Fahamu madhara/maudhi ya dawa za presha Captopril na Enalapril

Dec 8, 2023
19
27
Captopril na enalapril ni dawa muhimu kwa watu wenye matatizo ya presha na kisukari.

Maudhi ya dawa hizi ni pamoja na kikohozi kikavu, ambapo mgonjwa huanza kukohoa kikohozi kisichopona au kutulizwa na dawa za kikohozi.

Katika tiba, mgonjwa anapaswa kurudi kwa daktari wake na kuelezea tatizo alilokumbana nalo baada ya kutumia dawa ya captopril au enalapril, ili daktari aweze kubadilisha dozi au kumpatia dawa nyingine mbadala.

Ni muhimu kuzingatia angalizo kuwa, endapo unatumia dawa hizi na ukianza kukohoa kikohozi kikavu, usitumie dawa yoyote ya kikohozi, bali nenda ukamuone daktari wako.

Regards:
Your pharmacist, the medicines expert
 
Back
Top Bottom