Happy birthday Innocent Bashungwa, kwanini baadhi ya viongozi hutenguliwa ghafla!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,789
21,220
Bwana Inno alivyokataa Bilioni 5 za Hayati kwenye miaka ya 2018
Alitokea mfanyabiashara mmoja alimfuata Bwana Inno ofisini pale Wizara ya Biashara, na alifika pale akaanza kumshawishi ili amkubalie ombi lake la kwenda kumuombea kibali cha kuagiza sukari kutoka nje kwa sababu wakati huo SHUGA ilikua imeadimika.

Yule Mfanyabiashara alimfuata Bwana Inno kwa sababu moja wakati ule alikuwa mtu anayeaminika na kukubalika sana kwa Hayati, kwa sababu nyingi nitazisema anather day.

Basi yule Mfanyabiashara kwa nia ya kumshawishi Bwana Inno alienda na kiasi kikubwa cha hela katika mfumo wa USD ambayo thamani ilikua kama Bilioni 5 kasoro ilikuwa cash, Ili kumshawishi Bwana Inno akubali aende akamuombee kibali cha kuingiza hiyo sukari kwa Hayati.

Wakati wa kikao chao yule mfanyabiashara hakua maneno mengi, alimwambia "Mhe. Bwana Inno wewe ndiyo wetu wafanyabiashara ebu nipambanie nipate kibali cha kuleta sukari, mzigo wako huo hapo" akatoa hizo USD zenye thamani ya Tsh. Bil 5 kasoro.

BWANA INNO bila kupepesa macho alimwambia yule mfanyabiashara "Mzee wangu najua una hela, unadhani hii Pesa unayonipa maanake mimi naenda kumuaminisha Mkuu (Hayati) kwamba wewe uko sawa, wakati najua ukishaleta bidhaa hii adimu utawatesa Watanzania kwa sababu utauza kwa bei juu, Mimi kama Waziri kwanza sifanyi huo ujinga, na nitaenda kwa Hayati kumwambia asikupe kabisa kibali kwa sababu wewe ni mtu wa rushwa.

"Hayo ndiyo yalikua majibu ya BWANA INNO kwa huyo Mfanyabiashara, alikataa rushwa ya Bilioni 5 kwa sababu ya uzalendo wake kwa Taifa lake na Serikali yake. Baada ya kukataa ile Bil 5, hapohapo analetewa Simu na msaidizi wake kuwa (Hayati) anampigia inabidi aongee naye ile anapokea simu kauli ya kwanza ya Hayati "INNO HONGERA SANA WEWE NI MZALENDO WAKWELI".

Bwana Inno akamuuliza Hayati hongera yanini akamwambia najua kinachoendelea muda huu, kumbe Hayati ndiyo alisuka ule mchongo alikua anapima Uzalendo wa Mawaziri wake, hasa kupitia KIBUNDA na moja ya Mawaziri ambao walifaulu alikua Bwana Inno.

Na moja ya maneno ambayo Hayati alishawahi kumwambia MAZA, katika Mawaziri wangu huyu KIJANA namuamini sana, ikitokea unataka kufanya kazi na vijana huyu usimsahau. Basi kuanzia 2018 hadi sasa BWANA INNO ndiye Waziri anayeongoza kuongoza Wizara nyingi zaidi kuliko wote walioko kwenye Baraza la sasa hivi la MAMA. Nimeandika hivi kwa sababu leo NI SIKU YA KUZALIWA YA BWANA INNO, shujaa aliyekwepa mtego wa kukataa Bilioni 5.

HAPPY BIRTHDAY INNONB: WAPO MAWAZIRI AMBAO WALIUIGIA HUU MTEGO NA WALICHOMOLEWA, GHAFLA.

GM1JX_qXMAA4aXH.jpeg
 
Kama ni kweli basi hongera kwake, nimekuwa nikijiuliza sababu ya yeye kupanda vyeo harakaharaka sikuwa nikiijua.

Ila katika mambo huwa ananishangaza ni muonekano wake ambao ni tofauti na umri wake, anaonekana mdogo sana ingali ana umri mkubwa!
 
Back
Top Bottom