Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislamu wenyewe kwa Tanzania...

Status
Not open for further replies.
Mleta mada amegusia matatizo yanayoukabili uislamu,wakristu wanaitwa makafir ila wao hawajawahi kuwaita waislamu jina lolote,wachungaji, mapadre na maaskofu wana kiwango bora cha elimu na hivyo wanahubiri upendo,amani na mshikamano,tofauti na wenzetu wanaohubiri sisa za chuki na umwagaji damu.TUACHE CHUKI,TUJADILI MATATIZO YETU NA CHANGAMOTO ZETU KAMA TAIFA.HONGERA SANA MLETA MADA.
 
hoja Yako MM ni nzuri kwa sababu imejaribu kueleza hali halisi na kushauri.
mimi pia napendekeza kuwa wale tunaoelewa tukatae kudanganywa na wachache wasiolewa. kwa sasa wote wakristo na waislamu na wengine wote inafaa tujichanganye pamoja. tutafute elimu popote. tufanye kazi kwa bidii. tutumie fursa zilizopo kujiendeleza. imani tusiache lakini tujue pia kwamba kuishi hapa duniani viizuri ni lazima tuwe na elimu dunia. Ni lazima ujue mambo ya msingi kuhusu duna, viumbe, na uhai. kwa ujumla ni vipi tutatumia mazingira tuliyonayo kuendelea. hii ni akili ambayo tuinapata darasani na katika kuishi. ikiwa tutajali zaidi imani na kudharau elimu dunia basi tusilalamike kuwa tunaonewa maana shida ni nini si mbingu inatusubiri? kwa sababu hao tunaosema wanatuonea hawajatuzuia kwenda mbinguni. maana malalamiko yetu ni ya kidunia zaidi yaani "wana vyeo sisi hatuna ; wana utajiri sisi hatuna ..." je, hayo si ya dunia? wengine wanakwenda mbali na kuwaambia vijana wajifunge mabomu wakaue nao wafe na mbingu wataiona haphapo! hii imani jamani!
haya, kuna suala la mahakama ya kadhi. wengine wanafuata mkumbo tu japo wanajua lakini hawatazami undani wake. wengine haohao kia siku wako guest house siku mahakama ya kadhi ikifanya kazi ilivo wataanza kulalama haki za binadamu. sheria za torati ni kali. hivyo vimodo na vimini vyenu mnavyovaa huku mnajifanya mnaonewa sheria mtaziona. Narudia tena tujichangaye tuishi kama binadamu na watanzania na dini zetu zibaki mioyoni mwetu na katika familia zetu. tukimwona mtu njiani tumwone ni binadamu ni mtanzania anaweza kuwa dini yoyote basi na tuvumiliane.
 
Chama you are always negative sijui kwanini maana nimekua nikifuatilia comments zako mpaka huwa nashangaa Kiwango cha elimu/uelewa na cha ajabu bado kuna baadhi ya wenye upeo kama wako wamekuunga Mkono.

Na kama kweli uko geniune weka majina yako halisi hahaha


founder and CEO of www.oric.co.tz and www.aio.co.tz skype: alfred.kohi, 0784800989, 0715800989/0715800989

Mkuu wala usihangaike sana Mungu kanijalia kisomo kwa kiwango changu; mfumo mzima tulionao Tanzania huitaji Ph.d kuelewa; badala ya kuja na majibu muafaka umekimbilia kutaka kujua kiwango changu cha elimu hii inaonyesha jinsi ulivyoguswa na mada lakini huna majibu yakinifu; ila tu nikufahamishe nimesoma kwenye mfumo wenye kueleweka sio huu wa shule za kata. Umekimbilia kudai nipo always ngative hii unaonyesha ni kiasi ulivyo muoga wa kujadili mada; lengo kuu la majadiliano sio kulumbana ni kuelimishana; kama una majibu muafaka njoo vinginevyo ni ubabaishaji tu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kiukweli huu ndo ukweli japo kuna watu wenye sababu zao ukweli huu kwao hauonekani, nakupongeza sana ndg yangu Mohammed, umeeleza kwa lugha rahisi na umeeleweka sana, nataka kusema kitu hapa.

Kwa kutumia vigezo vyovyote vile ili kujua idadi ya waislamu na wakristo hapa Tanzania lazima jibu litakuwa wakristo ni wengi kuliko waislamu, miaka yote hata kabla ya uhuru tumeishi pamoja kwa upendo na amani na kama elimu kweli ndo msingi wa mafanikio basi wakristo kwakuwa ni wengi kwa idadi na walijenga shule zao nyingi basi ni dhahiri walio wengi wamefanikiwa zaidi kielimu, sasa tofauti hii ya mafanikio katika elimu kwa maoni yangu nayo ni sababu inayowafanya waislamu waonekane wanyonge, kuhisi walionewa na wanazidi kuonewa, lakini kiukweli alichokisema MOHAMMED hapo juu ndo ufumbuzi wenyewe, waislamu muache kulalama na kujiona wanyonge kila wakati,nyie ni watu mnaomjua Mungu!

Leo hii iko wazi kabisa kwamba "ADUI WA WAKRISTO NI SHETANI LAKINI ADUI WA WAISLAMU NI UKRISTO" Hii hapana ndg zangu hebu tuwe na subira, kuna mambo yalivyo sasa kama ingekuwa ni nyie sijui ingekuwaje hebu fikiria kama ingekuwa Rais ni mkristo, makamu wa rais ni mkristo, mkuu wa polisi ni mkristo,Jaji mkuu ni mkristo,mkuu wa usalama mkristo....kutaja wachache tu hao, je hali ingekuwaje? Wakristo muda wote wamekuwa watulivu!

Hebu tusidanganyike tuishi kama zamani changamoto za maisha tuzijadili pamoja kwa hali ya amani na utulivu! Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Hadi sasa toka CCM waanze kupandikiza mbegu za udini kwa maslahi yao binafsi, jumla ya makanisa 57 yamechomwa au kuhujumiwa hadi sasa.Idadi inaweza kuongezeka kutokana na mtazamo hasi. Wakristo hawajalalamika hadharani. Wameandika barua kadhaa kwa rais, waziri mkuu,polisi, waziri mambo ya ndani kwa serikali zote (Bara na Visiwani)HADI SASA, hakuna majibu. nao wanajiulizas labda kwa sababu Rais, Makamu wake, jaji mkuu, mkurugenzi usalama wa taifa, mkuu wa polisi ni WAISLAMU. Nadhani wameamua kuaacha waislamu waunyanyase ukristo. Kuna agenda ya siri ndani yake.

Kama uislam hauwakilishwi na wavunja na wachoma makanisa, kwanini waislam waliosafi na waislam wa kweli hawaandamani kupinga uhuni unaouchafua uislam?
 
Sasa Ritz mbona unafanya vurugu zisizo na maana yoyote. Hiyo mikeka ya sheikh Mohamed Said tena font size ndogo kiasi hicho nani anaweza kuisoma? Jenga hoja vizuri bila kujitia upofu na kuukimbia ukweli.

Kama utakuwa umemsoma na kumuelwa Mkandara basi utaacha ubishi usio na tija. Amesema kitu cha msingi sana, inakuwaje mnamuona sheikh amir kuwa shujaa wenu wa waislamu huku mkimtaja Nyerere kuwa adui yenu namba moja lakini hamuwataji waislamu wenzenu akina mwapachu, sykes, na wengine wengi unaowafahamu ambao walikuwa bega kwa bega na Nyerere?
 
Last edited by a moderator:
natamani kucheka ila ina sikitisha kwa kweli. siamini kuwa muisilamu mwenye kutambua kuwa "hawata kuwieni radhi mayahudi na manaswara mpaka mfuate mila zao' ata toa hoja kama hii. nina maana gani? tumeona migogoromingi ikihusishwa na waisilamu kulalamika kuwa wanaonewa. hivi kwa dunia hii ya sayansi bahati nziri mimi nimesoma sayansi mpaka sasa niko chuo. tatizo liukitokea huwa tuna tafuta ufumbuzi kisayansi. kama kweli tunataka suluhisho la kudumu kwanini sasa serikali isiite hao viongozi wakiisilamu wenye kulalamika juu ya swala hili na kukaa nao mezani watoe hoja zenyemashiko na ushahidi wa kisayansi alafu yawekwe wazi tujue wanacho dai ni kweli au si kweli kwa ushahidi. venginevyo, kuna ksemo unasema ukifuata njia iliyo andikwa potelea mbali utafika kwenye kijiji kinachoitwa laiti ningelijua na wakazi wake wanaitwa ole wako wewe uliofika hapa.
sio rahisi kwa sababu wanaolalama wanafanya hivo kwa kuammini zaidi. imani kwa imani sayansi kwa sayansi
 
Nafikiri kwa hili, Riz itabidi ameze machungu tu na maumivu.

Hata Sheich anasema "Hata ukikasirika, vumilia maana ndiyo haki ilivyo. Inachomachoma......"

Anzia: 7:30 upate ukweli wako


Ritz je Unajua ya kwamba Sheikh Hassan bin Amir aliunda chama cha Upinzani kikiitwa All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT) baada ya kujitoa TANU na wenzake, hivyo kuendeleza propaganda zake za kisiasa kwa kutumia imani ya dini?. Hivi ulitegemea huyu Hassan angesema nini dhidi ya Nyerere ambaye sio tu TANU kilikuwa na wanachama waislaam wengi bali pia kulikuwa na viongozi wa Kiislaam miaka hiyo hiyo.

Na ukumbuke huyu Hassan kaandika yote haya kabla ya Azimio la Arusha akizungumzia serikali ya Mkoloni na hata baada ya Uhuru tukitumia bado mfumo wa Mkoloni, hivyo kwake yeye hakuwa na karata ya ushindani isipokuwa kutumia dini dhidi ya uchaguzi wa Nyerere. Na maajabu ya Mussa alipokamatwa kwa uchochezi kama huu wewe bado unamuona yeye kuwa mkombozi ilihali Nyerere hakuchaguliwa na Wakristu bali waislaam wenyewe kina Abdulwahid, Mwapachu na wengine wengi ambao hadi leo mnawapongeza kama waasisi wa Uhuru wetu..

Unajua kuna wakati nashindwa kabisa kuwaelewa Wadanganyika. Unapompongea Sheikh Hassan ambaye alipingana na kina AbdulWahid Sykes lakini waote mnawpa sifa sawa.. Mmesimama upande gani? kama mnamsifia Sheikh Hassan bin Amir mnatakiwa kuwalaani kina Sykes lakini maajabu kila napowasoma wadanganyika kusema kweli huwa nashindwa kuwaelewa mmesimama wapi isipokuwa hizi chuki za Udini zilizopandikizwa lakini watu wanaamini ni makosa ya Waislaam au wakristu na mko radhi kabisa kutetea upande wenu, wengine ndio wenye makosa..
 
Last edited by a moderator:
Sasa Ritz mbona unafanya vurugu zisizo na maana yoyote. Hiyo mikeka ya sheikh Mohamed Said tena font size ndogo kiasi hicho nani anaweza kuisoma? Jenga hoja vizuri bila kujitia upofu na kuukimbia ukweli.

Kama utakuwa umemsoma na kumuelwa Mkandara basi utaacha ubishi usio na tija. Amesema kitu cha msingi sana, inakuwaje mnamuona sheikh amir kuwa shujaa wenu wa waislamu huku mkimtaja Nyerere kuwa adui yenu namba moja lakini hamuwataji waislamu wenzenu akina mwapachu, sykes, na wengine wengi unaowafahamu ambao walikuwa bega kwa bega na Nyerere?
pia akumbuke Mwalimu alipokuwa Bagamoyo na Shikh Ramia na wazee wengine wa kiislamu tena kafunga! mwalimu akaomba aspirini maana kichwa kilikuwa kianauma. Sheikh akamwabia subiri, baada ya kula Ramia akamuuliza, "bado kichwa kinauma?' akachinjwa mnyama ... mwalimu akaambiwa "tambuka " akatambuka. mwalimu hakuwa adui wa waislamu maana alipotaifisha mashule hata ya wakristo alitaka waislamu pia wasome kwenye hizo shule mfano forodhani hapahapa Dar. Acheni kumwonea marehamu!
 
Pole sana kwanza umeuliza elimu ya Mtoi sijui ni kwanini? kwangu ni bahati mbaya tu kuwa hujamuelewa kabisa Mohamed Mtoi na hoja yake...ukweli anazungumia watu kama wewe wanaochangia kudidimia kwa waisilimu kwa kushughulikia mambo yasiohusiana na changamoto zinazowakabili....sina hakika sana kama umeelimika ila nina hakika umeona kuta za darasa. Nakuomba utufahamishe kwa uelewa wako ni namna gani waisilamu wameathirika na mfumo ullipo sasa ili tuweze kujadili kama watu walioelimika kidogo.

Huewezi kuelewa kwa nini nimuliza kiwango chake; na kama umenisoma vizuri nimeweka wazi yapo matatizo yamechangiwa na waislamu na yapo kwa kiwango kikubwa yamechangiwa na mfumo mzima wa serikali; tatizo lipo na si lakufumbiwa macho wewe kama hulioni huo ni mtazamo wako; hapa siongelei kwa misingi ya udini ila ni matatizo yanaweza kutokea siku za mbeleni yataharisha amani ya nchi yetu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Umenichekesha nina coaligue mpya alinipa stori yake na nssf. Anaitwa jina la kiislamu. Sasa akaajiriwa harakaharaka. Baada ya mwaka wakagundua sio muislamu, akahamishiwa mtwara akiwa na ujauzito wa miezi 5. Akagoma kuondoka. Akatafuta kazi akaondoka baada ya kukaa mtwara 3 months.Sasa baba unataka tuanze kufanya interview kwa dini? Umeniacha solemba.

Red: Usikute Mwislam alifaulu baba akaona atachelewa kupata mahari akagoma mtoto kwenda shule wajanja wakachangamkia post. usikute baba ni mmoja wa wanaharakati wa kupinga mfumo kristo
 
nimependa jinsi ulivyoelimisha naomba isomwe na waislam wengi kwa manufaa ya imani zetu na inchi kwa ujumla
 
Nadhani hujamuelewa Mtoi; amedai haoni tatizo liliopo liwe ni mfumo kristo kama unavyodaiwa au mfumo wa ukandamizaji; cha kushangaza amekuja mawazo ya kurekebisha mfumo ambao hauna tatizo; yeye haoni tatizo la mfumo mzima kwa sababu lengo lake kuu ni kutaka kuishutumu CCM; ushauri ni serikali kuvunja MoU na taasisi zote za kidini hapo ni pa kuanzia tu.

Chama
Gongo la mboto DSM

Hivi unafahamu maana ya MOU?? Na unajua impact ya serikali kuvunja mou as u wish? una uhakika kwamba ukivunjwa ndo waislam mtapata manufaa kielimu kiafya etc? Tell me how.
 
Mkuu naomba kaelimu kidogo hapo maana huwa nasoma mara nyingi inaandikwa Mou ila sijui ni nini na inahusu nini,inamfaidisha nani kwa namna gani ?

Mkuu kwa ufupi MoU ni kama maelewano/makubaliano kati ya serikali na taasisi mbalimbali; katika makubaliano hayo serikali inatenga mamilioni ya pesa na kuzipa taasisi za kidini kuendesha shughuli mbalmbali kwa lengo la kutoa huduma za kijamii

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Lol!!!Thats ma'school mate Mohamed Mtoi kaka nimekukubali vilivyo sana tu aisee hii nyuzi yako imetulia sana kaka huna budi kuwa kiongozi tena utookee kwenye chama cha siasa chenye akili na si vinginevyo nimekukubali sana kama ni kura yangu utapata pale ukiomba uongozi popote pale hata isiwe kwa vyama vya siasa,nimeichambua hii issue y right kaka naomba uiweke kwa kumbukumbu i mean weka kopy yake kwa libraly yako hapo kwako kwa vizazi vijavyo,ushafahamu sie waafrika hatuna utamaduni wa kuhifadhi mambo yetu ndio maana huwaga tunakuwa wasahaulifu wa mambo ya msingi na hii ndio inatufanya tuweze kurubuniwa na watu ambao hawatupendei tuishi vyema kwa kutaka kuwa madarakani na kushibisha familia zao na matumbo yao.
Kaka be blessed,wewe ni kiongozi
 
Mkuu kwa ufupi MoU ni kama maelewano/makubaliano kati ya serikali na taasisi mbalimbali; katika makubaliano hayo serikali inatenga mamilioni ya pesa na kuzipa taasisi za kidini kuendesha shughuli mbalmbali kwa lengo la kutoa huduma za kijamii

Chama
Gongo la mboto DSM

Kumbe hata hujui maana ya Mou.
 
Hili ndio tatizo kubwa linalotukabili wengi wetu, badala ya kujadili mada husika unaleta siasa kwenye suala la dini, hakuna mahali popote Mohamed mtoi amezungumzia chadema, kwa jinsi ulivyochangia mada hii ni dhahir kwamba huwezi kumkaribia Mr.Mtoi kwa namna yoyote ile kwenye kiwango cha kuchambua mambo na kujenga hoja yenye mashiko. Nashangaa sana unapoamua kutilia shaka kiwango cha elimu cha Mohamed Mtoi.

Kwa nini ulete lugha ya kashfa kwenye mjadala ambao mpaka nilipofika kwenye post yako ulikuwa ukienda vizuri tu, unaposema kiwango cha muuza kahawa una maana gani? kwamba wauza kahawa hawana uwezo wa kufikiri? au hawana akili?

Mimi naona kama unaleta ushabiki usio na maana wala tija, kubali kubadilika usadie kujenga Confidence, Competence na Commitment kwenye uislamu ambao naamini ni dini nzuri tu. hamaki na kejeli hazisaidii chochote hapa zaidi ya kushangaza wote watakaosoma post yako.

Tafakari.... unless wewe ni mmoja wa wanaotumiwa na wachache kwa maslahi binafsi.

Soma kwenye article ya mtoi kipengele #3 & 4 lengo lake hasa ni kutaka kuipaka matope CCM tatizo la mfumo uliopo ni la kurithi tangu serikali ya kikoloni na yamekuwa yakiendelezwa siku hadi siku; hakuna wa kunitumia sina shida ya maisha kidogo nilichonacho namshukuru Mungu; nimeongea kwa mtazamo huru; kama kuna kitu hukubaliani nacho njoo mjadala tutaelemishana kadri ya uwezo wetu; lengo ni kuhahkisha Tanzania hatuingii kwenye mtego wa wavaa mabomu tunataka amani ya kudumu. Usiogope kuulizana viwango ni kawaida kwa wajadili mada.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Soma kwenye article ya mtoi kipengele #3 & 4 lengo lake hasa ni kutaka kuipaka matope CCM tatizo la mfumo uliopo ni la kurithi tangu serikali ya kikoloni na yamekuwa yakiendelezwa siku hadi siku; hakuna wa kunitumia sina shida ya maisha kidogo nilichonacho namshukuru Mungu; nimeongea kwa mtazamo huru; kama kuna kitu hukubaliani nacho njoo mjadala tutaelemishana kadri ya uwezo wetu; lengo ni kuhahkisha Tanzania hatuingii kwenye mtego wa wavaa mabomu tunataka amani ya kudumu.

Chama
Gongo la mboto DSM

Sasa Kama una tambua ni MFUMO tangu ukoloni, tufanyejje ili tuondokane nao??? Maana HAtuna uwezo wa kuifuta hii historia!!!!! Very unfortunate
 
shark nakushukuru sana kwa analytical thinking uliofanya na kueleza.mimi ni mkristo lakini wakati nafanya thesis yangu nilisimamiwa na dr muisilamu he my friend mambo ulioyaraise exactly right after my thesis discussion ndio tulikuwa tunadisscuss kwa kweli hata mimi nilisoma na watoto wengi sana wa kiislam lakini kadri nilivyo kuwa naenda mbele wnapungua kwa kasi ya ajabu sana ukienda majera makonda mateja na kazi mbali mbali za hali ya chini you find them wengi tu i think is better for the moslem community in my country to change the way currentry they do pursue their way of living hii itasaidia sana hata haya mamigomo yanayoendelea is simply because people have no alternative to do so any person can just simply wachochea watu wakafanya matukio yanayoendelea sasa hivi inchini sisi sote ni ndugu dini zisitutenganishe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom