Ijue siri kuu ya mahusiano katika Ulimwengu wa Roho

Mtoa mada mimi nipo hapa naanda script hapa ukitoa Uzi mimi nipo nyuma nakuja na summary lazima kieleweke njoo udondoshe madini hapa mzee baba
 
Hajaoa au kuolewa lakini mwili wake kiasili umeumbwa na matamanio soon baada ya kubalehe anaanza kupata hisia za kufanya mapenzi, dini inasema nini kuhusu hilo?
So anapaswa kufanya suppression ya hizo hisia akidhi matakwa ya dini ya kusubiri mpaka aoe au aolewe to which anabalehe akiwa 10s na ataoa au kuolewa kuanzia 20s mpaka 30s na wengine mpaka 40s.
Hebu nyie warohoni wasaidieni vijana sio kuwaita wazinzi sijui waasherati wakati wanatii hisia walizoumbiwa pasipo ridhaa yao.
Maana Kama vipi ili wasitende dhambi waondolewe hizo hisia na sio ku supress hisia kitu ambacho kimsingi kina madhara makubwa tu.
Waarabu kijana akibalehe mzazi humuoza despite anasoma au la ila sisi weusi na wazungu tunasubiri kwanza huku tunazo hisia tunazihifadhi kinafiki tunajiona tunasubiri wakati.

Ikiwa bikira Maria tunaambiwa alichumbiwa akiwa binti mdogo alikuwa bikra, Sasa huyu unaemuokokesha halafu anasuburi amalize University ndipo apatikane mchumba amuoe, hicho kipindi chote hisia zake za kimahaba anapeleka wapi mnadhani?

Halafu tendo moja mnalipea majina mabaya kibaooo kiasi kwamba mnalimalizia utamu na kuleta madhara kisaikolojia kila mtu akitafakari saa hiyo kichwa cha chini hakisomi namba balaa tupu.

Watu wa vitabu mje mseme hapa.
1. Kama kutenda kabla ni kosa kwanini hisia ziumbwe kabla ya hiyo ndoa?
2 kwanini hizo hisia hazikuumbwa baada ya ndoa ili ibalansi mahesabu?
3. Kwanini mnazuia watu wasifanye wakati hawana option na hizo hisia zao, yaani ana njaa mnamkataza kula msosi uko mbele yake dah!
4. Sex Kama other basic needs why inawekewa masharti Sana?
Warohoni hawana majibu ya maswali yako. Wakikujibu nitag
Ni maswali mepesi, nitakuja baadaye kukutoa upofu. Kwa sasa naandika mada.
 
Ukitaka kuchunguza maana ya kila neno, najua tofauti utaikuta tu na kufanana pia kupo.
Lakini uasherati na uzinzi, dhambi hizi zimekatazwa katika Amri ya ngapi?

Na Yesu alisema ukitamani tu hata kama hujamvulisha chupi, umekwisha kuzini.
Hapo utaona maana ya neno kuzini inazidi ku pana.
Nitarudi, usinitoe kwenye reli. Maswali mepesi hayo, unahitaji kueleweshwa
 
Yote tisa, kumi.. mie mkristo na naujua ukristo vizur.
Sijui anataka kutupiga kamba kupitia wapi.
I know many things about ulimwengu wa Roho..

Sasa sijui yeye anakuja na maelezo ya ulimwegu upi wa Roho.
Haya, mbona hujibu neno? Nimeandika tayari tangu asubuhi, naona kimya.
 
Utufundishe na jinsi ya kujitakasa pia naomba uandae topic ya hiyo kitu
Ndio tunaelekea huko
1. Maana ya ndoa
2. Kwa nini ndoa zinayumba
3. Kwa nini mabinti hawaolewi
4. Hatua za kuchukua kuweka sawa
5. Furaha ya kweli katika ndoa
 
Amani iwe nawe pia Mkuu.

Bandiko lako limejaa maarifa makubwa ambayo wengi wetu hatuna.

Tunaenda enda tu bila kujua, kumbe ni maagano tunaweka, kumbe tunaacha nafsi, kumbe ndo ndoa tayari.

Daaaah!!!
Ni kweli kabisa mkuu. Sehemu ya pili inafafanua kwa kina kabisa jambo hili. Ni vema kuelewa ukiwa ndani ya ndoa mafanikio yako yanakwenda sambamba na amani ya ndoa. Nje ya hapo labda kutumia nguvu za giza. Yote haya yanakuja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom