Hakuna faida ya kumpeleka mtoto English Medium (mabasi ya njano)

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,388
13,140
Kuna huu mkumbo tulionao watu weusi wa kuigana igana mambo hata yasiyo na maana.

Hapa nitazungumzia huu mtindo walionao wazazi wengi kupeleka watoto wao English medium kwa minajiri kwamba wakapate elimu bora.

Inshort hakuna faida yoyote ya kumpeleka mtoto English medium kwa elimu ya bongo anayesoma English medium na anaesoma Changamkeni wote wanakula makapi na uchafu wa mfumo wa elimu ya hapa Tz.

Utofauti mdogo pekee uliopo wa anaesoma English medium na Changamkeni ni kukajua kakiingereza ka hovyo ka kuombea maji na kuita dad na mum basi.

Ila viwango vya ujinga na upumbavu vilivyo athiriwa na mfumo takataka wa elimu ya Tanzania wote vipo sawa baina ya anaesoma English medium na anaesoma Changamkeni.
 
Masikini alio kosa pesa za kununa nyama kujidanganya bogaboga ni nzuri kuliko nyama.
Screenshot_20231003-220508_WhatsApp.jpg
 
Mkuu anayesoma english medium ni kwamba anakuwa aware na lugha ya kingereza akiwa bado mdogo
Na lugha ya kingereza ndio lugha ya dunia
Kusema dad na mum, please madam/sir basi hiyo ndio awareness unayo izungumzia ? Na kingereza unacho zungumzia ?
 
Masikini alio kosa pesa za kununua nyama kujifaliji kwamba bogaboga ni nzuri kuliko nyama, zina ongeza damu na nyama kusababisha pressure mwilini..........
Ulitaka kusema nini ?
 
Kimsingi hapo kale kidogo hasa miaka ya mwishoni mwa 90 na 2000 kuendelea,jambo hili lilikuwa na maana sana,maana ajira na mifumo ya maisha ilikuwa rasmi kwa sehemu kubwa.

Kwa Sasa kupeleka mtoto shule hizo hakutafsiri mafanikio ama uhakika wa maisha kwa mtoto husika tena,maisha yamebadilika.haya maigizo ya msomi mwanafunzi anakodi boda boda wakiwa njiani wakipiga story na boda boda anashangaa kusikia boda nayeye kamaliza kozi kama yake tena kwa ufaulu wa juu na ni miaka kadhaa haelewi hatma yake
Hali ni mbaya sana unawezapuuza ukadhani ni maigizo tu.

Kwa Hali ilivyo kwa Sasa kama una nafasi na hela ya uhakika ni afadhali uwekeze zaidi katika assets,halafu kwenye elimu iwe kawaida tu kumpa mtoto utayari na Dunia ya kileo.
 
Kimsingi hapo kale kidogo hasa miaka ya mwishoni mwa 90 na 2000 kuendelea,jambo hili lilikuwa na maana sana,maana ajira na mifumo ya maisha ilikuwa rasmi kwa sehemu kubwa.

Kwa Sasa kupeleka mtoto shule hizo hakutafsiri mafanikio ama uhakika wa maisha kwa mtoto husika tena,maisha yamebadilika.haya maigizo ya msomi mwanafunzi anakodi boda boda wakiwa njiani qakipiga story na boda boda anashangaa kusikia boda nayeye kamaliza kozi kama yake tena kwa ufaulu wa juu na ni miaka kadhaa haelewi hatma yake

Kwa Hali ilivyo kwa Sasa kama una nafasi na hela ya uhakika ni afadhali uwekeze zaidi katika assets,halafu kwenye elimu iwe kawaida tu kumpa mtoto utayari na Dunia ya kileo.
Sahihi
 
Najaribu kufikiria tu mtoto wangu wa miaka 7 namna atakavyoweza kwenda shuleni mwenyewe akivuka barabara na kupishana na bodaboda za hapa jijini. Nawaza jinsi wazazi tulivyo bize na mishe zetu na hakuna muda wa kuwapeleka shule. English medium na mabasi ya njano yanatusaidia sana sisj tulio busy na harakati
 
We jamaa leo umeamkia elimu yetu ya private.
Usiiseme vibaya maana sisi ndo imetufanya tuko hapa tulipo na sijui tungekuwa wapi kama tungepita swahili medium.
Itakuwa kweli hakuna maana huko mbona wote tupo hapa,haaaahaaaa
 
Back
Top Bottom