Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 6,564
- 13,778
Ukiwa alosto huna mia ya kutu wanakukwepa. Kipindi kile cha kujitafuta ukiwapiga kirungu cha buku ya nauli au bundle ili uweze kufanya mawasiliano wanakupa majibu ya kilokole.
Utasikia asiefanya kazi na asile. Au, wewe una mikono miwili na miguu miwili na macho mawili unaomba walemavu wafanyaje. Hapo umeomba haujamfosi. Na bado ataenda kukupiga majungu kwa ndugu wengine na pamoja watakuchukulia poa sana mixer dharau za wazi wazi. Utatumwa hadi mafuta ya kupikia dukani ili mradi wakuonyeshe wewe hauna maana sasa kwenye familia.
Unakubaliana na hali maana kama Yesu mwana wa MUNGU aliteswa na wanadamu sembuse mimi. Unapiga moyo konde unasema ngoja ufosi kupambana na mitaa na walimwengu kuliko kupambana na ndugu ambao wamekuonyesha kuwa kumbe si muda wote damu ni nzito kuliko maji.
Unaenda kwa wanao mtaani unawapa ya moyoni na kutubu sana. Wana wanaingia na huruma wanakushika mkono na hizo hizo buku buku za mawazo mixer kuingia madeni kwa niaba yako.
Unajikaza unaweka mitego sawa, uhakika wa elfu 10,30,50 80 na hata laki kwa wiki na mwezi unakuwepo. Unalipa madeni unajiimarisha kiuchumi. Muda wa shukrani nawatafuta wanangu maana siwezi watupa maana ndio walinishika mkono gizani. Tunakula kitimoto pamoja na hata kusaidiana shida ndogo ndogo bila husuda.
Ndugu wanaona post, simu zao zinapigwa wanasema unajiweka mbali na familia siku hizi. Umepata mafanikio unakula na marafiki siku ukianguka hao hawatakubeba wala kukuuguza ni sisi ndugu zako wa damu.
Hapo ndipo unajua si muda wote damu ni nzito kuliko maji. Unaamua kupiga kimya tu sms za kikuda kama hizo haujibu unaamua kuwa outcast maana sometimes familia ndizo chanzo cha watu kukosa uelekeo badala kuwa chanzo cha uelekeo.
Haya maisha haya.