Hebu tuone kwenye friji lako kuna nini!

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,745
4,277
Nimeenda kwa rafiki yangu nikafungua friji lake nikajionea maajabu ya dunia. Mambo ya aibu kwa mtoto wa kike.

Hata friji la nyumbani kwa mama huwa nahangaika sana kupanga, kutoa vitu visivyo muhimu. Unakuta mboga imebaki kidogo tu dada kwa uvivu anatia hotpot lote kwenye friji au hata sufuria.

Vitu vingine vinasahaulika humo hadi havifai tena.

Kinachonikera kuliko vyote ni kuweka mavituvitu bila kufunika. Friji linanukia ovyo ovyo.

Haya mimi naweka langu; sasa hivi ni high season flani so limenona kidogo(teh teh).

Naruhusu michango na marekebisho nitayafanyia kazi.

Naomba utuoneshe friji lako au hata utuambie lina nini hivi sasa?



20180727_180301.jpg
20180727_180320.jpg


=======

Hivyo, ili litimize matarajio hayo, hupaswi kuliacha kiholela bila kulipa utunzaji wa uhakika.

Njia sahihi za kulitunza zitasaidia kifaa hiki kufanya kazi bila matatizo na kwa muda mrefu. Tupate ujuzi kutoka kwa mtaalamu wa majokofu, Hafiz Ali, anayefanya shughuli zake jijini Dar es Salaam, ambaye anaanza kwa kusisitiza yafuatayo:

Usiligandamize ukutani
Jokufu linahitaji nafasi za kutolea hewa ili liweze kufanya kazi vizuri. Kama umeweka jokofu likakabanana na ukuta halitafanyakazi kikamilifu, ni lazima lifanye kazi ya ziada kuweka vyakula vyako baridi, ambapo halikutengenezwa kufanya kazi hiyo ya nyongeza. Wakati unapochagua mahali pa kuweka jokofu hakikisha angalau kuna nafasi ya wazi ya sentimita tano kila upande.

Hili ni la kuzingatia kama unaliweka kwenye jiko ambalo limejengewa eneo la kuweka jokofu. Kwa upande wa ndani hakikisha kuwa hauhifadhi vyakula kwa mtindo wa vitu vikubwa na vilivyoshikana bila kuachiana nafasi.

Safisha koili
Ni bahati mbaya kuwa pamoja na walio wengi kusafisha majokofu yao kwa ndani na milangoni, wengi wetu tunasahau nyuma ya jokofu. Ambapo ndiyo kuna zile koili zinazosaidia kufanya chakula kibaki na ubaridi. Hali hiyo inatokea kwa sababu koili hizi zinaondoa joto kutoka ndani ya jokofu na kwenye friza. Kutegemea na muundo wa jokofu zipo koili zilizo nyuma au chini na ni rahisi vumbi, buibui na chembechembe nyingine za taka kujishika humo baada ya muda.

Uchafu huu unasababisha jokofu kuongeza msukomo wa kazi na kusababisha kuchoka hivyo kuhitaji matengenezo ya gharama kubwa. Kusafisha koili za nje ya jokofu ni kazi rahisi ya utunzaji wake ambayo unaweza kuifanya mwenyewe.

Zima jokofu, livute mbali na ukuta na tumia ufagilio wenye brashi laini kusafisha mavumbi yote hata kama yatadondoka sakafuni utasafisha sakafu baadaye. Fanya hivi kila baada ya miezi sita ili lifanye kazi vizuri.

Mipira milangoni ibanane
Ili jokofu liweze kufanya kazi kikamilifu na pia lisiongeze gharama za umeme, milango yake inatakiwa iwe inabana ipasavyo. Milangoni mwa jokofu kuna mpira ambayo inakuwa dhaifu baada ya muda. Inapotokea hivyo hewa ya nje yenye joto inapenya na kuingia ndani ya jokofu na kulisababishia kufanya kazi ya ziada kuondoa joto hilo linalozidi.

Kama joto linaongezeka inamaanisha gharama kubwa zaidi za umeme na pia jokofu kuchakaa mapema. Kusaidia mipira ya milangoni idumu, uwe unaisafisha baada ya kipindi kwa sabuni na maji.

Kama unahisi imeanza kuchoka fanya jaribio jepesi la kufungua mlango uufikishe nusu halafu uachie polepole ujifunge wenzewe. Kama haubani vizuri fahamu mpira umeanza kuchoka. Habari njema ni kwamba mipira ya spea ipo na si bei kubwa vilevile kuibandika upya ni rahisi pia.

Liyeyushe barafu baada ya kipindi
Kama jokofu lako ni moja ya matoleo mapya utakuwa una bahati kwamba halijengi barafu ndani (non frost) na huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu dondoo hii ya utunzaji. Ila kama ni la zamani kidogo, bila shaka unasumbuliwa na tatizo la barafu kuganda ndani ya chumba cha friza.

Barafu zinazojitenga katika koili zilizo ndani ya jokofu zinalilazimisha kufanya kazi ya nyongeza ili kubaki katika ubaridi unaotakiwa.

Barafu inapojijenga hadi inchi 1.5 (sentimita moja) ni wakati wa kuyeyusha jokofu. Zima umeme, ondoa vyakula vyote, acha milango wazi ili iyeyuke. Endapo hujalitoa nje unaweza kubeba mabonge ya barafu kadiri yanavyojiachia na kuyaweka kwenye chombo ili kuepuka maji mengi kujaa ndani yatakapoyeyuka.

Mara barafu yote inapoyeyka, mwaga na kausha mashelfu yaliyojikusanya maji, washa jokofu na rudishia vyakula ndani.

Michango ya wadau

-----
Here we go, as promised!

Looks like it’s time to replenish....

View attachment 820782View attachment 820783View attachment 820784
----
----
 
Back
Top Bottom