Ipi kampuni nzuri ya kuagiza gari kutoka nje kati ya SBT na Befoward?

Mtanzanyika

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
370
425
Heshima kwenu wakuu.

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu. Ningependa kujua ni kampuni gani nzuri ya kuagiza gari kutoka Japan kati ya SBT na BEFORWARD.?

Vigezo viwe katika maeneo yafuatayo:
(1) Ubora na uzima wa magari
(2) Uharaka wa huduma
(3) Uaminifu wa watumishi
(4) Huduma nzuri
(5) Bei ya magari

Karibuni kwa mchango kwa wale wenye ufahamu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Niende nje ya hizo options zako kwa upande wangu sehemu bora ni trade carview ingawa sio maarufu.

-hawa magari sio ya kwao hivyo hawana interest na gari lazima liuzwe.

-wanakuunganisha na mwenye gari hivyo unafursa ya kumuhoji chochote unachotata anaelimiliki gari hadi utakapojiridhisha.

-wanatoa huduma ya check in details, nje ya picha zilizowekwa kwenye matangazo wao watakwenda na kulikagua tena gari na kulipiga picha zingine nje ya zile zilizowekwa na muuza gari hivyo kama kuna tatizo lilifichwa utaliona hapa na utahairisha manunuzi
Mtanzanyika,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
analgesic,

Ni kweli kabisa,nimeshawahi nunua gari kwa hawa jamaa,gari ilikuja kama walivyonitumia picha baada ya wao kuikagua.

Sijui huduma hii kama bado wanayo. Ukishakubaliana na muuzaji unalipa hela wako trade carview then wao watampa muuzaji gari ikishafika kwenye yard ya tradecarview na kukaguliwa kama ipo kama alivyosema muuzaji.

Kingine gari za hawa jamaa nyingi ni zile zilizoenda km chache saana ingawa bei yao nao ipo juu kiasi uki compare na bforward.
 
Kwa nijuavyo Mimi

Be forward, Sbt, Enhance n.k
Wanauza magaei kulingana na 'mfuko' wako mteja jinsi ulivyo

Ukiingia kwenye site zao, kuna sehemu huwa wana magari 'premium' hayo ndio unakuta yanakua na gharama kubwa, yet kiwango cha ubora cha juu zaidi.

Kwahiyo, kwa mtazamo wangu, ni kwamba wote wako vyema, ni suala la wewe na budget yako na gari unayoihitaji.

Aidha, unaweza kuja ofisini kwetu ukishafikia uamuzi. Sisi tunakuletea gari uliyochagua kwa malipo ya awamu -awamu ya hadi miezi saba.

Mfano, kama labda umechagua IST
Unatupatia unatupatia stock id yake
Tunapiga hesabu zote kwa pamoja sisi na wewe

Madharani ni ist sema 12m ya gharama zote unalipia 9,000,000
Gari ikifika, unakabidhiwa

3,000,000 iliyobkia unamalizoa kwa instalment

Yani kila mwezi 429,000
For 7 months period.

Karibu ofisini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila nikitaka kununua gari kupitia beforward huwa sifanikiwi kwa sababu hawana room for negotiations na hawajibu maswali kama ambavyo mteja anastahili kujibiwa. Kwa mfano ubora wa gari au ikiwa limewahi kupata ajali etc wameshajijengea jina hivyo wana kibri na dharau kwa wateja. Ninaamini kabisa kuwa watu wanaonunua magari kupitia beforward are less informed.

Lakini tradecar view wana room for negotiations maana wao wanakuunganisha moja kwa moja na mteja anayeuza siyo wakala kama beforward. Mteja atakueleza abc's zote za gari na mtanegotiate bei. Na hata website ya tradecarview ina option ya kujua ikiwa gari iliwahi kupata ajali au la.

SBT, Beforward etc huwezi kuona option hiyo....unauziwa mbuzi kwenye gunia.....at your own risk
 
Back
Top Bottom