Watanzania wengi hawapo Flexible, Wengi ni Conservative na hapo ndipo CCM inaposhindia.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,552
52,226
Kwema Wakuu!

Watanzania waliowengi ni Conservative(Watu ambao ni wagumu kubadilika au wanachukia au kuogopa mabadiliko)…

Sio ajabu mtu ni muislam au mkristo kwa sababu alizaliwa na kukulia kwenye Ukristo. Sio ajabu mtu ni Simba au Yanga kwa sababu alipokulia ni Washabiki wa Simba na Yanga.

Katika siasa, tabia hii ni mtaji na tegemeo kubwa kwa chama kama CCM. Moja ya mambo ambayo CCM inajiamini nalo ni hilo la watanzania kutokuwa Flexible au kuwa conservative.

Sio ajabu mpaka leo kuna Watu wanahangaika na kumtajataja JPM. Wapo wengine wanamtajataja Nyerere. Wao kila kitu kwao ni Nyerere au JPM. Hiyo ni ishara ya mtu kutokuwa Flexible au kuwa conservative.

Ni sawa na wale Walokole au Wasabato au waislam wao kila kitu lazima warejelee Watu wa zamani waliokufa miaka zaidi ya elfu elfu huko. Yesu anasema, Mara Mtume anasema. Ukimuuliza wewe kwaakili yako unasema nini anawasha macho.

Dunia haihitaji kuongozwa na Watu wasiotaka mabadiliko, Watu wanaochukia mambo mapya. Watu wasio wabunifu.

Wananchi wengi hawaoni chama kingine zaidi ya CCM, hata hao wapinzani waliowengi ni kama CCM tuu sio ajabu ukasikia mpinzañî akiiñgia CCM.

CCM wanaamini bila wao nchi hii haiwezi kuongozwa na kuletwa maendeleo. Huo ndio u-conservative wenyewe huo.
Ni kama Watu wa dini wanaoamini kuwa dini yao ndio itawapeleka mbinguni na dini zingine mbingu hawaendi. Ni dalili ya kutokufikiri vizuri. Kuifunga akili katika vikao.

Usitegemee maendeleo yoyote ya maana kwenye jamii yenye Watu wengi ambao wapo conservative au ambao hawapo flexible.

Mimi nimemaliza, leo sihitaji maswali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama
 
Umeongea ukweli mleta mada.watanzania wana allergy na vipya ndio maana mpaka leo vyakula vyetu vikuu ni wali, ugali kidogo na chipsi ukila tofauti na hivyo unaonekana wa ajabu.
 
Kwa tume hii ya uchaguzi na katiba hii, lazima hilo liwe hitimisho lako. Lakini tume ikiwa huru na katiba bora, utaona ukweli ambao huwezi kuuona katika mazingira haya.
 
Umeongea ukweli mleta mada.watanzania wana allergy na vipya ndio maana mpaka vyakula vyetu vikuu mpaka leo ni wali, ugali kidogo na chipsi ukila tofauti na hivyo unaonekana wa ajabu.

Na wanaunda na propaganda kabisa îli kujifungia kwenye Boksi
 
Si Kweli,

Watanzania ni flexible,

Ndio maana Mrema alimshinda Mkapa kwenye Sanduku la kura,

Tuache wizi wa kura ndio ujue flexibility au static ya Watanzania ilipo.
 
Somesheni kizazi hiki tunachokifyatua sasa , acheni kulaumu kizazi ambacho hakijasoma hata hivyo kimejitahidi
 
Yaani kuikataa ccm ndiyo flexibility!?..Sasa uiondoe ccm umpe nani nchi!?..Tanzania ndiyo sehemu inayoshangaza wageni wengi wafanyabiashara,bidhaa mpya inaingia sokoni na inauzika fresh tu,huko unakowaona wako flexible bidhaa mpaka iaminiwe inunuliwe ni miaka na baada ya promotion ya kutosha
 
Kuku wa kizungu wamempiga propaganda weee! Cha ajabu ukiwakuta kwenye vibanda vya chipsi wanavyowatafuna mpaka unashangaa!

Wengine wanakwambia mayai ya kuku wa kizungu yana madhara cha ajabu wanayala miaka na miaka na madhara hatujawahi kuyaona

😀😀
Alafu unakuta anayetoa maelezo hana hata uelewa wowote na mambo ya utabibu ila umkute akieleza utachoka
 
Kwema Wakuu!

Watanzania waliowengi ni Conservative(Watu ambao ni wagumu kubadilika au wanachukia au kuogopa mabadiliko)…

Sio ajabu mtu ni muislam au mkristo kwa sababu alizaliwa na kukulia kwenye Ukristo. Sio ajabu mtu ni Simba au Yanga kwa sababu alipokulia ni Washabiki wa Simba na Yanga.

Katika siasa, tabia hii ni mtaji na tegemeo kubwa kwa chama kama CCM. Moja ya mambo ambayo CCM inajiamini nalo ni hilo la watanzania kutokuwa Flexible au kuwa conservative.

Sio ajabu mpaka leo kuna Watu wanahangaika na kumtajataja JPM. Wapo wengine wanamtajataja Nyerere. Wao kila kitu kwao ni Nyerere au JPM. Hiyo ni ishara ya mtu kutokuwa Flexible au kuwa conservative.

Ni sawa na wale Walokole au Wasabato au waislam wao kila kitu lazima warejelee Watu wa zamani waliokufa miaka zaidi ya elfu elfu huko. Yesu anasema, Mara Mtume anasema. Ukimuuliza wewe kwaakili yako unasema nini anawasha macho.

Dunia haihitaji kuongozwa na Watu wasiotaka mabadiliko, Watu wanaochukia mambo mapya. Watu wasio wabunifu.

Wananchi wengi hawaoni chama kingine zaidi ya CCM, hata hao wapinzani waliowengi ni kama CCM tuu sio ajabu ukasikia mpinzañî akiiñgia CCM.

CCM wanaamini bila wao nchi hii haiwezi kuongozwa na kuletwa maendeleo. Huo ndio u-conservative wenyewe huo.
Ni kama Watu wa dini wanaoamini kuwa dini yao ndio itawapeleka mbinguni na dini zingine mbingu hawaendi. Ni dalili ya kutokufikiri vizuri. Kuifunga akili katika vikao.

Usitegemee maendeleo yoyote ya maana kwenye jamii yenye Watu wengi ambao wapo conservative au ambao hawapo flexible.

Mimi nimemaliza, leo sihitaji maswali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama
Kama wewe ni mwanaume bila shaka hadi sasa umeshapata mume. Si uko flexible? Ndio...
 
Back
Top Bottom