Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,357
- 35,829
Kuna vitu ukiviona bado vinafanywa na viongozi wa kiafrika katika karne hii unabakia kucheka na kuwaza kuwa kumbe viongozi wa kiafrika bado wana akili za kitoto mnoo.
Moja ya vitu vya kipuuzi kabisa ni msururu wa msafara wa magari ya kifahari kwenye ziara za viongozi duni wa nchi za kiafrika (Tanzania ikiwa ni mfano mzuri). Mambo ambayo yalipaswa kufanywa karne iliyopita wakati watu wakiwa harusini, eti ndio trend fashion ya viongozi wa kiafrika wa sasa.
Mbwembe hizo na ufahari hazina faida yoyote, zinawaudhi mnoo raia wa kawaida wanaokuwa busy na maisha yao na wala hawana time na hizo takataka.
Misafara hiyo hufunga barabara kwa muda, huacha vumbi la hatari vijijini, hupelekea matukio ya ajali nk. Utasikia viongozi wakisema eti wako busy kwenda kusikiliza kero, kuzindua ujenzi wa vyoo vya shule vilivojengwa kwa pesa za misaada ya wazungu, kukagua mradi wa bomba la maji la kijiji, kukata utepe ili kuzindua kivuko cha miguu cha kijiji
Inatia kinyaa mnoo.