Je, Sokoine alikufa kwa ajali ya gari, Au aliuawa kwa kupigwa risasi 18 kifuani?

Wanaokumbuka vizuri waatujulishe. Gari alilokuwa anatumia Sokoine siku ile alipopata ajali lilikuwa Mercedes Benz au Land Rover?
 
Je, nani anasema ukweli kuhusu kifo cha Sokoine.!? Ni Nyerere aliyedai alikufa kwa ajali ya gari, lakini hakutaka kabisa watu wahoji wala kuchunguza ajali hiyo ilikuwaje au tumuamini Dr. Shaba aliyewahi kudai kwamba wakati anamfanyia postmortem alitoa risasi 18 kifuani..!? Nani alisema ukweli na nani alidanganya..!? Je, ukifa kwa ajali ya gari unatolewa risasi kifuani..!? Je, na aliyekufa kwa ajali ya gari kuna haja ya kuwaomba na hata kuwalazimisha watu waamini kwamba ni kweli kilikuwa kifo cha ajali ya gari..!? Je, kifo cha Edward Moringe Sokoine kitaendelea kuwa siri nyeti na tata ya taifa hili hadi lini…!!!!!!!!!!????????
Of course I found 18 bullets in his chest when I was doing postmortem” haya ni maneno yalitamkwa kwenye Bar moja jijini Dar es Salaam na Dr. Shaba (surgeon) daktari bingwa wa maswala ya upasuaji; ikumbukwe Dr. Shaba ndye aliyeufanyia mwili wa Marehemu Edward Sokoine utafiti baada ya kuuwawa kule Dakawa nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Mwalimu Nyerere alifanya safari ya ghafla kwenda Msumbiji kwa Rais Samora Machel kuomba ushauri juu ya kasi ya utendaji wa waziri wake mkuu; kasi ambayo ilitishia usalama wa nafasi yake
haya ni maneno ya afisa mmoja mkubwa na msaidizi wa Mwalimu Nyerere aliyenukuliwa na baadhi ya wananchi.
Ndugu zangu watanzania wenzangu kijana wetu, ndugu yetu waziri mkuu Edward Moringe Sokoine amefariki dunia baada ya msafara wake kupata ajali huko Dakawa nje kidogo ya mji wa Morogoro; ndugu zangu watanzania nawaombeni sana muamini kwamba waziri mkuu Edward Sokoine amefariki kwa ajali ya gari
haya ni maneno ya Mwalimu Nyerere aliyowatangazia watanzania kwenye taarifa ya habari ya saa 10.00 kupitia Redio Tanzania tarehe 12 April 1984. “It’s impossible to believe that Prime Minister Edward Sokoine was died after his Mercedes Benz car crushed..!!! Even if the Mercedes Benz could crush with Scania lorry loaded with 40 tons still couldn’t die..!!! We have to send a team of seven experts to Tanzania to investigate on this issue because it may pose threats to our market strategy
haya ni maneno ya uongozi wa juu wa kampuni ya Mercedes Benz ya Ujerumani ambayo inatengeneza magari ya Mercedes Benz malumu kwa ajili ya kubeba viongozi wa dunia nzima, na gari aliyokuwa amepanda waziri mkuu Sokoine wakati kifo chake kinahusishwa na ajali hiyo ilikuwa Benz. Ajali ya Waziri mkuu Marehemu Edward Sokoine ilitokea muda mfupi baada ya Mzee Rashidi Kawawa ambaye alikuwa waziri katika ofisi ya Rais kuuza meli ya wananchi kinyemela kwa Tsh. 60 millioni ya mwaka 1984 ambapo Tsh. 20 zilikuwa ni sawa na US $ 1; ina maana meli hiyo iliuzwa kwa US $ 3 million (Tsh. 6.6 Billion) kwa thamani ya leo. Meli hii aliuziwa tajiri mmoja wa Kihindi kwa jina maarufu Lord Rajpar. Pamoja na kwamba Mwalimu Nyerere na Mzee Kawawa ambao ndiyo wahusika wakuu wa ufisadi huu wa kutisha walishatangulia mbele ya haki, lakini shahidi mkuu na mshitakiwa namba tatu Lord Rajpar bado yupo hai na yupo hapa nchini. Je, waziri katika ofisi ya Rais anaweza kufanya ufisadi mkubwa wa kutisha wa Tsh. 6.6 Billion na Rais asiwe na habari na hata akijuwa bado tu abaki kimya….!!!??? Je, Nyerere na Kawawa waligawanaje pesa ya ufisadi huo…!?
Rashidi naenda Dodoma kulihutubia bunge nakupa siku saba uzirudishe pesa za wananchi Tsh. 60 millioni ulizouza meli ya wananchi; na kama ukishindwa nitakupeleka Redio Tanzania ukawaambie watanzania umezipeleka wapi pesa zao
hayo ni maneno ya mwisho kwa watanzania yaliyotamkwa na Marehemu Sokoine kwa kupitia Redio Tanzania wakati anajiandaa kwenda kulihutubia bunge Dodoma na alipoondoka kwenda Dodoma Mzee Kawawa akakimbilia kijijini kwao huko Liwale na Mwalimu Nyerere akafanya safari ya dharura nchini Mozambique. Waziri mkuu Edward Sokoine alitakiwa arudi kwa ndege kutoka Dodoma, lakini ghafla alipangiwa kwamba arudi na gari kwa vile alipangiwa na Mwalimu Nyerere akague mashamba ya mahindi mkoani Morogoro na wakati anarudi Dar es Salaam msafara wake ukapata ajali ya gari baada ya gari lilikokuwa limembeba kugongana na gari la Toyota Landcruser la mtu mmoja anayetajwa kama Dumisan Dube ambaye wengine wanamtaja kama raia wa Afrika ya Kusini na wengine wanamtaja kama raia wa Mozambique ambaye aliingia nchini muda mfupi kabla ya kifo cha Sokoine kutokea. Inasadikiwa kwamba kwenye mgawo wa ufisadi huo mkubwa wa kutisha enzi hizo Mwalimu Nyerere alichukuwa Tsh. 50 millioni na Mzee Kawawa Tsh. 10 millioni; na hii ndiyo sababu kubwa ambayo Mwalimu Nyerere alikuwa anampenda sana Mzee Kawawa kwa vile hata aliweza kutumwa na Nyerere kufanya jambo baya na la kutisha, lakini bomu likifumuka Nyerere ameshamkana na wala hakuwahi kumtaja Nyerere wala kulalamika, bali siku zote alibeba lawama zote za bosi wake ili aendelee kuwa karibu naye na kutumbua nchi.
Je, kwa mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini kwamba waziri mkuu akiwa kwenye msafara anaweza kufa kwa ajali ya gari tena siyo ya gari lake kupinduka, hapana, bali anakufa kwa kuwa gari lake limegongana na gari linguine ambalo halipo katika msafara huo…!!!??? Wote tunajua kwamba msafara wa viongozi wakuu wa kitaifa inakuwa na ulinzi mkali na hata hivyo si rahisi gari kuingilia msafara wa waziri mkuu kwa vile kuna pikipiki na magari mengi yanayotangulia mbele kabla ya gari lake na huku mengine mengi yakiwa nyuma yake pia. Sasa huyo Sokoine amekufaje kwa ajali ya gari..!!!??? Ningeambiwa amekufa kwa vile gari lake lilikuwa kwenye mwendo mkali likaserereka na kupata ajali ningelikubaliana na maneno hayo, lakini tuliambiwa na bado wanaendelea kuambia kwamba Sokoine alikufa kwa kuwa gari yake iligongana na Landcruser ya Dube..!!! “Sitaki uchunguzi wowote wa wataalamu saba wa kampuni ya Mercedes Benz ya Ujerumani; nawataka wachunguzi hao waondoke nchini mwangu mara moja kwa vile nilishawaambia watanzania kwamba Sokoine amekufa kwa ajali ya gari na wameshaamini; sasa wakifanya uchunguzi na wakaja na taarifa tofauti zinazoonyesha kwamba Sokoine hakufa kwa ajali ya gari, bali ameuwawa nitawaambia nini watanzania” haya ni maneno ya Mwalimu Nyerere. Je, mtu aliyekufa kwa ajali ya gari una haja yoyote ya kuwaomba wananchi na ndugu zake waamini kwamba ni kweli amekufa kwa ajali ya gari..!? Kama kweli alikufa kwa ajali ya gari ni kwanini Mwalimu Nyerere alikataa timu ya Wajerumani wa Mercedes Benz wasifanye uchunguzi wao…!?
Kwanini kifo cha kutatanisha cha Marehemu Edward Sokoine kitokee mara tu baada ya waziri na swahiba wa karibu wa Mwalimu Nyerere Mzee Kawawa alipouza meli ya serikali kwa kiasi cha Tsh. 6.6 Billion na hata Sokoine alipomjulisha Mwalimu Nyerere kuhusu hilo hakupata ushirikiano wowote zaidi ya kujengewa chuki na ratiba ya msafara wake ikabadilishwa kwa kuambiwa kwamba asirudi kwa ndege, bali arudi kwa gari ili akague mahindi mkoani Morogoro na hapo hapo ndipo akauwawa na ajali ya gari…!!!! Ikumbukwe kwamba wakati anaondoka kwenda Dodoma Marehemu Sokoine alisema maneo ya mwisho yafuatayo “Nikimaliza kuwatumbua majipu mawaziri wangu, basi napanda juu nikamtumbue majipu Mwalimu Nyerere kwa vile anaonekana siyo msafi” maneno haya ya Marehemu Sokoine yalimtisha sana na kumuweka katika wakati mgumu Mwalimu Nyerere na alikuwa hana jinsi yoyote zaidi ya kwenda kuomba ushauri kwa rafiki yake Samora Machel wa Mozambique.
Kulingana na ukweli huu ndiyo maana nawachukia wale wote wanamtaja Mwalimu Nyerere kwa uadilifu. Ufisadi wa kuuza meli ya taifa uliofanywa na Mzee Kawawa ulipata Baraka zote za Mwalimu Nyerere na hata pesa iliyopatikana waligawana na ndiyo maana hata Marehemu Sokoine alipokuwa anamkemea na kumbana Mzee Kawawa Mwalimu Nyerere alikuwa anambeza na ni kipindi hiki ambacho Mwalimu Nyerere alimuona Sokoine kwamba ni mtu hatari katika serikali yake. Sitaki kuzungumzia ufisadi wa Mwalimu Nyerere wa mali nyingi alizojilimbikizia nchi za nje, ila kama Rais Magufuli anakusudia kwa dhati kupambana na ufisadi kwa dhati kwa ajili ya kulikomboa taifa hili, basi anatakiwa aunde tume huru ili imchunguze Mwalimu Nyerere na mfumo wake wote wa utawala; tume hiyo ikiundwa, basi tutataji hadharani wapi Mwalimu Nyerere amezificha mali zake zote ili watanzania wote waweze kufunguka.
Nihitimishe makala hii kwa kusema kwamba hakuna binadamu mwadilifu mpaka athibitishe kwa vitendo. Edward Sokoine alikuwa mwadilifu na msafi kama malaika wa mbinguni na ndiyo maana Mwalimu Nyerere na mafisadi wenzake hawakumpenda na waliona wamsingizie kifo cha ajali ya gari ili watanzania waendelee kuwa watumwa wa mfumo wake wa kidhalimu. Aliyekufa kwa ajali ya gari hubembelezwi uamini, bali unaona wewe mwenyewe. Aliyekufa kwa ajali ya gari wasioamini hawazuiwi kuchunguza kifo chake. Aliyekufa kwa ajali ya gari hawezi kutolewa risasi 18 kifuani mwake. Ukiyatafakari yote haya unakuta kwamba kifo cha Edward Sokoine kinaendelea kuwa siri nyeti na tata ya taifa hili licha ya kwamba Rais Magufuli anaimba nyimbo za mabadiliko ya kinafiki…!!!!!!!!!!!

©Dr. Noordin Jella

Mkuu ilikuwa ajali kama ajali nyingine tu. Nisiache kukuwekea hii hapa:

Dr. Noordin Jella
Hii story umeunga vipande vya hadithi ulizosimuliwa toka sehemu mbali mbali na wewe ukatudanganya hapa tukuone unajua ukweli.
Story ya awali kabisa ya kifo cha Sokoine ilihusu uchawi na kwamba alirogwa na kupelekwa Gamboshi na Kawawa na genge lake la akina Mzee Msuya. Kwamba kilichozikwa ni gogo tu.
Awali tukiwa watoto tuliamini sana huu ujinga, hadi siku nilipokutana uso kwa Uso na dereva wa Mercedes Benz aliyekuwa akiendesha gari ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine. Hakuna hata moja uliloeleza linaloshabihiana na ukweli. Na usiniambie eti alichosema dereva yule kilipangwa na system. Watu wa Musoma Mjini wanamfahamu huyu jamaa maana amefanya kazi ofisi ya RSO Mara zaidi ya miaka 7 ambako alihamia akitokea Rukwa na amefariki miaka chini ya 5 iliyopita. Nyerere hawezi na asingeweza kufanya ufisadi wa kitoto kama huu. Wazushi kama wewe waliwahi kusema Nyerere ana mashamba ya Miwa Cuba, lakini Leo tunaona kina Makongoro wanakubali kuajiriwa na miaka 62. Tafuteni Kiki nyingine lakini hii haitusombi.
 
Hivi huyo Dumisan Dube raia wa afrika kusini wanayesema alimgonga na gari alifanywa nini?

Alifikishwa mahakamani akafungwa miaka 13. Lakini baada ya kina Mandela kuchukua nchi, kibinadamu alirejeshwa kwao.

Nyerere alikuwa mtu sana hata katika kukikubali kifo cha swahiba wake Sokoine ki hivi:

Nyerere aliyeweza kupiga simu benki kuu na kuagiza apewe fedha anazotaka kwa sababu za "usalama wa taifa" alihitaji kuuza meli ili aibe hela za umma?

Ushawahi kufika kwa Nyerere ukaona alivyoishi?
Ujinga ndo umeanzia hapo.. yaani nyerere aibe hela kwa kuuza meli tena aliyoinunua yeye mwenyewe!?? Halafu sokoine alikuwa na ukubwa gani wakati alikuwa mteule wa nyerere?? Hii ni moja ya hekaya za kitoto mnoo!!
 
Nimesikitika sana, Nyerere, mtu aliyeweza kutuibia alivyotaka kama Mobutu alivyoiba Congo, lakini kwa uadilifu mkubwa akaishi maisha simple tu, kwa muktadha wa kiongozi wa taifa, leo hii amekuja kusingiziwa wizi kijinga hivi.

Nyerere ana makosa mengi, kifalsafa, kisiasa, lakini hili la wizi bado sijaliona.

Alipofariki Nyerere, alikuja Mama Gracia Machel, mke wake Mandela, mwanzo kabisa, akitaka kuwa karibu na mjane Mama Maria Nyerere msibani.

Basi yule Mama akapelekwa Msasani kwa Nyerere.

Alipofika Msasani, alivyopaona pako simple vile, na jina la Nyerere alivyolijua limevuma dunia nzima miaka na miaka kwamba Nyerere ni bonge la giant katika siasa za dunia, yule Mama akaona bila shaka hapa si kwa Nyerere, hii ni government guest house tu nimeletwa kupumzika kabla ya kufika kwa Nyerere.

Mama Gracia Machel akasema jamani nipelekeni kwa Nyerere nataka kufika mara moja nikae na Mama Maria, msinicheleweshe.

Watu wakamwambia Mama mbona umeshafika kwa Nyerere ndiyo hapa.

Yule Mama alivyopaona pako simple ilikuwa kama hajaamini hapo ndiyo kwa Nyerere.

Nyumba ya Butiama ya Nyerere aliyojengewa na jeshi ndani kuna viti vya plastiki. Vile viti wanavyoweka watu kukalia nje kwenye bar kunywa pombe, viko ndani Wazanaki wanakalia. Kama vile si nyumbani kwa rais.

Sasa mtu kama huyo aibe hela afanyie nini?
 
Kwa maisha aliyoishi Nyerere baada ya kustaafu. Na hata aina ya maisha ya familia yake baada ya kifo chake, sioni base yotote ya kudai Nyerere alikuwa fisadi.

Linganisha familia ya Jomo Kenyatta wa Kenya na ya Nyerere. Familia ya Kenyatta ni matajiri sana hata kwa macho ya nyama tu iko wazi kabisa. But familia ya Nyerere hata ukifika pale Butiama wako kawaida sana kimaisha.
 
Hata kama aliuwawa na Nyerere secret police,tukijua sasa hv haiwezi kutusaidia kitu,wote waliohusika wameishakufa,
Ni kawaida,ukijifsnya kieleele zaidi ya Raisi,lazima utulizwe,ilitokea kwa Robert Ouko wa Kenya,George Saitoti wa Kenya,
Ni system duniani kote
 
“Of course I found 18 bullets in his chest when I was doing postmortem” haya ni maneno yalitamkwa kwenye Bar moja jijini Dar es Salaam na Dr. Shaba (surgeon) daktari bingwa wa maswala ya upasuaji;

A single bullet is enough to totally eliminate the intented target!
 
1623506239610.png

Gari iliyosababisha umauti kumkuta
 
Back
Top Bottom