Je, ndoa ngapi “zinatosha” mtu mmoja kufunga?

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,835
4,684
Wakuu,

Nimekaa nikafikiria suala zima la kufunga ndoa, talaka na kufunga ndoa tena.

Najua kuna dini zinakataza talaka na kuna ambazo zinaruhusu mtu kuoa wake wengi kwa wakati mmoja. Lengo hapa sio tuangalie kwa jicho la kidini bali kijamii. Let us factor suala la dini out.

Katika ndoa kuna kukosea, kuna kugombana na kadhalika na ndoa huvunjika wakati mwingine watu wakiwa na umri mdogo hivyo wanaingia kwenye mahusiano mengine na ndoa nyingine kuzaliwa.

Je, ni ndoa ya ngapi mtu akifika tunasema sasa hapana huyu amezidi au huyu atulie tu sasa anazingua?

Na je, namba hii ni tofauti kwa wanaume na wanawake?

Kwanini?

Karibuni

IMG_5388.JPG
 
Ndoa moja inatosha
Ikifeli na wewe umefeli kwenye suala hilo hivyo kaa aside
 
Siku zote ndoa ni ile ya kwanza...

Kama utafanya nyingine hizo ni za kwako na mambo yako...

Cc: mahondaw
 
Me nadhani pale jamii yako tuu itakapo kuchoka hapo ndio tuseme Wewe Ndoa basi uwe Mwanamke Au Mwanaume, Hatuwez Sema ndoa ngapi
.
Kuchokwa huko nadhan ni kote kote tuu , Huwezi kuwazungusha Watu kila Siku Ndoa uwe Mwanamke Au Mwanaume umachokwa vizuri
.
Nina Shangaz yangu harusi yake ya Mwisho ilikua ni ya Tatu, baada ya maharusi kuondoka watu wakasema hii ya mwisho hatuji tena
Hap enyewe tulilkua wachache
 
Ndoa iko moyoni mwako, hata kama ni ya 99.....moyo wako una amani? una furaha? ukiwa navyo hivyo hiyo ndio ndoa halisi....
amani , upendo na furaha, kwani hapo Mungu anaishi.......
 
Me nadhani pale jamii yako tuu itakapo kuchoka hapo ndio tuseme Wewe Ndoa basi uwe Mwanamke Au Mwanaume, Hatuwez Sema ndoa ngapi
.
Kuchokwa huko nadhan ni kote kote tuu , Huwezi kuwazungusha Watu kila Siku Ndoa uwe Mwanamke Au Mwanaume umachokwa vizuri
.
Nina Shangaz yangu harusi yake ya Mwisho ilikua ni ya Tatu, baada ya maharusi kuondoka watu wakasema hii ya mwisho hatuji tena
Hap enyewe tulilkua wachache

Hebu niambie, shangazi alionekana kuwa na bashasha kama za ndoa ya kwanza?
 
Mm naona ntu hata afunge 10 ni yeye mradi isiwe oa acha oa acha hapo utakera walimwengu
 
Hebu niambie, shangazi alionekana kuwa na bashasha kama za ndoa ya kwanza?
Ndoa za Kwanza Sikuhudhulia kwa kweli
Lakin kwenye ile ndoa alikua nayo hyo Bashasha Usoni
Kwanini unauliza kwa Makini hvyo
Is there Anything happen huk Dada ?
 
Me nadhani pale jamii yako tuu itakapo kuchoka hapo ndio tuseme Wewe Ndoa basi uwe Mwanamke Au Mwanaume, Hatuwez Sema ndoa ngapi
.
Kuchokwa huko nadhan ni kote kote tuu , Huwezi kuwazungusha Watu kila Siku Ndoa uwe Mwanamke Au Mwanaume umachokwa vizuri
.
Nina Shangaz yangu harusi yake ya Mwisho ilikua ni ya Tatu, baada ya maharusi kuondoka watu wakasema hii ya mwisho hatuji tena
Hap enyewe tulilkua wachache
Nafikiri unaongelea harusi, Mleta mada anaongelea ndoa. Ndoa sio lazima iwe na sherehe ya harusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hakuna aliyeumbwa ili aishi peke yake,mwingine akiachia unatafuta atakayeziba pengo..hayo mengine ni makaratasi tu
 
Back
Top Bottom