Mtanzanyika
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 370
- 425
- Thread starter
- #21
mkuu mpaka muda huu najua ulishaagiza gari, tupe basi mmrejesho na sisi wengine tufaidike
Kweli mkuu, niliagiza gari last year na Beforward moja kwa moja kutoka Japan kupitia simu yangu ya Mkononi. Gari ilifika miezi miwili baada ya kuagiza ikiwa katika ubora ule ule kama niliouona kwenye picha. Beforward walinipa nafasi ya kubargain nao bei ya gari na walifanikiwa kunipunguzia USD 450 kutoka bei ambayo walikuwa wameiweka kwenye website Yao.
Kila kitu cha kwenye gari nilikikuta kama kilivyo hakukuwa na wizi wala upotevu wa kitu chochote. Gari niko nayo takribani miezi 6 sasa na wala hakuna tatizo lolote service pekee niliyofanya ni kumwaga oil sijawahi kubadilisha chochote kwenye gari. Narecommend Beforward kuwa ndo kampuni bora kabisa ya uagizaji wa magari kutoka Japan kwa kigezo cha ubora wa magari, uaminifu, huduma bora kwa wateja na nafasi ya kubargain bei ya gari.
Sent using Jamii Forums mobile app