvu ya kuzuia hiyo mauti isikufuatilie katika maisha yako.

MITHALI.18:21.

Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;nao wao waupendao watakula matunda yao

Kwahiyo unaweza kuizuia kwa kuikataa kama wao walivyopatana na kukutumia. Kwa kutumia silaha ya neno la Mungu, upanga wa Mungu na damu ya Yesu inakutoa katika maangamizi ya roho za mauti,hata ziwe nyingi kiasi gani;Bwana Yesu atakutetea na kukushindia.

ISAYA 54:17
Kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yangu katika hukumu nitauhukumu kuwa mkosa.

Hapa lazima utumie kuongea kwa kinywa chako na ulimi wako kama jinsi wao walivyofanya, au hata waliokufa walivyoacha wametamka, nawe tamka kinyume chake.

ILA UNATAMKA KATIKA ULIMWENGU UPI?

Ni ulimwengu wa Nuru ambao mtawala wake ni Yesu Kristo aliye hai peke yake.Huko kwingine ni upotofu tu.Wao huwa wanasalitiana na kuraruana.

Ikiwa utamkiri Yesu,au uliwahi kumkiri Yesu kwa kinywa chako, basi unayo haki ya kutumia neno lake kukufungua kutoka katika maagano na madhabahu ya vifo vinavyotokana na shetani.

Ndio maana huwa ninawashangaa watu wanaombea marehemu eti wasamehewe dhambi zao huwa ni kujilisha upepo tu,wafu hawana walijualo kama ni adhabu huwa tayari wameshahukumiwa katika mauti ya kwanza, wamengoja mauti ya pili siku ile ya mwisho wakamilishe hukumu zao.

Mungu hana muda wa kusikiliza maombi ya wafu, yeye ni Mungu wa walio hai siku zote.Tunatengeneza tukiwa hapa hapa duniani, na siyo baada ya kufa.

Kwahiyo kufuatwa fuatwa na watu waliokufa siyo dalili njema,kuna mambo yako mengi yanafuatiliwa na mauti ikiwemo na roho yako mtu wa Mungu. Kataa hizi roho za namna hii.

"Na unazikataa kwa kumkiri Yesu Kristo".

WARUMI 10:9-12.

Kwasababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana,na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu,utaokoka.

Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki,na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Kwa maana andiko lanena,kila amwaminiye hatatahayarika kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani;maana yeye yule ni Bwana wa wote,mwenye utajiri kwa wote wamuitao.

Kwahiyo ndugu zangu nyote Yesu anawapenda,uwe Mkristo muite atakuitikia, uwe Muislamu muite atakuitikia, uwe mpagani muite naye atakuitikieni, anachoangalia ni kukiri kwako,achana na stori za kijinga huko mtaani kwamba Yesu ni wa Wayahudi tu.Tangu mwanzo hata sasa Yeye ni wa wote.

Sisi tunaomtumikia ndio tunajua watu anaowahudumia wenye imani na jina lake,Waislamu tunawaombea wanapona, Wakristo hivyo hivyo,hata ambao hawana dini wanapona vile vile baada ya kuliamini jina lake.

Nitawapa ushuhuda kidogo.(Mtanisamehe mimi ni Mwalimu huwa ninafundisha kwa mifano halisi ).

Siku moja niliitwa na Mwalimu wa sekondari niende shuleni kwake ana maongezi na mimi.Nikaitikia wito wake.

Nilivyofika pale shuleni akanieleza alichoniitia, ila kabla sijaondoka akaniomba niwafanyie maombi wanafunzi wake maana walikuwa wamebakiwa na wiki moja ya kufanya mtihani wao.

Nikaingia darasani nikawauliza mnahitaji maombi,wote wakaitikia ndiyo. Nikawaambia kila mmoja afunge macho ili tuombe (kufumba macho na kuomba ni ile hali ya kuingia rohoni ili usione vitu vya nje ukashindwa kumakinika).

Niliomba kama dakika 5, nikasema itikieni Amina. Wakaitikia, ila baadhi hawakuinua vichwa vyao,walibaki wameinamia chini kwenye madawati. Ni wadada na hijabu zao.

Nikajiuliza wamesinzia au? Nikasogea karibu nijue kulikoni. Kumbe masikini walikuwa wanalia machozi kabisaaa.

Nikapata jibu kwamba wameguswa na furaha ya Yesu na kutuliwa mizigo yao; hawajawahi kuisikia hii hali.Watumishi wa Mungu nyinyi ni mashahidi mkiwaombea Waislamu huwa wanawahi kupokea kuliko Wakristo,na wanawake wengi wa Kiislamu huwa wanalia machozi sana katika maombezi au baada ya maombezi.

KWANINI?

"Yesu huwa anawapokea haraka na kuwaonyesha kwamba mimi NDIYE MUNGU,huwa mnadanganywa msinijue lakini MIMI NIPO AMBAYE NIKO."

YESU ANAWAPENDA NYOTE.

Mfano mwingine nilienda kwa mpemba alikuwa anaumwa mguu kwa muda mrefu sana,nikamuombea, dakika 10 nyingi akasimama akaanza kusema sisikii maumivu kama mwanzo nayasikia kwa mbali.

Nikamwambia subiri hadi kesho utaona utaamka vipi.Kesho asubuhi anaamka, anasema mtumishi yaani hata sielewi sisikii maumivu kabisa nimepona, maombi yako yamefanya kazi.

Nikamwambia Yesu huyoo, akasema ni kweli ameniponya. Hadi leo hii hawezi kusahau. Kumbe Yesu anawaponya hata wapemba Waislamu.Yesu hana ubaguzi,muite wakati wowote naye atakuponya na shida zako zote.

Mwingine anaweza kuhisi ninatanganza dini,mimi sina kanisa,huduma,wala ushirika popote,hivi ukiomba mwenyewe kimya kimya nani atajua kwamba ulikuwa unaomba?

Jaribu mwenyewe uone kama hutapata matokeo chanya kupitia hapa hapa mtandaoni. WOKOVU NI SASA,USINGOJE KESHO,KWA MAANA HUJUI SAA WALA SIKU YESU ANARUDI SAA NGAPI KULINYAKUA KANISA LAKE.

MUNGU AWABARIKI SANA.
Sasahivi nndo nazidi kukuelewa maankipindi cha mwanzo kabla sijakombolewa na damu ya Yesu nilikuwa nikiona unatoa mabandiko kuhusu ndugu zetu waislamu nilikuwa naona kama unapotoka hivi ....
lakini ndugu ....acha mungu aitwe mungu nakuunga mkono moja kwamoja ndugu zetu hawa wamkiri tu kuwa Yesu ni bwana watakomboka kwenye vifungo wengi kama hawa niliowashuhudia wamekombolewa na wanakiri mambo mazito mpaka......
 
Ahsante sana mkuu.
Hivyo vinyesi unavyoviota mara nyingi ni uchawi ambao umefanyiwa ili kukuchafulia baraka zako, kukuharibia mambo yako,kufunga baraka zako,kukuchafulia nyota yako.

Chooni mtu anaenda kujisaidia na kinachotoka kwa mtu kuingia chooni ni uchafu (kinyesi).Kwahiyo kuota kinyesi unakishika maana yake unashika uchafu.Mikono yetu imeumbiwa kushika vitu visafi ambavyo kiroho ni baraka.Ila hata tukishika uchafu huwa tunajisafisha na kuwa safi.Sasa wewe kuna wakati unashika kinyesi(baraka zako kuchafuliwa),baadaye unajisafisha na kuwa safi(kukomboa baraka zako kwa njia ya maombi).

Miguu yetu huwa inajikuta imekanyaga sehemu yenye madhabahu ya nguvu za giza,sehemu iliyotegewa tego la kichawi, au wakati mwingine kuibiwa baraka kwa njia ya mchanga wa nyayo zetu.Ndio kama hivyo wewe ambavyo huwa unaingia chooni na kukuta kuna kinyesi kila sehemu hata wakati mwingine unajikuta umesafisha lakini hali inajirudia tena.

KWAHIYO UFANYEJE?
1.Vunja roho za uchawi, ushirikina katika ardhi unayoishi unaotumwa kukukwamisha katika mipango yako.
2.Komboa nyayo zako kokote kule zilipo zilizoibwa kwa njia ya mchanga kichawi.
3.Komboa baraka zako zilizofichwa katika madhabahu zote za kichawi ambazo zilifichwa na wachawi na washirikina.
4.Futa maagano yote kwa damu ya Yesu ya kiganga na kichawi yanayotumika kama uhalalisho wa kukufungia baraka zako.
5.Komboa nyota yako kokote ilikofungiwa na mnyang'anye mamlaka yake huyo aliyeifunga na anayeitumia kwa kutumia mamlaka kuu kushinda zote ambayo ni mamlaka ya Jina la Yesu Kristo wa NAZARETHI aliye hai,na iamuru ikurudie mara moja.
6.Kwa kuwa waliitumia pasipo haki na ridhaa yako;Na kwa kuwa walikuwa wameiiba, basi nawe iamuru irudi na faida ya 7 mara 70 kama ilivyoandikwa katika kusamehe.Wewe usisamehe kwasababu waliokukosea kwa kukuibia nyota yako na kukutia kifungoni cha mkwamo wa maisha hawajakuomb msamaha.
7.Funga malango yote yaliyotumika kama sababu ya kuruhsu uchawi upate haki juu yako kwa kutumia haki ya msalaba na kiapo cha damu ya Yesu.
8.Mshukuru Mungu kwa kukurejeshea baraka zako kwa kutumia nguvu ya urejesho na malaika wa Mungu warejeshaji wa haki na baraka za watoto wa Mungu.

NB.Ndoto za namna hii huwa wanaziota watu wengi sana;Hivyo basi yeyote anaruhusiwa kuyatumia maombi haya ili ajinasue kutoka katika vifungo vya namna hii.
Mungu awabariki sana.
AMEN.
Mkuu 7seven kwa kifupi niseme tu kua mafundisho yako yameokoa wengi sana ambao huenda walikua katika njia panda wasijue nivip wasimame kiimani. Mungu atukuzwe na jina lake lihimidiwe na watu wote wamtumainiao na akubariki pia uzid kutuongoza katika kweli. Akuzidishie palipo punguka.

Swali langu pia nihili. Kabla sijasimama kiimani nlikua mpuuziaj mzur wandoto haijalishi ikoje ila toka nijitambue megundua ndoto nyingi niotazo zina maana ndani yake.

Kuna ndoto nomeziota mara kazaa nayo ni hii . Nimeota mara nyingi hua naenda uani kujisaidia labda haja kubwa. Lakini naweza kuta kuna vyoo vingi ila vyote nivichafu sana kiasi kwamba vinatia kinyaa na nikizubaa naweza shika hata kinyesi. Hii ndoto meiota mara kazaa haifanan mazingira ila lazima vyoo viwe vichafu mno. Jana pia nimeota naenda uani kujisaidia na kabla cjafika kinyesi kiliniponyoka ila ckujinyea . Na pia nilivyofika vyooni vyote vilikua vichafu chakwanza nkasafisha ili nijisaidie. Kisha nkarudi mara yapili nkakuta tena nikichafu nkakiacha nkaenda chapili nkakuta nikichafu zaid nkarud kile chakwanza nkakisafisha pia nkajisaidia je hii ndoto ya vyoo vichafu kupindukia inamaana gani?. Unakuta watu wamejisaidia ovyo bila kusafisha nikiingia nakosa wapi pakujisaidia namimi.

Sent using Jamii Forums mobile a
 
Mzazi alikutamkia Maneno ambayo ukiwa mtoto ulichukulia kawaida...! Bila elimu ya kiroho bila kujua namna ya kuzuia Uhai wa hayo maneno mabaya kama unavyofundisha hapa...!

Sasa nimekuwa nimekutana na Uzi wako nimerudi nyuma utotoni kukumbuka maneno ambayo Mzazi aliwahi kutamka....!

Naweza kuyafuta....!?
Nayafutaje...!?

Naweza kuyabadirisha yakaleta Maana..!?
Nayabadirishaje....!?
Katika ulimwengu wa Nuru hili jambo liko rahisi sana maana tumepewa damu ya Yesu kufuta kila aina ya maagano na maneno tuliyotamkiwa kwa kusikia au pasipo kusikia tumetamkiwa nini!

Kama unayakumbuka hayo maneno uliyotamkiwa ambayo kwayo ni mabaya katika mtazamo wako basi huna budi kuyafuta kama jinsi yalivyotamkwa kwa kufuta kila neno kwa damu ya Yesu na kuligeuza maana yake iwe nzuri zaidi.

"Nitakupa mfano wangu.Kuna siku nilikuwa nimekaa na ma mkubwa tunapiga stori nikiwa kidato cha pili,sasa tukaongelea mambo ya kujenga nyumba.Nikamwambia siku moja nitakujengea nyumba na wewe utakuja kuishi ndani yake."

Akacheka kwa dharau na kabehi,kwamba wewe naye unaongea maneno ya kitoto tangu lini uweze kujenga nyumba? Wewe ndiye wa kujenga nyumba wakati wameshindwa watu wa maana?

Yale maneno yaliniuma sana.Bibi akamkatisha kwa kusema,usiseme hivyo atakuja kujenga ngoja kwanza amalize shule.

Baadaye sana.Siku moja ile nyumba aliyokuwa akiishi ikaanza kuharibika ikahitaji marekebisho, nikamtumia hela akarekebisha, baadaye tena hivyo hivyo.Sasa nikasema ngoja nikafanye marekebisho makubwa nikiwepo mwenyewe. Pesa ikawa haitoshi. Halafu napata ugumu sana,tena sana.

Nikaingia kwenye maombi.Nikaambiwa kwa kukumbushwa yale maneno ya kabehi ya mama yangu mkubwa.Halafu isitoshe ile nyumba haikuwa yake kabisa,ilikuwa ni ya mama yangu mzazi,ila yeye alishatangulia mbele ya haki.

Ikabidi nielekezwe jinsi ya kuyafuta. Kwahiyo nilisema nafuta yale maneno yote kwa damu ya Yesu kwamba mimi siwezi kujenga nyumba,niliyotamkiwa na mama yangu mkubwa tukiwa sehemu fulani(nikapataja),mbele ya bibi yangu,nayafuta kwenye kinywa chake,nayafuta jwenye akili yake,ufahamu wake,moyo wake,nayafuta kwenye ardhi na kwenye vitu vyote vilivyosikia,yakatumika kama kifungo cha mimi kutokuweza kujenga hii nyumba.

Nitaijenga na itaisha na nitaishi na wote waliomo humu wataendelea kuishi ndani yake,maana neno la Mungu linasema tutajenga nyumba na kuishi ndani yake.

Na maneno yote yafutike sasa hivi,nyumba iishe kama nitakavyoijenga. Nikapewa ufunuo wa upako wa kuongezeka kila hatua na kifaa ninachotumia kujengea.

UPAKO WA KUONGEZEKA.Kwa kifupi. Kwa mfano unajenga au una wageni wako na unaona chakula hakitoshi, sasa hapa badala ya kuanza kuhangaika na kupika tena,unatumia upako wa kuongezeka na kusaza kama vile Yesu alivyolisha watu 5000 kwa samaki 2 na mikate 5.Ambapo Filipo baada ya kuulizwa swali na Yesu la mtego huku akijua alichopanga kukifanya kwamba tutapata wapi chakula cha kuwalisha watu wote hawa? Filipo akajibu kwamba tunapaswa kufanya kazi kwa mwezi mmoja angalau kila mtu apate kipande kidogo cha mkate. Lakini kwa kutumia upako wa kuongezeka Yesu aliwaombea hao samaki 2 na mikate 5 hadi watu wote wakatosheka, wakala na kusaza.

"Na hao watu 5000 ni wanaume tu weka mbali watoto na wanawake".

Kwa uchache. Ile nyumba iliisha salama kwa uweza wa Mungu.

Kwahiyo kama unakumbuka baadhi ya maneno yafute kwa kutumia kiapo cha damu ya Yesu kilichoapiwa pale msalabani kwa kuvuja kwa damu ya Yesu,futa laana zote ndani ya hayo maneno,futa majina yote mabaya uliyotamkiwa kwa damu ya Yesu.

Pia kama wao walikuwahi kukutamkia maneno mabaya nawe huyajui, sasa watangulie mbele zaidi ili ufute majina yote mabaya yenye maagano ya laana ndani yao kwa kila agano lao litakapokuwa linatakiwa kuanza kufanya kazi.

Mfano wameagana kwamba ukifika miaka 30 uanze kuumwa magonjwa ya uzee. Ukifikisha miaka 58 ufanye makosa kazini ufukuzwe kazi na usipate kiinua mgongo chako. Miaka 65 ufe kwa msongo wa mawazo.

Sasa na wewe unawawahi kwa kuyafuta yote waliyokupangia yakupate katika nyakati na wakati wa majira wa hayo maagano yaliyopangwa kuanza kufanya kazi.

Kuna wengine wanatakiwa kuanza uchawi wakifikisha miaka 18 tu.Kuna wengine wanatakiwa kuanza utumishi wa Mungu wakifikisha miaka 25 ila walishatamkiwa kinyume kwamba waanze wakiwa na miaka 78 na wafe na miaka 80,yaani watumikie miaka 2 tu tena wakiwa wazee.

"Kwahiyo laana zote,maagano yote,maneno yote ya kichawi yanafutwa kwa damu ya Yesu. Na yale uliyoyafuta unayaumba upya na kuwa mazuri kwako.Maana nguvu ya kuumba tumepewa wanadamu cha muhimu ni kujua umesimamia wapi kati haki zipi."
Amen.
 
Ahsante mkuu.

Siyo wewe tu wapo wengi,hata wao walikuwa hawaniamini na walikuwa wanaona kama ninautukana Uislamu ndio maana mwanzo nilipata nao changamoto kiroho, ila sasa hivi wamekuwa shwari,hata kiroho sina mpambano nadhani wameona ukweli na Roho Mtakatifu ameshaanza kuwagusa, wengi wameshakombolewa.

Yesu ni wa kila mtu,kila ajaye kwake hatamuacha gizani,wala hataacha kumfufua kwa kumpa uzima wa milele baada ya kumfufua siku ya mwisho.

Yeye ndiye aliyepewa mamlaka zote na Baba yake za kuwaingiza watu mbinguni,alijitoa msalabani ili watu wote waupate uzima wa milele.

Alishuka kutoka mbinguni kuja duniani ili watu wote wapate kumjua Mungu na kuupata uzima wa milele.

Na pia anayetoa mafundisho haya ana mamlaka ipi? Ni mamlaka iliyotoka mbinguni kwa uweza wa Roho na siyo mapenzi yangu au nipendavyo mimi,bali apendavyo Yesu aliyenituma kuwapasheni habari njema za ufalme wa Mungu kwa wale ambao hawakuwa wameusikia,ndio maana walio na imani wakinisadiki wataokoka.

Kwa kweli Yesu ni wa wote.Ninaamini siku moja atakuja kuhubiriwa Misikitini na Waislamu wote watajazwa na Roho Mtakatifu. Hiyo siku haiko mbali;watu watasema iliwahi kuandikwa na manabii wa Mungu enzi hizo.

Yesu anaanza kujifunua kwa ndugu zetu Waislamu ili siku anavyonyakua watu wake hata wao wasije wakaachwa maana nao wamestahili kuurithi uzima wa milele.

NITAANDIKA KWA KIREFU HAYA NILIYOANDIKA KUKOPI KATIKA BIBLIA ILI IWE RAHISI KWA MSOMAJI.

Imeandikwa katika MATHAYO MTAKATIFU NA LUKA MTAKATIFU.

37.Vyote anavyonipa Baba vitakuja kwangu,hata hivyo yeyote yule atakayekuja kwangu sitamkataa kabisa.Nami kwa hakika daima nitawapokea.

38.Nilishuka kutoka mbinguni kuja kufanya yale Mungu anayopenda, siyo ninayoyapenda mimi.

39.Nami sitampoteza hata mmoja wa wale alionipa Mungu.Bali ninataka nimfufue katika ile siku ya mwisho.Haya Ndiyo Baba yangu anayotaka.

40.Kila anayemtazama mwana na kumwamini anao uzima wa Milele (sasa hivi tumepewa sisi watumishi hiyo mamlaka ya kuwahaubiria watu ufalme wa mbinguni na wao kupewa uzima wa milele na Yesu Kristo.)

"Nami nitamfufua katika ile siku ya mwisho. Hayo ndio anayoyataka Baba yangu."

41.Baadhi ya Wayahudi walianza kumlalamikia Yesu kwa vile alisema."Mimi ni mkate unaoshuka kutoka mbinguni."

42.Wakasema,"Huyu ni Yesu.Tunawajua baba na mama yake.Yeye ni mtoto wa Yusufu.Anawezaje kusema,'Nilishuka kutoka mbinguni?"

43.Lakini Yesu akawaambia," Acheni kunung'unika miongoni mwenu.

44.Baba ndiye aliyenituma na ndiye anayewaleta watu kwangu.Nami nitawafufua siku ya mwisho. Hakuna mtu anayeweza kuja kwangu asipoletwa na Baba yangu.

45.Hii iliandikwa katika vitabu vya manabii; Mungu atawafundisha wote.Watu humsikiliza Baba na hujifunza kutoka kwake.Hao ndio wanaokuja kwangu.

46.Sina maana kwamba yupo yeyote aliyemuona Baba.Yule pekee aliyekwisha kumwona Baba ni yule aliyetoka kwa Mungu.Huyo amemuona Baba.(Yesu alijisemea Hapa).

47.Hakika nawaambieni kila anayeamini anao uzima wa milele.

48.Maana mimi ni mkate unaoleta uzima wa milele.

49.Baba zenu walikula mana waliyopewa na Mungu kule jangwani, lakini haikuwazuia kufa.

50.Hapa upo mkate unaotoka mbinguni, yeyote anayekula mkate huu hatakufa kamwe..

51."Mimi ni mkate ulio hai ulioshuka kutoka mbinguni. Yeyote atakayekula mkate huu ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu.Nitautoa mwili wangu ili watu wa ulimwengu huu waweze kuupata uzima."

52.Kisha Wayahudi hawa wakaanza kubishana wao kwa wao.Wakasema ."Yawezekanaje mtu huyu akatupa mwili wake tuule?"

53.Yesu akasema.Mniamini ninaposema kwamba mnapaswa kuula mwili wa Mwana wa Adamu; na mnapaswa kuinywa damu yake. Msipofanya hivyo,hamtakuwa na uzima wa milele.

54.Wale wanaokula mwili wangu na kuinywa damu yangu wanao uzima wa milele. Nitawafufua siku ya mwisho..

55.Mwili wangu ni chakula halisi na kuinywa damu yangu ni kinywaji halisi.

56.Wale waulao mwili wangu na kuinywa damu yangu wanaishi ndani yangu,nami naishi ndani yao.

57.Baba alinituma. Yeye anaishi, nami naishi kwasababu yake.Hivyo kila anayenila mimi ataishi kwasababu yangu.

58.Mimi siyo kama ule mkate waliokula baba zenu.Wao waliula mkate huo,lakini bado walikufa baadaye.Mimi ni mkate uliotoka mbinguni. Yeyote atakayeula mkate huu ataishi milele.

59.Yesu aliyasema haya yote alipokuwa akifundisha kwenye Sinagogi katika mji wa Karpenaumu.

60.Wafuasi wa Yesu waliposikia haya,wengi wao wakasema, fundisho hili ni gumu sana.Nani awezaye kulipokea?

61.Yesu alikwisha tambua kuwa wafuasi wake walikuwa wanalalamika juu ya hili.Hivyo akasema,"Je, fundisho hili ni tatizo kwenu?

62.Ikiwa ni hivyo mtafikiri nini mtakapomwona Mwana wa Adamu akipanda kurudi kule alikotoka?

63."Roho ndiye anayeleta uzima,siyo mwili.Lakini maneno niliyowaambia yanatoka kwa Roho ,hivyo yanaleta uzima."

64.Lakini baadhi yenu hamuamini. (Yesu aliwafahamu wale ambao hawakuamini. Alijua haya tangu mwanzo.Na alimjua yule ambaye angemsaliti kwa adui zake).

65.Yesu akasema,"Ndiyo maana nilisema, 'Hayupo hata mmoja ambaye anaweza kuja kwangu pasipo kusaidiwa na Baba.'

66.BAADA ya Yesu kusema mambo hayo,wafuasi wake wengi wakamkimbia na wakaacha kumfuata.

67.Yesu akawauliza wale mitume kumi na wawili,Nanyi pia mnataka kuondoka?

68.Simoni Petro akamjibu, Bwana,tutaenda wapi?Wewe unayo maneno yanayoleta uzima wa milele.

69.Sisi tunakuamini wewe. Tunafahamu kwamba wewe ndiye yule Mtakatifu atokaye kwa Mungu.

70.Kisha Yesu akajibu, Niliwachagua nyote kumi na wawili. Lakini mmoja wenu ni Ibilisi.

71.Alikuwa anazungumza juu ya Yuda mwana wa Simoni Iskariote. Yuda ailikuwa miongoni mwa mitume 12 lakini baadaye angemkabidhi Yesu kwa adui zake.
***********************************
Nimeandika kwa urefu ili ndg msomaji apate kusoma kwa urefu zaidi,ajue jinsi ambavyo Yesu ni njia ya kweli na Uzima.Ajue ahadi za Yesu kwa kila aaminiye jina lake,hana dini,dhehebu,kabila wala utaifa. Injili ni kwa watu wote,tena ni habari njema kwa ulimwengu wote ili upate uzima wa milele.

Pia kuna watu hawapendi kusoma maandiko,hivyo anavyopita hapa anapata kusoma maandiko mengi zaidi na katika hayo maandiko anapata neno linalompa uhai katika kiroho chake.Macho yenu yafumbuliwe sasa ili mpate kuona sawa sawa nyakati hizi za mwisho, mwishowe msije mkaachwa wakati wa UNYAKUO WA KANISA.

Mungu awabariki sana.
 
KUINUKA KWA ROHO YA MAUTI.
Hii inasababishwa na mambo mengi sana ambayo kwa kujibu swali lako ni ngumu kuyaorodhesha yote hapa.

Ila sababu kubwa zaidi ambazo hupelekea yote haya ni MADHABAHU,MAAGANO,MAMLAKA na UTAWALA wa huyo mtu aliyekusudiwa hiyo roho ya mauti.

Ndoto zote zinazohusiana na watu waliokufa siyo nzuri,wawe ni wazazi,ndg,jamaa na marafiki,au hata watu wasiojulikana.Hizi siyo ndoto nzuri hata kidogo.

Kwasababu roho ya huyo mtu inakuwa na mahusiano na roho za hao waliokufa ambao wao wako katika ulimwengu mwingine; huku aliye hai yuko katika ulimwengu wa mwili.Haitakiwi kuwepo mawasiliano ya watu waliokufa na walio hai,kwa kuwa waliokufa hawajui chochote kinachoendelea hapa duniani.

MTU ATAULIZA KWANINI SASA IWE HIVYO.

Tazama hapa.MUHUBIRI 9:5

"Kwasababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa;lakini wafu hawajui neno lolote,wala hawana ijara tena;maana kumbukumbu lao limesahauliwa."

SASA HUWA NI AKINA NANI TUNAWAOTA KWA SURA TUNAZOZIJUA?

"Mtu anaweza kumuona mzazi wake, mume/mke wake,mtoto wake,rafiki yake n.k,akizungumza naye mambo ya kawaida au hata mambo ya siri na yote hayo yasemwayo ni hakika ,yaani kweli kabisa." Hii isimpe uhalali kwamba yuko katika njia za haki.

Ndio maana unaweza kukuta mtu anasema yeye akiota ndoto huwa ni za kweli,akimuotea mtu hutokea hivyo hivyo kama alivyoota, na wakati huo huo ni mtenda dhambi kama zote.

Hapa kinachofanyika ni mapepo ambayo huvaa sura za hao wahusika na kuja kwa huyo mtu,mara nyingi sehemu za namna hii ni zile zenye chimbuko la kuabudu mizimu,familia za kichawi,kishirikiana,za waganga wa kienyeji, kutambikia mizimu na makafara ya kila aina.

KIUFUPI,ni familia zenye madhabahu ya miungu zilizo hai,mapepo na mizimu ipo mahali hapo,inawaongoza na kuwapa maelekezo ya jinsi ya kuendelea kuitunza hiyo madhabahu ili iendelee kupata huduma, hasa katika KUABUDIWA.

Madhabahu zina mambo mengi,sasa ikiwa katika familia kuna mtu anatembelewa na hiyo roho ya mauti kwa kuota watu waliokufa, kuota sana makaburini,anaota anazikwa, jeneza,sanda, au amekufa. Hapo kuna uwezekano ametumiwa hiyo roho ili imvae na iharibu afya yake,mambo yake na hata uhai wake.Haiji hivi hivi mpaka awepo mtu mwingine wa kuituma.

Ikishatumwa itaamua imuondoe kwa ajali,kuumwa sana,au muda mfupi,kifo cha ghafla, kujiua, kuua na kisha kujiua.

Na hii roho ikiingia kwenye familia itawasumbua sana,inaweza kuua hata ndg watano mpaka mshtuke. Ikiingia ofisini inaweza ikawamaliza Wakurungenzi, Mameneja, Viongozi wakubwa,wafanyakazi wa kawaida mpaka wafanyakazi wengine wakaanza kuikimbia Ofisi kwa kuacha kazi ili wazinusuru roho zao.

Hii roho inawezekana ikaja kwa njia ya laana, yaani ndani ya familia,kazini au nchi kuna dhuluma iliwahi kutendeka kwa mtu aliyekuwa na haki ,akadhulumiwa aidha kiwanja,shamba,nyumba,pesa,cheo chake,au nafsi yake ikafa (mauti).

Sasa ile nafsi inarudi kulipa kisasi, au kuna aliyejua huo mchezo kisha akatamka kwamba hata kama mmemuua huyu mtu kwa kosa ambalo hakulitenda ipo siku yatawarudia.

Kwahiyo ardhi ilisikia, ikayatunza. Sasa anatokea mtu anataka cheo cha huyo muhusika, au ushindani wa kazi na biashara; sasa huyu mtu anataka amshushe chini mpinzani wake,hapa hawezi kwenda kwenye ulimwengu wa nuru maana anajua hakuna maombi ya hila,ataenda gizani.

Akifika.Wataangalia kwenye matunguri yao,nayo yataiona hiyo laana,hapo hapo ndipo watapitia.Hapo hapo ndipo palipo na njia ya kupitishia pigo. Ataanza kudondoka mmoja mmoja mpaka waishe. Labda neema ya Kristo iingie ndani yao ndipo watapata nafasi ya kutengeneza.

Ikiwa roho ya mauti inatembea ndani ya familia Ebu chunguzeni hapo ndani au kwenu kuna mlango gani usio wa haki na uko wazi,angalieni kazini kwenu,angalieni kwenye uko wenu huko nyuma kuliwahi kutokea nini?

Na huyo anayetembelewa muangalieni machoni pake anaangalia kwa namna gani,?

1.Anaona aibu isiyo ya kawaida?
2.Anakuwa ni mtu wa mawazo hana furaha tena?
3.Amejikatia tamaa anasema bora afe tu maana hana thamani?
4.Macho yake ni kama yana Ukungu haoni vizuri?
5.Amekosa nuru ,uso wake umefifia?
6.Rangi ya uso wake ni kama mtu aliyekufa, yaani mfu?
7.Hapendi ushauri, anajitenga na hataki tena maombi?

"Iwapo utagundua dalili kama hizi ujue huyo mtu ameshavishwa roho ya mauti kupitia jini maiti."

Ikiwa upo katika kundi la watu,au sehemu ukasikia watu unaowafahamu wanazungumza mambo ya vifo,yaani wao kila wakikuona ni mambo ya kufa kufa tu,shtuka kwamba wameshapatana na mauti ili wakutupie, mara nyingi hii huitafutia sababu ya wivu, ugomvi usio wa lazima,ila hasa ni 'WIVU WA MAENDELEO.'

Wanaweza kusema hivi,yaani mtaani kwetu kuna mtu kagongwa na gari ghafla akafa muda huo huo,tena alikuwa amevaa nguo za rangi hii na ile( wakati huo huo wewe umevaa hivyo hivyo).

Au kazini kwa rafiki yangu kuna mama kapigiwa simu na mumewe kwamba mtoto wao ameumwa ghafla wakati wanampeleka hospitali wakakuta amekufa tayari jamani,yaani Amelia huyo hadi huruma.Wanafiki sana wanajifanya kujisikitisha.

Au kuna mwenzetu nasikia kafukuzwa kazi kwasababu ya kuchelewa kufika kazini!

SASA UTAJUAJE NI WEWE?

Kila wakiongea maongezi ya hivi mara nyingi hujikuta wewe moyo wako unauma, na kweli saa nyingine unaweza kurudi nyumbani na kukuta vitoto vyako vyote vimejikunyata eti vinaumwa, hapa shtuka.

Kama ni kazini bosi wako anakuazishia bifu, anakuchukia ghafla,anakugombeza pasipo sababu za msingi,kwenye ndoa hivyo hivyo mnaanza kugombana kwa vitu vya kijinga. Mambo ni mengi siwezi kuyaandika yote nikayamaliza.

SASA UFANYEJE ILI ROHO YA MAUTI ISIKUFUATILIE?

Kwanza wao wamepatana na kuzimu ili wakutimie hiyo roho na kukupata.Kwa kuwa ndio hivyo,Kumbuka imeandikwa kwamba mapatano yenu na kuzimu mliyopatana na mauti hayatafanikiwa, nayakataa, mimi sitakufa bali nitaishi ili niyasimulie matendo makuu ya Mungu.

Wewe ndugu msomaji unayo nguvu ya kuzuia hiyo mauti isikufuatilie katika maisha yako.

MITHALI.18:21.

Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;nao wao waupendao watakula matunda yao

Kwahiyo unaweza kuizuia kwa kuikataa kama wao walivyopatana na kukutumia. Kwa kutumia silaha ya neno la Mungu, upanga wa Mungu na damu ya Yesu inakutoa katika maangamizi ya roho za mauti,hata ziwe nyingi kiasi gani;Bwana Yesu atakutetea na kukushindia.

ISAYA 54:17
Kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yangu katika hukumu nitauhukumu kuwa mkosa.

Hapa lazima utumie kuongea kwa kinywa chako na ulimi wako kama jinsi wao walivyofanya, au hata waliokufa walivyoacha wametamka, nawe tamka kinyume chake.

ILA UNATAMKA KATIKA ULIMWENGU UPI?

Ni ulimwengu wa Nuru ambao mtawala wake ni Yesu Kristo aliye hai peke yake.Huko kwingine ni upotofu tu.Wao huwa wanasalitiana na kuraruana.

Ikiwa utamkiri Yesu,au uliwahi kumkiri Yesu kwa kinywa chako, basi unayo haki ya kutumia neno lake kukufungua kutoka katika maagano na madhabahu ya vifo vinavyotokana na shetani.

Ndio maana huwa ninawashangaa watu wanaombea marehemu eti wasamehewe dhambi zao huwa ni kujilisha upepo tu,wafu hawana walijualo kama ni adhabu huwa tayari wameshahukumiwa katika mauti ya kwanza, wamengoja mauti ya pili siku ile ya mwisho wakamilishe hukumu zao.

Mungu hana muda wa kusikiliza maombi ya wafu, yeye ni Mungu wa walio hai siku zote.Tunatengeneza tukiwa hapa hapa duniani, na siyo baada ya kufa.

Kwahiyo kufuatwa fuatwa na watu waliokufa siyo dalili njema,kuna mambo yako mengi yanafuatiliwa na mauti ikiwemo na roho yako mtu wa Mungu. Kataa hizi roho za namna hii.

"Na unazikataa kwa kumkiri Yesu Kristo".

WARUMI 10:9-12.

Kwasababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana,na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu,utaokoka.

Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki,na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Kwa maana andiko lanena,kila amwaminiye hatatahayarika kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani;maana yeye yule ni Bwana wa wote,mwenye utajiri kwa wote wamuitao.

Kwahiyo ndugu zangu nyote Yesu anawapenda,uwe Mkristo muite atakuitikia, uwe Muislamu muite atakuitikia, uwe mpagani muite naye atakuitikieni, anachoangalia ni kukiri kwako,achana na stori za kijinga huko mtaani kwamba Yesu ni wa Wayahudi tu.Tangu mwanzo hata sasa Yeye ni wa wote.

Sisi tunaomtumikia ndio tunajua watu anaowahudumia wenye imani na jina lake,Waislamu tunawaombea wanapona, Wakristo hivyo hivyo,hata ambao hawana dini wanapona vile vile baada ya kuliamini jina lake.

Nitawapa ushuhuda kidogo.(Mtanisamehe mimi ni Mwalimu huwa ninafundisha kwa mifano halisi ).

Siku moja niliitwa na Mwalimu wa sekondari niende shuleni kwake ana maongezi na mimi.Nikaitikia wito wake.

Nilivyofika pale shuleni akanieleza alichoniitia, ila kabla sijaondoka akaniomba niwafanyie maombi wanafunzi wake maana walikuwa wamebakiwa na wiki moja ya kufanya mtihani wao.

Nikaingia darasani nikawauliza mnahitaji maombi,wote wakaitikia ndiyo. Nikawaambia kila mmoja afunge macho ili tuombe (kufumba macho na kuomba ni ile hali ya kuingia rohoni ili usione vitu vya nje ukashindwa kumakinika).

Niliomba kama dakika 5, nikasema itikieni Amina. Wakaitikia, ila baadhi hawakuinua vichwa vyao,walibaki wameinamia chini kwenye madawati. Ni wadada na hijabu zao.

Nikajiuliza wamesinzia au? Nikasogea karibu nijue kulikoni. Kumbe masikini walikuwa wanalia machozi kabisaaa.

Nikapata jibu kwamba wameguswa na furaha ya Yesu na kutuliwa mizigo yao; hawajawahi kuisikia hii hali.Watumishi wa Mungu nyinyi ni mashahidi mkiwaombea Waislamu huwa wanawahi kupokea kuliko Wakristo,na wanawake wengi wa Kiislamu huwa wanalia machozi sana katika maombezi au baada ya maombezi.

KWANINI?

"Yesu huwa anawapokea haraka na kuwaonyesha kwamba mimi NDIYE MUNGU,huwa mnadanganywa msinijue lakini MIMI NIPO AMBAYE NIKO."

YESU ANAWAPENDA NYOTE.

Mfano mwingine nilienda kwa mpemba alikuwa anaumwa mguu kwa muda mrefu sana,nikamuombea, dakika 10 nyingi akasimama akaanza kusema sisikii maumivu kama mwanzo nayasikia kwa mbali.

Nikamwambia subiri hadi kesho utaona utaamka vipi.Kesho asubuhi anaamka, anasema mtumishi yaani hata sielewi sisikii maumivu kabisa nimepona, maombi yako yamefanya kazi.

Nikamwambia Yesu huyoo, akasema ni kweli ameniponya. Hadi leo hii hawezi kusahau. Kumbe Yesu anawaponya hata wapemba Waislamu.Yesu hana ubaguzi,muite wakati wowote naye atakuponya na shida zako zote.

Mwingine anaweza kuhisi ninatanganza dini,mimi sina kanisa,huduma,wala ushirika popote,hivi ukiomba mwenyewe kimya kimya nani atajua kwamba ulikuwa unaomba?

Jaribu mwenyewe uone kama hutapata matokeo chanya kupitia hapa hapa mtandaoni. WOKOVU NI SASA,USINGOJE KESHO,KWA MAANA HUJUI SAA WALA SIKU YESU ANARUDI SAA NGAPI KULINYAKUA KANISA LAKE.

MUNGU AWABARIKI SANA.
Kusimama kwangu kulianzia katika jumbe zako nikajifunza mengi sana hata juyachukulia hatua ila sasa mejitambua nina vita yakiuchumi na sasa ndo nazid kufunguka nakugundua viko vifungo vingi vinanisumbua. Now niko katika mapambano naamin Mungu atazid kunifungua. Nazid kukaza mwendo japo huibuka mambo yasoeleweka ila katu sitarud nyuma had Mungu anishindie katika vita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante sana mkuu.
Hivyo vinyesi unavyoviota mara nyingi ni uchawi ambao umefanyiwa ili kukuchafulia baraka zako, kukuharibia mambo yako,kufunga baraka zako,kukuchafulia nyota yako.

Chooni mtu anaenda kujisaidia na kinachotoka kwa mtu kuingia chooni ni uchafu (kinyesi).Kwahiyo kuota kinyesi unakishika maana yake unashika uchafu.Mikono yetu imeumbiwa kushika vitu visafi ambavyo kiroho ni baraka.Ila hata tukishika uchafu huwa tunajisafisha na kuwa safi.Sasa wewe kuna wakati unashika kinyesi(baraka zako kuchafuliwa),baadaye unajisafisha na kuwa safi(kukomboa baraka zako kwa njia ya maombi).

Miguu yetu huwa inajikuta imekanyaga sehemu yenye madhabahu ya nguvu za giza,sehemu iliyotegewa tego la kichawi, au wakati mwingine kuibiwa baraka kwa njia ya mchanga wa nyayo zetu.Ndio kama hivyo wewe ambavyo huwa unaingia chooni na kukuta kuna kinyesi kila sehemu hata wakati mwingine unajikuta umesafisha lakini hali inajirudia tena.

KWAHIYO UFANYEJE?
1.Vunja roho za uchawi, ushirikina katika ardhi unayoishi unaotumwa kukukwamisha katika mipango yako.
2.Komboa nyayo zako kokote kule zilipo zilizoibwa kwa njia ya mchanga kichawi.
3.Komboa baraka zako zilizofichwa katika madhabahu zote za kichawi ambazo zilifichwa na wachawi na washirikina.
4.Futa maagano yote kwa damu ya Yesu ya kiganga na kichawi yanayotumika kama uhalalisho wa kukufungia baraka zako.
5.Komboa nyota yako kokote ilikofungiwa na mnyang'anye mamlaka yake huyo aliyeifunga na anayeitumia kwa kutumia mamlaka kuu kushinda zote ambayo ni mamlaka ya Jina la Yesu Kristo wa NAZARETHI aliye hai,na iamuru ikurudie mara moja.
6.Kwa kuwa waliitumia pasipo haki na ridhaa yako;Na kwa kuwa walikuwa wameiiba, basi nawe iamuru irudi na faida ya 7 mara 70 kama ilivyoandikwa katika kusamehe.Wewe usisamehe kwasababu waliokukosea kwa kukuibia nyota yako na kukutia kifungoni cha mkwamo wa maisha hawajakuomb msamaha.
7.Funga malango yote yaliyotumika kama sababu ya kuruhsu uchawi upate haki juu yako kwa kutumia haki ya msalaba na kiapo cha damu ya Yesu.
8.Mshukuru Mungu kwa kukurejeshea baraka zako kwa kutumia nguvu ya urejesho na malaika wa Mungu warejeshaji wa haki na baraka za watoto wa Mungu.

NB.Ndoto za namna hii huwa wanaziota watu wengi sana;Hivyo basi yeyote anaruhusiwa kuyatumia maombi haya ili ajinasue kutoka katika vifungo vya namna hii.
Mungu awabariki sana.
AMEN.
Dah! Nikivuta picha ninayo safari ndefu yamapambano ziko nguvu bado hazitaman nijikomboe ila kwa mamlaka yake Mungu hakika nitashinda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusimama kwangu kulianzia katika jumbe zako nikajifunza mengi sana hata juyachukulia hatua ila sasa mejitambua nina vita yakiuchumi na sasa ndo nazid kufunguka nakugundua viko vifungo vingi vinanisumbua. Now niko katika mapambano naamin Mungu atazid kunifungua. Nazid kukaza mwendo japo huibuka mambo yasoeleweka ila katu sitarud nyuma had Mungu anishindie katika vita

Sent using Jamii Forums mobile app
Amen.Uzidi kubarikiwa na kupata mafundisho yatakayokutoa mahali hapo ulipo kwasababu umeshapiga hatua moja kubwa na ya muhimu katika vita yako ya kiroho.

Kitu ambacho shetani huwa hapendi watoto wa Mungu wakijue ni kuujua ukweli,kujua matatizo waliyonayo siyo mpango wa Mungu.

Shetani hapendi na hataki mtu wa Mungu ajijue yeye ni nani,Mungu amemkusudia nini, baraka zake zipo wapi,mke/mume wake kutoka kwa Mungu ni nani. HATAKI NA HAPENDI MTU AUJUE UKWELI WAKE.

Kwahiyo pale unapoanza kuonyesha dalili za kuijua kweli huanzisha vita vya kiroho na kisha huvileta mwilini ili akutishe na kukukatisha tamaa.Ukiwa mbishi hadi mwisho anaachana na wewe maana anajua mtu huyu imani yake ni kali,na mtu mwenye imani huishi katika haki za Mungu na hawezi kudanganyika kirahisi na uongo wa shetani.

Watu wengi wamefichwa njia za mafanikio yao ndio maana siyo rahisi kuelewa wanatakiwa wafanye nini,waishi wapi, wale nini,wavae nini,watembelee wapi,waoe na kuolewa wapi.Anawakengeusha ili apate sehemu ya kuwashikilia na baraka zao awape wengine.

Una nyota kali ndio maana unaona ndoto za vinyesi. UCHAWI NI UCHAFU UNAOFANANISHWA NA KINYESI.Wachawi ni watu wachafu kiroho ndio maana ndotoni huonekana wakiwa katika mazingira machafu,wanakula sehemu chafu, wanakula uchafu.

Hivi unaweza kuamini mchawi anapewa masharti ya kuramba ,ped' ya mwanamke aliyetoka kwenye hedhi na wanaramba? Sasa huu ni uchafu wa namna gani jamani!?

Kwahiyo fanyia kazi hayo maeneo maana tayari Mungu ameshakuonyesha mahali pa kuanzia,kadri unavyozidi kusonga mbele na kuwa karibu na Mungu ndivyo utakavyozidi kuona mambo mengi zaidi.

Utafikia wakati hadi unaanza kuwajua wote waliokufanyia huo mchezo, wengine nduguzo, marafiki,na jamaa.Cha msingi usiwafuate kuwauliza kwanini mlinifanyia hivyo? Mambo yetu huwa tunayamalizia rohoni na matokeo yake huonekana mwilini lakini hushitakiwi kwa kuwahukumu waliokukosea kwasbabu siyo wewe uliyetoa hukumu bali ni Yesu kupitia maombi yako.

Kiwango chako cha kumtafuta Mungu kupitia maombi yako,ndicho kipimo cha kujibiwa mahitaji yako na Mungu.

OMBA MPAKA MBINGU ZIFUNGUKE.
 
Katika ulimwengu wa Nuru hili jambo liko rahisi sana maana tumepewa damu ya Yesu kufuta kila aina ya maagano na maneno tuliyotamkiwa kwa kusikia au pasipo kusikia tumetamkiwa nini!

Kama unayakumbuka hayo maneno uliyotamkiwa ambayo kwayo ni mabaya katika mtazamo wako basi huna budi kuyafuta kama jinsi yalivyotamkwa kwa kufuta kila neno kwa damu ya Yesu na kuligeuza maana yake iwe nzuri zaidi.

"Nitakupa mfano wangu.Kuna siku nilikuwa nimekaa na ma mkubwa tunapiga stori nikiwa kidato cha pili,sasa tukaongelea mambo ya kujenga nyumba.Nikamwambia siku moja nitakujengea nyumba na wewe utakuja kuishi ndani yake."

Akacheka kwa dharau na kabehi,kwamba wewe naye unaongea maneno ya kitoto tangu lini uweze kujenga nyumba? Wewe ndiye wa kujenga nyumba wakati wameshindwa watu wa maana?

Yale maneno yaliniuma sana.Bibi akamkatisha kwa kusema,usiseme hivyo atakuja kujenga ngoja kwanza amalize shule.

Baadaye sana.Siku moja ile nyumba aliyokuwa akiishi ikaanza kuharibika ikahitaji marekebisho, nikamtumia hela akarekebisha, baadaye tena hivyo hivyo.Sasa nikasema ngoja nikafanye marekebisho makubwa nikiwepo mwenyewe. Pesa ikawa haitoshi. Halafu napata ugumu sana,tena sana.

Nikaingia kwenye maombi.Nikaambiwa kwa kukumbushwa yale maneno ya kabehi ya mama yangu mkubwa.Halafu isitoshe ile nyumba haikuwa yake kabisa,ilikuwa ni ya mama yangu mzazi,ila yeye alishatangulia mbele ya haki.

Ikabidi nielekezwe jinsi ya kuyafuta. Kwahiyo nilisema nafuta yale maneno yote kwa damu ya Yesu kwamba mimi siwezi kujenga nyumba,niliyotamkiwa na mama yangu mkubwa tukiwa sehemu fulani(nikapataja),mbele ya bibi yangu,nayafuta kwenye kinywa chake,nayafuta jwenye akili yake,ufahamu wake,moyo wake,nayafuta kwenye ardhi na kwenye vitu vyote vilivyosikia,yakatumika kama kifungo cha mimi kutokuweza kujenga hii nyumba.

Nitaijenga na itaisha na nitaishi na wote waliomo humu wataendelea kuishi ndani yake,maana neno la Mungu linasema tutajenga nyumba na kuishi ndani yake.

Na maneno yote yafutike sasa hivi,nyumba iishe kama nitakavyoijenga. Nikapewa ufunuo wa upako wa kuongezeka kila hatua na kifaa ninachotumia kujengea.

UPAKO WA KUONGEZEKA.Kwa kifupi. Kwa mfano unajenga au una wageni wako na unaona chakula hakitoshi, sasa hapa badala ya kuanza kuhangaika na kupika tena,unatumia upako wa kuongezeka na kusaza kama vile Yesu alivyolisha watu 5000 kwa samaki 2 na mikate 5.Ambapo Filipo baada ya kuulizwa swali na Yesu la mtego huku akijua alichopanga kukifanya kwamba tutapata wapi chakula cha kuwalisha watu wote hawa? Filipo akajibu kwamba tunapaswa kufanya kazi kwa mwezi mmoja angalau kila mtu apate kipande kidogo cha mkate. Lakini kwa kutumia upako wa kuongezeka Yesu aliwaombea hao samaki 2 na mikate 5 hadi watu wote wakatosheka, wakala na kusaza.

"Na hao watu 5000 ni wanaume tu weka mbali watoto na wanawake".

Kwa uchache. Ile nyumba iliisha salama kwa uweza wa Mungu.

Kwahiyo kama unakumbuka baadhi ya maneno yafute kwa kutumia kiapo cha damu ya Yesu kilichoapiwa pale msalabani kwa kuvuja kwa damu ya Yesu,futa laana zote ndani ya hayo maneno,futa majina yote mabaya uliyotamkiwa kwa damu ya Yesu.

Pia kama wao walikuwahi kukutamkia maneno mabaya nawe huyajui, sasa watangulie mbele zaidi ili ufute majina yote mabaya yenye maagano ya laana ndani yao kwa kila agano lao litakapokuwa linatakiwa kuanza kufanya kazi.

Mfano wameagana kwamba ukifika miaka 30 uanze kuumwa magonjwa ya uzee. Ukifikisha miaka 58 ufanye makosa kazini ufukuzwe kazi na usipate kiinua mgongo chako. Miaka 65 ufe kwa msongo wa mawazo.

Sasa na wewe unawawahi kwa kuyafuta yote waliyokupangia yakupate katika nyakati na wakati wa majira wa hayo maagano yaliyopangwa kuanza kufanya kazi.

Kuna wengine wanatakiwa kuanza uchawi wakifikisha miaka 18 tu.Kuna wengine wanatakiwa kuanza utumishi wa Mungu wakifikisha miaka 25 ila walishatamkiwa kinyume kwamba waanze wakiwa na miaka 78 na wafe na miaka 80,yaani watumikie miaka 2 tu tena wakiwa wazee.

"Kwahiyo laana zote,maagano yote,maneno yote ya kichawi yanafutwa kwa damu ya Yesu. Na yale uliyoyafuta unayaumba upya na kuwa mazuri kwako.Maana nguvu ya kuumba tumepewa wanadamu cha muhimu ni kujua umesimamia wapi kati haki zipi."
Amen.
Mkuu Shalom, maelezo yako, yatakua Msaada Mkubwa kwangu... Hujajua tu asante.
 
Amen.Ubarikiwe sana na Mungu azidi kukufungua kwa kila hatua unayopiga usonge mbele,uvishinde vikwazo vyote ulivyowekewa na shetani katika ile imani kuu ya Yesu Kristo aliye hai.
Mkuu Shalom, maelezo yako, yatakua Msaada Mkubwa kwangu... Hujajua tu asante.
 
U

Ushauri mzuri sana.Hili suala la kuchanganya miungu Lipo kwa watu wengi hasa jamii zetu za Afrika hususani Tanzania.Kumchanganya Mungu na miungu ni sawa na maji na mafuta ambavyo huwa havichangamani.

Mungu anachukizwa na hali ya namna hii,ukishaanza kwenda huko kwa waganga na wachawi,basi naye huwa ananyamaza na kukaa kimya,anajitenga na mtu yeyote aendaye katika njia za namna hii.

Tena watu wengi huwa wanatumia msemo usemao 'jisaidie nami nikusaidie',kwamba hapo alimaanisha njia nyingine hasa za giza. Huu ni uongo,upotoshaji na udanganyifu wenye makufuru ya kumuasi Mungu.

Haimaanishi hivyo.Kama upo kweli huo mstari kwenye Biblia basi unamaanisha kuchukua hatua ya kumtafuta Mungu kwa bidii naye atakuonekania. Na kila amtafutaye atamuona. Kila ajaye kwake hatamtupa kamwe.

Ndio maana imeandikwa ni heri uwe moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu maana BWANA atakutapika. Mungu hachanganywi.

Ni bora uwe na Mungu kabisa,umche Yeye na kumuabudu Yeye katika roho na kweli, umtegemee Yeye kwa nguvu zako zote ili awe nawe siku zote na akufundishe njia zake.(Huku ndiko kuwa moto).

Kuwa baridi ni kutokumjua Yeye ili basi aje ndani yako na kukusaidia kumjua. (Kuishi katika dhambi).

Lakini kuwa vuguvugu ni ile hali ya kwamba leo uko kwa Mungu na kesho upo kwa shetani kupitia kwa waganga wa kienyeji, wachawi,washirika na matendo yote mabaya ya mwilini.

Kwahiyo ni vizuri kwenda kwa Mungu kwa moyo wako wote,kumtumainia kwa akili zako zote,na kwa nguvu zako zote,naye atakuonekania.

Angalia watu wengi waliochanganya miungu mwisho wake ulikuwaje, waliishia pabaya au kumaliza vibaya.

Mfano. Ni mfalme Suleimani. Yeye pamoja na fahari yake yote lakini Yesu anasema hakuvishwa kama miongoni wa hao wadogo.Maana yake hakupewa taji la uzima.

Alipewa hekima kuliko mtu yeyote aliyewahi kuwepo hapa duniani,alipewa utajiri hapana mtu amewahi kuupata hapa duniani.Alikuwa na karama za kutafsiri lugha mbalimbi hadi za ndege,ila mwishowe alianza kusema kwamba hekima yote aliyonayo haikutoka kwa Mungu bali ni miungu yake ambayo hapo awali hakuwa anaijua isipokuwa alifundishwa na miongoni wa wakeze kuiabudu.

Ikambadilisha moyo Suleimani,akamuacha Mungu wa baba zake; Mungu wa Daudi,Yese, Yakobo,Isaka na Ibrahimu,akaitumikia miungu ya wake zake,akaiabudu, akaipa sadaka,akaifukizia uvumba na mambo mengine mengi kama watu wengine wafanyavyo ambao huabudu miungu.

Hii ilimkasirisha sana Mungu."Alimuona kama muasi,alimuacha mpaka anakufa hakuwa ametubu."

Kama umewahi kuangalia filamu ya mfalme Daudi na Mfalme Suleimani; utaona kuna utofauti katika vifo vyao,pia Biblia inasema Daudi alikufa kifo chema na uzee mwingi,ila Suleimani sijui kama inasema hivyo.

"Sasa kwenye filamu zao Daudi alikufa kama mtu aliyelala kama jinsi Biblia inavyosema, ila Suleimani alikufa kwa kukakamaa kama vile hataki kufa au anapokwenda siko alipokuwa amepatarajia."

Sasa tukija kwa usemi wa Yesu kwamba hakuvikwa kama miongoni mwa hawa wadogo itakuwa sehemu aliyoonyeshwa aende hakuitarajia ukizingatia alikuwa mfalme aliona si hadhi yake,hivyo basi alilazimishwa kwa nguvu maana maisha yake ya duniani ndio yaliyomchagulia hiyo sehemu baada ya yeye pia kuyachagua kwa kumuasi Mungu.

NB.WATOTO WA MUNGU,MUNGU HACHANGANYWI NA MIUNGU.Ile kauli ya jisaidie naye Mungu atakusaidia haimaanishi hivyo.Ni kumtafuta Mungu kwa bidii zako zote naye atakuonekania na kukupigania na kukushindia vita zako zote.Amen.

Mkuu , Mtumishi wetu tunaekuamini Mimi Nina swali dogo
Binafsi Nina mipango mikubwa ya kufanikiwa kiuchumi na nimegundua Bila ya Mungu Mkuu siwezi kuifanikisha abadani hivyo nikafanya Kama mlivyotushauri humu tufanye.. Mimi nikafanya hivi "E bwana , Jehovah, Yahweh, Mungu Uliyenipa nafsi , roho na mwili naomba Nisamehe makosa yangu yote niliyoyatenda kwa kuwaza, kunena na kutenda nikastahili adhabu yako , ila kwa rehema kuu Nisamehe na kuniokoa Mimi niliye masikini na dhaifu.

Baba Nakuja mbele za uso wako kwa kutumia damu ya mwanao yesu kristo ili nizungumze na wewe.. Baba Leo tarehe .. kwa hiari yangu Bila kushawishiwa na mtu , Wala kupiga yoyote , naweka nadhiri mbele yako kwamba , Ukinipa Utajiri katika maisha yangu yaliyobaki apa ulimwenguni, nitakutolea zawadi ya kuwakidhi na kusomesha mayatima idadi kadhaa , kwa miaka 7 Kila mmoja. Na agano hili nalitia muhuri wa damu ya yesu, ili liwe hai.. na Nina omba nafsi yangu uimbatanishe nawe ili nisinane kwa waovu.. katika damu ya Yesu kristo bwana wangu , Najua umenisikia nikamalizia kwa kusema Ushukuriwe Wewe Utupaye vyote tunavyokuomba na tunavyostahili Ameen.

Sasa mkuu , hoja yangu ni kwamba je ombi la namna hii linaweza chukua muda gani mbaka kutimia.? Na Mimi maisha yangu yote mbaka Sasa Nina 30yrs sijawahi kufika kwa waganga. Na bwana aniepushe.

Kuna muda Mambo yangu ndo Kama yanaharibika kabisa , kazi sipati , hela ya kujikimu inaleta shida. , nakwama wapi Mtumishi.
 
Safari iliyonikuta safarini
Mkuuu nasema hivi kwakua kabla sikujua kua ningepaswa kua hiv nilivyo ila niliwaza kua vile nilivyotaka mimi. Sikujua kua Mungu anayomipango yake kwangu. Sasa kazi yangu kiuhalisia hupingana na kilichoko ndani yangu(Utumishi).Uchumi ndo sehem niliko shikwa japo sasa hapa sababu ninyingi lipo kusudi natakiwa timiza ili nipate baraka.

Tafsiri ndoto hii
Niko kwa gar yaan dala dala na ilikua na tv na tulikua abiria wengi mno ila ile tv ilikua inaonyesha video moja ya watu wakiabudu ila mavazi yao na cheza yao nikama walikua wanafanya zihaka. Wanevaa nguo fupi huku wanabambiana na ni ibadani inavyoonyesha. Kuna wamama hapo kwa gar wakasema tv izimwe wengine wakasema hii ni roho hutengenezwa iwaingie watu. Kisha nikaamka

Ndoto ya 2
Nimeota napigana nawatu niwengi sana kiasi kwamba ningumu kuwashinda ila nikawa nauwezo wakuwapiga kimawazo ngumi moja nawaza adondoke na anadondoka nikaamka.

Mungu ni wa kila amtumikiaye katika roho na kweli naamin ataniongoza kwa kunipa njia sahihi nikaitumie nifike pale ahitajiko. Kwako 7seven. Ushauri pia ntafurahi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom