Fahamu zaidi kuhusu Kardashev

Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
1,177
3,318
Kardashev Scale ni mfumo wa kupima uwezo wa jamii iliyostaarabika (civilization) kiteknolojia kutokana na kiwango cha nishati wanachoweza kutumia.

Mfumo huu ulioanzishwa na mwanasayansi Mrusi Nikolai Kardashev (1932-2019) unaweka jamii hizi katika makundi matatu ya uwezo.

Type 1 Civilization
Hii ni jamii inayoweza kutumia nishati yote iliyopo katika sayari wanayoishi.

Hii ni pamoja na nishati ya jua lake, nishati zote za hali ya hewa nakadhalika.

Binadamu kama jamii mpaka sasa hatujafikia hiki kiwango na wanasayansi wengi wanategemea tutafikia hapa ndani ya miaka 100 mpaka 200.

Jamii iliyofikia huu uwezo inaweza kudhibiti hali ya hewa na wasipate tabu za vimbunga, ukame, mafuriko, volkano nk.

Kiufupi hakuna kitakacho washangaza au wasichokijua kuhusu sayari yao.

Type 2 Civilization
Jamii hii inaweza kutumia nishati yote inayotolewa na jua na mfumo wa jua (solar system).

Jamii yenye uwezo huu inaweza hata ikahamisha sayari ya Jupiter ikitaka au kuhamisha mfumo mzima wa jua kutoka sehemu moja au nyingine.

Wanasayansi wanasema kwamba kama binadamu ataweza kufikia hatua hii basi hakuna kinachoweza kumdhuru au kummaliza sio maradhi wala kifo labda wajimalize wenyewe.

Type 3 Civilization
Hapa sasa ni jamii yenye uwezo wa kutumia nishati yote iliyopo kwenye galaxy yake.

Yaani nishati itakanayo na nyota zote, sayari zote, blackholes pamoja na kuwa na uwezo wakudhibiti muda jinsi watakavyo.

Mpaka kufikia hapa jamii hii itakuwa na ufahamu wa mambo yote yanayohusisha galaxy yake na watakuwa wana uwezo wa kutengeneza blackholes au hata kuziharibu kabisa.

Kardashev aliamini kwamba hakuna uwezekano wa kuzidi Type 3 lakini baadae wanasayansi waliongeza makundi zaidi ambayo ni,

Type 4 Civilization.
Hapa jamii inauwezo wa kutumia nishati yote iliyopo katika Ulimwengu mzima. Nitoe tu picha kwamba kwenye ulimwengu tunaoujua sisi, kuna galaxy zaidi ya bilioni 200.

Sasa jamii yenye uwezo wakudhibiti Ulimwengu mzima itakuwa ina nguvu kupita kiasi, nguvu ambayo watu kama sisi hatuwezi hata kufikiria.

Kama binadamu ataweza kufikia hatua hii basi hata kuwa binadamu tena, hata kuwa na mwili wala hata kuwa na asichokijua.

Pia atakuwa na uwezo wakuona yaliyopita yaliyopo na yatakayokuwepo na muda kama tunavyopitia sisi hautakuwepo kwao kabisa.

Type 5 Civilization
Hapa sasa jamii inauwezo wakudhubiti nishati zilizopo katika ulimwengu zote (multiverse) na sayari zake zote, galaxy zake zote na muda zake zote. Yaani jamii hii ni kama miungu.

Type 6 Civilization
Jamii hii hapa inategemewa kuwa na uwezo wa kutengeneza ulimwengu na kuumba vyote vilivyomo.

Kuna hadi type 7 lakini nitaishia hapa. Kardashev alipendekeza huu mfumo ili kupima uwezo wa jamii za viumbe wa sayari nyingine (aliens) ambao hatujui kama wapo.

Pia hatuna uhakika sana na huu mfumo kwasababu hatuwezi kujua namna jamii zenye uwezo mkubwa zitakavyoendesha maisha yao na namna zitakavyofikiri.

Kiufupu hatuwezi kutabiri yatakayokuja.
 
Wordsworth,

Huyo kardashev alikuwa muisraeli? kwa sababu nadharia zake hizo zinafanana sana na nadharia za karl max katika Ukomunism.

Max alisema; katika nchi ya Ukomunism hakutakuwa na Askari wala magereza, watu wote watakuwa too morally perfect to see any criminals etc,, What a hillarious!!!😀

Sasa huyo naye analeta nadharia ya ustaarabu wa binadamu atumie nishati YOTE ipatikanayo duniani???

Hajua kila kitu chenye mass kina nishati??, hata yeye mwenyewe ni nishati, E=mc² 🤣
 
Mokaze,
Ndio hata binadamu ni nishati na ndio maana akifa ataoza na kugeuka nishati kwa mimea.
Na utamfananishaje Marx na Kardashev?
Itakuwa hujaelewa chochote nilichoandika.
 
Ndio hata binadamu ni nishati na ndio maana akifa ataoza na kugeuka nishati kwa mimea.
Na utamfananishaje Marx na Kardashev?
Itakuwa hujaelewa chochote nilichoandika.


Wote yumkini ni waisraeli, mmoja ni mwanafalsafa na mwingine ni mwanasayani (Astrophysicist ??), wote wameleta non applicable theories in their respective fields. Na ndiyo maana ninawalinganisha kwa njia hiyo.

Mwili wa mtu akiwa hai ni nishati na kama kutumia nishati yote iliyopo duniani au kwenye galaxes zote ni civilization basi kwanini mtu asijianze yeye mwenyewe kujimaliza (harness ) ili apate hiyo nishati kwa mujibu wa huyo kardashev??,

hii nilitaka kukujulisha kuwa hizo theories ni impractical kwa sababu muhusika mwenyewe mwilini mwake anayo nishati naye ndiyo beneficiary wa hiyo nishati na wakati huo huo yeye ni sehemu ya dunia, sasa itawezekanaje nishati yote katika dunia, galaxes au na Black holes nk, mtu huyo aweze kuzitumia bila kujizuru mwenyewe?.
 
Mokaze,
Wote ni Waisrael?😂😂😂
Hata wewe hapo unavyofikiria unavyoandika na unavyofanya kazi tayari unajitumia wewe mwenyewe kama nishati.
Pili mpaka binadamu aje kufikia huo uwezo we unahisi atakuwa bado Homo Sapiens? Hapana. Mpaka kujakufikia huko huu mwili unakuwa hauna msaada tena bali atakuwa zaidi kama roho au superintelligence.
 
Back
Top Bottom