Familia zina siri kubwa, mwanasheria msibani: Mwanasheria kazua gunzo msibani akisoma mirathi, watu tulishangaa sana

May 30, 2023
43
130
Kuna jirani yangu mmoja hapa alifariki mwaka jana.
Yeye na mkewe wa ndoa wanawatoto 3. Mtaani tulikuwa tunajua wote hawa ni watoto wake wa kuwazaa kabisa. Hata marafiki zake walikuwa wanajua hivyo kabisa na watu wanaofanya kazi moja.
Na ndugu wa mkewe na ndugu wa mume. Wote walikuwa wanajua watoto watatu kwenye ndoa hio ni wao kabisa.

Sasa msibani, mwanasheria alipewa nafasi ya kusoma mirathi, ni mwanasheria wake kabisa anayefahamika hata na familia kabisa. Alisoma mengi sana ila sasa kwenye utambulisho alisema kwamba,
Marehemu mtu flani alikuwa na mke mmoja wa ndoa na watoto 2 (nasio 3) wa kuwazaa. Watu tulishituka kidogo hata mkewe na watoto 3 wale.

Baadae akawataja majina, alimtaja mototo wa kwanza na wamwisho (tena alitaja kwa majina yao). Wa pili hakumtaja mwanasheria yule.

Kitu kile watu tulishangaa sana japo kichinichini. Hata ndugu nao walipata mshangao kidogo.

Walisafilisha maiti baadae.
Sasa watu tulijiuliza inamaana mama alichepuka akazaa na mtu mwingine?.

Baada ya kurudi kutoka kuzika nilisikia tuu kwamba yule mwanasheria aliongea jinsi marehemu alivyomwambia nini aseme kwa hio mengine hayo yeye hajui.

-Hivi ungekuwa wewe kama ni mke ungefanyaje na ungefikili watoto wanakufikiliaje mama yao???
-Au pengine wewe ni mtoto ambae hujatajwa pale ungejisikiaje, na mama yako ungemfikilije na mwishowe ungefanya nini?
-Na kama wewe ndo mtoto ambae umetajwa mwenzenu asiye Tajwa mungemuonaje na mngemfikilia nini mama yenu??

haya ni maswali nimejiuliza endapo ningekuwa mmoja wao pale sijui ingekuwaje

Hao watoto ni wa kubwa tuu wa mwisho kama anaumri wa miaka 27 hivi.
Karibuni jamani.
 
Marehemu alishajua kuwa huyo mtoto wa pili sio wake ndio maana akamkataa. Hiyo huwa ya kawaida na mara nyingi watoto wa pili huwa wa baba mwingine. Hii hutokea kwenye familia nyingi.
Kwa kauli hii naomba niseme umemanisha na kuthibitisha kwamba hata Mzee Gatete (according to your username) mtoto wake wa pili alipigwa changa la macho na mkewe!

Nikisema hivi nitakuwa nakosea?maana nimeshindwa kujua umetumia sample gani ktk utafiti wako hata ukaja na jibu hili.
 
Kwa kauli hii naomba niseme umemanisha na kuthibitisha kwamba hata Mzee Gatete (according to your username) mtoto wake wa pili alipigwa changa la macho na mkewe?

Nikisema hivi nitakuwa nakosea?maana nimeshindwa kujua umetumia sample gani ktk utafiti wako hata ukaja na jibu hili.
Hahaaaaa, yule Bro wangu kufanana na ndugu upande wa Mama ila hata sisi huwa tuna wasiwasi naye kama kwenu kulivyo yule ndugu yako wa pili. Huoni ana tabia na yupo tofauti na wengine?
 
Back
Top Bottom