Huu ni msafara Wa viongozi au mazoezi ya Msafara?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,517
34,314
Mwaka 2021 nilishangaa Msafara Wa Waziri Mkuu ulivyokuwa haujapangiliwa vizuri na nikasema ule ulikuwa ni upotevu Wa Hela za umma.

- Ziara hii ya Waziri Mkuu mbona haina utulivu?

Leo Tena nimeshuhudia magari ya serikali yakiwa kwenye Msafara mji mdogo Wa Ifakara.

Magari hayo yalipofika kwenye Hoteli ya Mountain Peak ghafla Kwa Kasi ya ajabu yakageuza na kurudi yalikotoka.

Watu wamepigwa na butwaa imekuwaje gari la Polisi ililokuwa linaongoza msafara limeachwa nyuma na lile lenye milingoti ya bendera limetangulia mbele bila ya kusubiria magari mengine yaliyomo kwenye Msafara.

kimetokea Nini Msafara kuvurugika hivi, maana siyo kawaida.
 
Walikula mikumi??

Au walipitia Ilovo wakanywa chai yenye sukari nyingi.

Ila gari la kuongozwa kujiongoza lenyewe ni sawa kweli??

Ghafla linageuza na kuliacha gari la Polisi nyuma, siyo sawa.
Ndio maana nikasema wamevimbiwa mshikaki ya mbuzi,si mkuu wa msafara wala kiongozi mwenyewe.sasa wangebinuka mbele huko walikoelekea wangejiteteaje??
 
Gari za askari huwa mbele na nyuma kwenye msafara hivyo hata ukigeuka.hamna shida mbele kunakuwa na gari ya polisi na nyuma pia
Sasa Leo walipogeuza ghafla gari lenye milingoti ya bendera ndiyo lilikuwa linaongoza Msafara huku likipiga ving'ora!!
 
Mambo yao waachiwe wenyewe
Wanajiona special kwenye lindi la watu waskini.

Haiba na moyo wa uongozi hawana kabisa.
 
Mambo yao waachiwe wenyewe
Wanajiona special kwenye lindi la watu waskini.

Haiba na moyo wa uongozi hawana kabisa.
Labda wametoka Morogoro mjini kwenda Ifakara kufanya mazoezi ya Msafara maana wiki ijayo mwenge utakuwa huko.

Lakini kwa Nini gari la Polisi liachwe nyuma badala la lenyewe ndiyo kuongoza Msafara!!??
 
Labda wametoka Morogoro mjini kwenda Ifakara kufanya mazoezi ya Msafara maana wiki ijayo mwenge utakuwa huko.

Lakini kwa Nini gari la Polisi liachwe nyuma badala la lenyewe ndiyo kuongoza Msafara!!??
Ulikuwa Msafara wa kiongozi gani mkuu
 
Back
Top Bottom