Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,562
- 37,916
April 12, 1984 Nilikuwa na umri wa miaka zaidi ya 10. Nalikumbuka vizuri tangazo la Mwalimu akitutangazia kifo cha Waziri Mkuu aliyepata kupendwa zaidi na Watanganyika Tangu Uhuru Edward Moringe Sokoine.
Kilichosababisha kupendwa kwake ni jinsi alivyowajali watu wa Hali zote na kuhakikisha wote wanaishi maisha ya heshima na utu.
Upungufu mkubwa wa bidhaa uliojitokeza baada ya Vita ya "Kagera" kutokana na upungufu wa Dola aliushughulikia Kwa Moto mkali baada ya kugundua wafanyabiashara wanaficha bidhaa muhimu makusudi ili kuongeza uhaba Kwa lengo la kupandisha bei.
Ni kiongozi aliyewahi kuacha ofisi (Uwaziri Mkuu) na kurudi shule kuongeza maarifa katika kilimo na uchumi. Aliporejea 1982 Mwalimu akamrejeshea nafasi yake.
Sifa Kuu zilizomtifautisha Sokoine na wenzake wengi ni;
1. Kuchukia rushwa kiuhalisia.
2. Ufuatiliaji wa kina na uchukuaji wa hatua bila kuona muhali.
3. Kutojilinbizia Mali na kuridhika na mshahara na posho halali alizolipwa.
4. Hakuwa na upendeleo wa kieneo au kifamilia.
5. Kiongozi aliyejiona Mtumishi wa watu badala ya mtawala.
Nk. Nk.
Leo April 12, 2024 miaka 40 baada ya kifo chake cha ajali pale Dumila Morogoro serikali nzima iko Monduli.
Wanasema wamekwenda kumuenzi Sokoine. Wanakwenda kuenzi jina lake au matendo yake?
Nani anaweza kuwa hata nusu tu ya Sokoine? Nani robo ya Sokoine? Mbona kama wamekwenda kwenye sherehe ya Nanenane?
Mnakwenda kumuenzi Mtu ambaye matendo yake na yenu ni mbingu na ardhi?