Ifike wakati shule zote za Secondary ziwekewe uzio

Witch hunter

JF-Expert Member
Nov 21, 2018
1,542
3,689
Hivi kwanza ni kwanini shule nyingi tena za serikali hazina uzio? Nyingine za wasichana na wanaishi hosteli, hivi kweli tangu uhuru mpaka sasa tumeshindwa tu kuweka uzio kwenye mashule yetu? Shule nyingine ziko katikati ya miji lakina hazina uzio.

Kuna shule moja hapa Arusha wananchi wanakatisha katikati ya shule ndipo njia ilipo. Hivi hapo mwanafunzi ataconcentrate na masomo kweli?

Vipi kuhusu nyakati za usiku? Hivi wanetu wanakuwa salama kweli? Hivi watu wote wanaopita hapo ni wema? Na ukizingatia umeme unakatika mda wowote, shule haina jenereta, hata umeme ukiwepo taa hazijasambazwa kwenye majengo yote.

QqHaya juzi kuna jamaa amekamatwa ndani ya bweni la wasichana. Na kesi iliisha kienyeji tu. Vipi kuhusu hili? Kwanini isiwe sheria kwamba hakuna shule mpya itafunguliwa bila kuwa na uzio? Duh!...

Vipi khali ya mashule huko uliko?
 
TUWAPELEKE FEZA SCHOOLS.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom