Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,311
5,466
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ya uongo na uzushi inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Robart Mushi maarufu kama Babu G. ambaye picha yake imeambatanishwa kwenye taarifa hizo kuwa alipotea tarehe 11 Aprili, 2024 na baadae kugundulika katika Chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road huku ikidaiwa Polisi kuhusika na kifo hicho kwa kumuua.

Ukweli ni kwamba tarehe 11 Aprili, 2024 majira ya saa 10 Alfajiri Askari Polisi wa Usalama barabarani alipewa taarifa na mwananchi kuwa eneo laTaa za kuongozea magari za Buguruni, Ilala mtu mmoja mwanaume aliyekuwa akivuka barabara eneo hilo la Kimboka kuelekea Chama aligongwa na gari ambalo halikusimama (hit and Run).

Mtu huyo alipata majeraha makubwa kichwani, kifuani na eneo la chini la mgongo na kisigino cha mguu wa kulia. Eneo hilo lina watu wengi ambao wanakesha kwa biashara mbalimbali na walishuhudia tukio hilo.

Mtu huyo alipelekwa haraka hospitali ya Amana na Polisi lakini baada ya kumfikisha Madaktari walibaini kuwa mtu huyo alikuwa tayari amekwishafariki, Kwa sababu chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Amana kilikuwa hakina nafasi, ilishauriwa akahifadhiwe kwenye Hospitali ya Jeshi la Polisi iliyo barabara ya Kilwa Temeke ambayo inatoa huduma hata kwa raia kuhusiana na suala hilo. Tarehe 21.4.2024 ndugu wa marehemu walipatikana na wakautambua mwili wa ndugu yao kwani hakuwa na kitambulisho wala simu. Taratibu za mwisho za mazishi zinafanywa ili akazikwe.

Kutokana na taharuki iliyotengenezwa na kujengwa kwa makusudi na mtu anayejiita Malisa gj na Bonoface Jacob ambao kwenye “post” zao walionesha nia ya wazi ya kutengeneza chuki dhidi ya Polisi na Serikali kwa wananchi kuwa mtu huyo aliyepata ajali alikuwa ameuawa na Polisi, Kitendo kilichofanywa na watu hao ni kosa kisheria na hakivumiliki na lazima Jeshi lichukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika ikiwa ni pamoja na kuwakamata, kuwahoji kwa kina na kuwafikisha mahakamani haraka iwezekanavyo.

Jeshi la Polisi halitavumilia watu ambao wanaibuka na taarifa za uongo na uzushi ambazo zinalenga kujenga chuki na taharuki kwa wananchi. Jeshi litaendelea kusimamia misingi ya kisheria na halitakuwa na huruma kwa mtuhumiwa yoyote wa kihalifu na litamshughulikia haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na ;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Pia soma:
-
Mauaji ya Robert Mushi ndugu wa aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob polisi wanahusika?

- Jeshi la Polisi lapekua nyumba ya Boniface Jacob, laenda na GJ Malisa Moshi kupekua nyumba yake

- Boniface Jackob afika kituo cha Polisi cha Oysterbay ili akamatwe kama alivyoagiza RPC

- Hatimaye Malissa na Boniface Jackob waachiwa kwa dhamana
 
Blah blah tu hii,Mr. Muliro unaweza pia ukaileta Doctor report kwa public kuhusiana na kifo hiki?,postmortem pathology report?,na pia mortuary ya kilwa rd (iliyochini ya police)na why sip ya muhimbili hospital?,ipo siku ukweli utakuja kusimama na kila mtu ana siku yake ya kuonana na maker wake,na hizi nyumba za ibada zinapokea watu makatili sana,wapi wale police wa awamu ya kwanza ya utawala?,vifo kama hivi havikusikika kabisa,kwangu mimi it's a NO kwa taarifa hii iliyojaa vitisho na sio ukweli
 
Muliro hajasema kama jeshi la polisi baada ya kupata taarifa ya marehemu kugongwa na gari, nao kufika kuuchukua mwili na kuupeleka mochwari, walitoa taarifa yoyote juu ya hilo tukio kwa umma?

Nijuavyo, kawaida kwenye matukio kama hayo, polisi huwa wana kawaida ya kutoa ripoti za kiusalama kwa raia, kama hilo tukio la ajali pia walitakiwa kutoa taarifa yake, lakini mbona wakanyamaza kimya mpaka ndugu wa marehemu wahangaike kwa siku kadhaa kumtafuta ndugu yao?

Jeshi la polisi ili lionekane linafanya kazi zake kwa weledi, kwanza lazima litoke kwenye hii mindset ya kutishana lihamie kwenye mindset ya kuelekezana, wawe wanajibu maswali ya msingi ili kuondoa sintofahamu zisizo na maana kwa raia wake, watengeneze mazingira ya kirafiki na jamii ili iwe rahisi kwao kupewa taarifa za kiusalama kila wakati.

Vinginevyo wataendelea kuonekana wababe waogopwe na raia, tuendelee kuishi kama paka na panya siku zote.
 
Blah blah tu hii,Mr. Muliro unaweza pia ukaileta Doctor report kwa public kuhusiana na kifo hiki?,postmortem pathology report?,na pia mortuary ya kilwa rd (iliyochini ya police)na why sip ya muhimbili hospital?,ipo siku ukweli utakuja kusimama na kila mtu ana siku yake ya kuonana na maker wake,na hizi nyumba za ibada zinapokea watu makatili sana,wapi wale police wa awamu ya kwanza ya utawala?,vifo kama hivi havikusikika kabisa,kwangu mimi it's a NO kwa taarifa hii iliyojaa vitisho na sio ukweli
hiyo wanaenda hata leo wanakamata daktari anaandika kwa kubackdate. cha kuwaambia tu ni kwamba amefariki, basi, mwogopeni Mungu ndiye aonaye sirini. na hakuna damu ya mtu huwa inaenda bure.
 
Blah blah tu hii,Mr. Muliro unaweza pia ukaileta Doctor report kwa public kuhusiana na kifo hiki?,postmortem pathology report?,na pia mortuary ya kilwa rd (iliyochini ya police)na why sip ya muhimbili hospital?,ipo siku ukweli utakuja kusimama na kila mtu ana siku yake ya kuonana na maker wake,na hizi nyumba za ibada zinapokea watu makatili sana,wapi wale police wa awamu ya kwanza ya utawala?,vifo kama hivi havikusikika kabisa,kwangu mimi it's a NO kwa taarifa hii iliyojaa vitisho na sio ukweli
Mungu atusaidie kwa kweli. Inatisha.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ya uongo na uzushi inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Robart Mushi ...
Uongouongo wa kipumbavu huu.Hivi huwa wakikaa na wake na familia zao ndiyo wanawasimuliaga upompompo kama huo?

Ujinga mtupu!
 
umefikiri kwa kutumia kariooo

atangazwe yeye ni nani
siku zote huwa kamanda anatoa taarifa mbalimbali za matukio mbona hili kaka kimya na Je iweje mtu atolewe amana apelekwe hospitali ya polisi yaan utoke ilala uende temeke wakati kuna Muhimbili?
na Pia kwa nini polisi kule.mochwari yao wanasema aliletwa na polisi akatelekezwa hapo! hili suala litamfukuzisha hapo!
 
Muliro hajasema kama jeshi la polisi baada ya kupata taarifa ya marehemu kugongwa na gari, nao kufika kuuchukua mwili na kuupeleka mochwari, walitoa taarifa yoyote juu ya hilo tukio kwa umma...
Ushawahi sikia siku polisi wanatangaza mtu kafa hana ndugu? Watu kibao wanakufa wanazikwa na halmashauri kimya kimya bila kelele
 
siku zote huwa kamanda anatoa taarifa mbalimbali za matukio mbona hili kaka kimya na Je iweje mtu atolewe amana apelekwe hospitali ya polisi yaan utoke ilala uende temeke wakati kuna Muhimbili?
na Pia kwa nini polisi kule.mochwari yao wanasema aliletwa na polisi akatelekezwa hapo! hili suala litamfukuzisha hapo!
taarifa ya kamanda imejitosheleza
 
Back
Top Bottom