Fanya vitu hivi ili usizeeke haraka

new level

JF-Expert Member
Apr 21, 2021
269
569
Habari Wana JF niende kwenye mada

VITU VYAKUZINGATIA ILI USI ZEEKE HARAKA.

Punguza kula nyama kwa wingi. Punguza kunywa pombe Kali au acha kabisa hasa hunywaji wa pombe za kienyeji matumizi ya madawa yakulevya. Uvutaji sigara Aina zote ..punguza au acha kabisa. Nyeto pia punguza au acha kabisa boys my bad

Zingatia vyakula natural Sina haja yakuvielezea vyote I mean punguza kula vyakula vya artificial Yani vile vya viwandani au kwa lugha nyepesi vya super market soda soda chocolate , biscuits ,nk sio kwamba uache kabisa ila unaweza ukapunguza.

Kunywa maji yakutosha fanya mazoezi hoga vizuri.. usipake mafuta wakati wakulala hii nimeiyona kwa watu wengi unakuta mtu ngozi yake Niya mafuta mafuta then usiku akimalia kuoga et anapaka mafuta uoni utaongeza acid kwenye ngozi ? Au huoni utachafua mashuka?

Tafuna punjee kadhaa za vitunguu swaum walau mara 3 kwa week hususa mida ya usiku pia kua na tabia yakupaka asali usoni walau Mara 2 kwa week kula matunda yakutosha Kuna nchi zingine familia inaweza ikalalia tikiti , papai na ndizi mbivu na ikalala fresh tu ila huku kwetu bila ugali dagaa au nyama au wali maharage apo bado hujalaza watu.

Watanzania wengi menu yetu ya kila siku imesha kalilika.
Yan asubui chai chapati mbili.
Mchana ugali dagaa
Usiku wali maharage

Sio wote ila mostly ndio menu kuu ya familia zetu zakiswahili ..do u wanna look good right? Sio lazima ule icho chakula January to December .. na issue sio pesa ila Ni mazoea tu. Ma getto boys Kuna maeneo wote hua tunayafaamu usiku wanauzag maziwa na viazi vitam vyakuchemsha ila tunapuuzia eti sio chakula rasmi Cha usiku!

Mtu Yuko radhi ale wali maharage Monday to Sunday kisa anaofia watu wakimuona anakula viazi na maziwa mtindi itatafsirika kua amefulia ..wakati Ni perfect meal sio tu kwa afya ya akili pia hunawirisha ngozi nakua strong na nyororo Kama ya mtoto.

YOU ARE WHAT YOU EAT just eat healthy and your body will be shining like diamond.


Mengine ongezeeni kwa yeyote anaye fahamu.
 
Wakati huo huo wataalam wanasema tule nyama, jamani hii sijui imekaaje!
 
1. Kula chakula hai/chenye kiini cha uhai
Chagua chakula ambacho kiini Cha uhai wake haujaharibiwa kama ni tunda basi mbegu yake iwe na uwezo wa kuota na kuendeleza kizazi.
Pia chakula fresh ni bora zaidi kuliko chakula kilichoandaliwa na kuhifadhiwa Kwa muda mrefu.

2. Kula chakula kizima
Hii husaidia mwili kula kiasi Cha nishati kinachohitajika tuu na mwili ukaridhika na Hilo. Mfano ni rahisi kutumia nusu kikombe Cha mbegu za alizeti kuungia mboga na ikawa tamu lakini nusu kikombe ya mbegu za alizeti ukikamua mafuta utapata kiasi kidogo sana ambacho yasingetosha kupikia mboga hiyo hiyo hivyo kufanya utumie zaidi ya kiasi kinachohitajika.

Mara nyingi maandalizi ya uhifadhi wa vyakula yanalenga kukifanya kuvutia machoni mwa mtumiaji na kukifanya kikae muda mrefu zaidi hivyo sehemu ya chakula inayoharibika kwa urahisi ama ambayo inapunguza mvuto wa kibiashara huondolewa, mfano kwenye maandalizi ya sembe kiini na magamba ya mahindi ambayo ndio bora zaidi hupotea hivyo kufanya chakula kipungue virutubisho muhimu.
Michele wa brown ni bora zaidi kuliko mchele mweupe vivyo hivyo kwenye ngano na bidhaa nyengine.

3.Kula zaidi chakula chenye unyevunyevu.
Maji ni muhimu katika kufanikisha na kurahisisha karibu process zote za mwili; digestion na secretion zikiwemo. Hivyo ulaji wa vyakula vikavu husababisha mwili upoteze maji ambayo yataelekezwa kwenda kurahisisha mmeng'enyo wa vyakula hivyo na tabia hii ikiwa ni ya kudumu inaweza kukuletea madhara mengine kama vile jasho kunuka isivyo kawaida, constipation na hemorrhoids.

Vyakula vyenye unyevu nyevu humeng'enywa kirahisi ndani ya mwili hivyo kuupunguzia stress mfumo wako wa chakula na matokeo yake huweza kuonekana hata katika ngozi ya mtu.

4. Lainisha viungo vyako vya ndani Kwa kutumia mafuta mazuri.
Mwili unahitaji mafuta Ili kutengeneza nishati na pia kama kilainishi kuzikinga ogani muhimu za mwili hivyo unahitaji kilainishi chenye ubora mzuri ili utendaji wake uwe ni wenye athari bora zaidi zisizo na madhara.
Mfano wa vyakula vyenye vilainishi hivi ni mafuta ya nazi, mafuta ya zaituni, parachichi, samaki wenye mafuta na mbegu kama karanga.
 
Back
Top Bottom