Je unaweza kufa 2016 na kuzikwa 2015?

hapa ndipo nnapoona watu wanajimix kwa kudhani muda unaenda mbele ama kurudi nyuma,binafsi nijuavyo muda ni uwepo/the existance of space ambayo haionyeshi kurudi nyuma ama kwenda mbele... ila watu tumechukulia hivyo kwa sababu kadharika...
ukitaka kujua kama ni uwepo huyo maiti uwe unamrudisha nyuma (kama alivyosema mweka mada) uone kama ataamka coz ya zile saa alizokuwa hai zinajirudi na mwili kutoharibika.
Mkuu umeelewa kweli mada iliyopo...?
 
Kuna concept ya time space travelling, ambayo ukisafiri kwa spidi kubwa kwenye space una-slowdown time. Hivyo siku moja in space inaweza kuwa miaka 20 dunian.

Ni complex idea, ila elewa hivyo. Watu wataenda kwenye solar systems za mbali kwa kutumia siku chache tu, lakini ni mamia ya miaka dunian. Watashangaa watakaporudi wanakuwa nyuma kwa miaka kibao na kila kitu kimebadilika sana.

Nao wanakuwa wanaishi past in present, maana wataonekana vijana wa miaka 20 kumbe wana miaka 600
time travelling....inawezekana kwa ndani ya dunia yetu? au kwenye sayari nyingine?
kama jibu ni ndiyo, basi upo uwezekano wa mtu kufa, kisha akazaliwa katika sayari nyingineyo...
 
wakuu asalaamu?

watu wengi hapa jf walishawahi kutoa michango yao kuhusu kurudi nyuma ya wakati yaani "back in time"
na mimi kwa mawazo yangu nahisi kama inawezekana!

mfano, nchi ya Rwanda iko nyuma ya Tanzania kwa saa moja , ikiwa Rwanda ni saa 12 asubuhi, basi Tanzania ni saa moja .

je ukifa Tanzania tarehe 1 january huwezi kuzikwa Rwanda tarehe 31 disemba.

wajuvi wa mambo nipeni ufafanuzi. !!
Nilifikiri ni uchawi kwa hili Mshana Jr, mpare wa milimani angekusaidia ila kwa kuwa ni geography wataalam wayakusaidia
 
je huo muda wa kufa na kusafirishwa kuwahi kule ambapo muda/masaa yapo nyuma utatumia usafiri gani uweze kuwahi? labda theoreticaly ukae mpakani mwa hizo nchi mbili ukisubiri kufauvushwe boda tu uzikwe jana yake kwa masaa ya tz. rwanda watakuconsider kuwa umekufa in future ukaja zikwa in present na tz wata kuconsider umekufa in present bt ukazikwa in past. ni concept ngumu kidogo kumeza but if u cant convivce them confuse them
Ulivyoanza nikaona kama vile uelewi lakini ukamalizia kwa weledi mkubwa.
Kuna documentary BBC jamaa wanaona kwamba vitu vingi ambavyo tunavifanya duniani na kuviamini ni simulations za 'great thinkers', ndio maana hadi leo tuna picha za Mars, Jupiter, Pluto na nyingine wanadai ni 150 light years kitu ambacho kwa asilimia kubwa ni imaginations.
Kwa maana hiyo kama mtu anaishi kwenye kijiji cha mpakani pale Rusumo na mwingine anaishi upande wa Rwanda kwa umbali wa mita 50, ni wazi bendera upande wa Tanzania itashuka saa moja kabla ya upande wa pili. Hivyo hivyo mtu akifa na katika dakika 45 wakamzika upande mwingine hii thgeory kwa akili hii tunayotumia (ya simulations) ni sawa lakini uhalisia wake, duh!...
 
time travelling....inawezekana kwa ndani ya dunia yetu? au kwenye sayari nyingine?
kama jibu ni ndiyo, basi upo uwezekano wa mtu kufa, kisha akazaliwa katika sayari nyingineyo...

Inaweza kuwa ndani ya solar system yetu, lakini zaidi kwenye deep space. Ukiwa kwenye chombo kinachosafiri kwa kasi sana (karibia ile ya mwanga), then una-slow down time. Hii ina maana kwamba wewe umri wako utasogea taratibu sana kuliko mtu uliyezaliwa nae siku moja ambaye umemuacha duniani. (Approaching the speed of light, a person inside a spaceship would age MUCH slower than his twin at home/duniani). Habari ya kuzaliwa sayari nyingine haina uhusiano na hii theory.

Maana yake ni kwamba, ukiwa kwenye hicho chombo, siku moja ndani ya hicho chombo inaweza kuwa sawa na miaka kadhaa duniani. Hivyo utakaporudi duniani baada ya siku chache unaweza kuta wadogo zako ni wazee sana wakati wewe bado kijana mbichi (hehehe).

NB// Hii ni complex theory ya watu wenye akili zilizopitiliza, kwa mbali sana wanasayansi wameanza kuona ukweli wa hii kitu
 
wakuu asalaamu?

watu wengi hapa jf walishawahi kutoa michango yao kuhusu kurudi nyuma ya wakati yaani "back in time"
na mimi kwa mawazo yangu nahisi kama inawezekana!

mfano, nchi ya Rwanda iko nyuma ya Tanzania kwa saa moja , ikiwa Rwanda ni saa 12 asubuhi, basi Tanzania ni saa moja .

je ukifa Tanzania tarehe 1 january huwezi kuzikwa Rwanda tarehe 31 disemba.

wajuvi wa mambo nipeni ufafanuzi. !!

nenda uzikwe ukitumia kalenda yako au ya waislam
 
Kuna concept ya time space travelling, ambayo ukisafiri kwa spidi kubwa kwenye space una-slowdown time. Hivyo siku moja in space inaweza kuwa miaka 20 dunian.

Ni complex idea, ila elewa hivyo. Watu wataenda kwenye solar systems za mbali kwa kutumia siku chache tu, lakini ni mamia ya miaka dunian. Watashangaa watakaporudi wanakuwa nyuma kwa miaka kibao na kila kitu kimebadilika sana.

Nao wanakuwa wanaishi past in present, maana wataonekana vijana wa miaka 20 kumbe wana miaka 600
Huko kwenye space huzeeki au? Mfano nilimwacha pacha wangu huku nitakuuta ana miaka mingi kuliko mimi?
 
wakuu asalaamu?

watu wengi hapa jf walishawahi kutoa michango yao kuhusu kurudi nyuma ya wakati yaani "back in time"
na mimi kwa mawazo yangu nahisi kama inawezekana!

mfano, nchi ya Rwanda iko nyuma ya Tanzania kwa saa moja , ikiwa Rwanda ni saa 12 asubuhi, basi Tanzania ni saa moja .

je ukifa Tanzania tarehe 1 january huwezi kuzikwa Rwanda tarehe 31 disemba.

wajuvi wa mambo nipeni ufafanuzi. !!
kwa rwandA haiwezekani labdA amerikA
 
Huko kwenye space huzeeki au? Mfano nilimwacha pacha wangu huku nitakuuta ana miaka mingi kuliko mimi?

utazeeka slow sana, ishu ni kwamba muda utaenda pole pole, wakati wewe umeongeza mwaka mmoja, nduguyo ataongezeka miaka 100, hivyo lazima yeye ataonekana mzee sana kwako. Kwa kifupi wewe utakuwa na umri mdogo japo mmezaliwa siku moja ;););)

Another confussion :mad::mad::mad::mad:
 
wakuu asalaamu?

watu wengi hapa jf walishawahi kutoa michango yao kuhusu kurudi nyuma ya wakati yaani "back in time"
na mimi kwa mawazo yangu nahisi kama inawezekana!

mfano, nchi ya Rwanda iko nyuma ya Tanzania kwa saa moja , ikiwa Rwanda ni saa 12 asubuhi, basi Tanzania ni saa moja .

je ukifa Tanzania tarehe 1 january huwezi kuzikwa Rwanda tarehe 31 disemba.

wajuvi wa mambo nipeni ufafanuzi. !!
Hiyo kitu hakuna. Kwa kawaida muda ukiandikwa inatakiwa kuweka na time zone (japo sisi hatujazoea kufanya hivyo), kwa hiyo hata ukifia mpakani kabisa mwa Tanzania na Rwanda au tanzania na Burundi na death certificate kabisa ikaandikwa (within minutes) inatakiwa ionyeshe ni time zone gani (Saa za Afrika mashariki), na ukivushwa kwenda Rwanda Burundi ukazikwa saa tano na dakika 53 usiku huo huo dakika chache baada ya kufa, wakirekodi muda wako wa kuzikwa wanatakiwa kuweka time zone (Saa za Afrika ya Kati). Hizo reference zitatosha kuondoa utata huu maana kama mtu akiamua kutumia muda wa E.A au akatumia muda wa C.A inabidi awe consistent all the way.
 
Back
Top Bottom