Je, binadamu ni kizazi cha Reptilia au kaumbwa na Annunaki?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,278
5,457
Nimekutana mara kadhaa na mafundisho ya siri kuhusiana na chanzo cha binadamu kuwa tuliumbwa na aliens wa nje ya sayari yetu toka katika sayari za mbali katika kundi nyota za huko nibiru waumbaji hao akina enki,enlil n.k wajulikanao kama Annunaki inasemekana waliumba viumbe binadamu hili wawasaidie katika kazi za machimbo yao ya dhahabu huku duniani hili wakakarabati sayari yao then ikapanda ikashuka then tuko hapa nasikia watarudi tena kutukomboa mikononi mwa watesi wetu Reptilia na Draco zetus.

Reptilia nao hawako mbali kwenye hili nao wanaushahidi dhahiri kupitia vitabu vya dini tunazotumia kuwa wao ndiyo haswaa chanzo chetu binadamu japo tulitengenezewa uadui nao kwa makusudio fulani.

Hii ni baadhi ya mistari katika biblia inayothibitisha hili:-

Mathayo 12:34 Enyi kizazi cha nyoka; mnawezaje kusema mambo mema hali nyinyi ni waovu?

Mathayo 23:33 Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa jehanamu?

Mwanzo 3:15, Yehova alisema: "Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino"

Kulingana na mistari kadhaa katika maandiko matakatifu Shetani ufananishwa na nyoka ambaye ni kundi la Reptilia na hata sisi binadamu tokea kuzaliwa ni dhahiri kuwa tumekwisha-kuhukumiwa pamoja naye na tu wadhambi ndiyo maana ya ubatizo kwa wakristo.

Hivyo basi maandiko ya dini umwelezea binadamu kama uzao wa jamii ya nyoka ambaye kwa namna fulani amelaaniwa kuwa adui na asili yake na watachukiana wao kwa wao yaani uzao wa nyoka na uzao wa mwanamke(binadamu) watang'atana na kupondana visigino, ila hapo hapo binadamu anatakiwa ajikomboe au ajinasue toka katika asili yake ya dhambi na arudi nuruni.

Ila wale wanaofundisha kuhusu asili ya binadamu kuwa Annunaki nao uwapinga kizazi cha Reptilia nakusema Binadamu hili ajitambue ni nani ana budi kufanya meditation, yoga na Kundalini (apokee nyoka wawili wa shaba) hivyo akishafungua jicho la tatu ataweza kujua yote yaliyojificha.

Lakini cha kushangaza kwa Annunaki ushahidi wao kuhusu wanachokihubiri upitia maandiko hayo hayo yanayomwongelea Reptilia kuwa chanzo cha binadamu kama lugha ya symbolism na alama ambazo ni lazima zifumbuliwe/zitafsiriwe katika namna fulani ya kufikiri(utumia filosofia ya freemanson)

Sasa ukiunganisha nukta kati ya Reptilia na Annunaki na bado akina Draco na wengineo unashindwa kuelewa yupi ni mkweli na yupi ni mwongo.
 
MAMBO MENGINE KUJICHOSHA TU, UNAWEZAJE KUFUATILIA ASILI YAKO WAKATI WOTE TUMEJIKUTA HAPA TUNAZAANA, CONCEPTS ZA ASILI YA MWANADAMU NI NYINGI MNOOO

TUTAFUTE NAMNA YA KUPAMBANA NA BEI YA MCHELE

Lakini haikuondolei haki ya kudadisi ili walahu kukisia tu
 
MAMBO MENGINE KUJICHOSHA TU, UNAWEZAJE KUFUATILIA ASILI YAKO WAKATI WOTE TUMEJIKUTA HAPA TUNAZAANA, CONCEPTS ZA ASILI YA MWANADAMU NI NYINGI MNOOO

TUTAFUTE NAMNA YA KUPAMBANA NA BEI YA MCHELE
Kuna hearsay (tetesi) kuwa Bitozo katema nyongo kuwa atakaa kimya hadi bei ya mchele labda ifike 5000!

Ni kweli kasema au kawekewa maneno mdomoni?

Kama kasema je, Waislamu wa bara si watafunga mwezi mtukufu kwa dhiki?

Au watahamia Zenj hadi Ramadhani iishe!

Je, Waislamu na Wakristo (ambao wote ni dini za kufunga kula kwa ajili ya ibada) si watamkumbuka jembe?

Washauri wa Bitozo chondechonde!

Nimeduwaa kuona Bashe amesalimika kwenye mabadiliko ya baraza la mawaziri.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom