English learning thread

Mimi Mama wawili (naamini na wengine wengi) nina nia sana ya kujifunza na kuboresha uwezo wangu wa kutumia Lugha ya Kiingereza. Nimeomba ushauri na nimepata jibu kuwa kuna washiriki wengi hapa JF wana uwezo wa kunikuza katika hii lugha ngeni ambayo kwangu ni Mtihani katika kuweza kuitumia. Naomba ushauri wenu lakini zaidi naomba kujifunza. Kila ambae anaona anaweza kuwa ni Mwalimu naomba niwe mwanafunzi wake katika hili.

Nitajitahidi sana post zinazofuata nitumie Kiingereza ambacho nina hakika kabisa kuwa kitapinda; na hapo ndipo najikabidhi kwenu ili kiwe kinyoofu. Nitakuwa huru sijali kukosea sababu najua ndio njia pekee naweza tambua ni kwa kiasi gani nakosea hasa nikitegemea masahihisho toka kwenu.

Natanguliza shukrani kwa washiriki wote wataoweza nisaidia katika mapungufu yangu ya lugha hii ya Kiingereza.

Mama Wawili.



Congratulations Mama Wawili 👏👏👏

Hope your endeavor has not been to no avail!
 
Are you prepared to invest some cash in this learning effort?

Home Version - Dragon NaturallySpeaking Home - Speech recognition software for the PC - Nuance.co.uk

Why this approach?
Many folks can communicate effectively through written means but that doesn't automatically translate to good verbal skills in the same language. This tool can bridge that gap for you in that you will be able to see your oral speech in text form. This can help to gauge your own preparedness in conveying a message and the words you use to achieve this. Think of this as the little voice in your head coming out to play.

Santa, please remember me when xmas comes round, I need this too!!!!
Noted
 
Hapana,

Kiranga hajui cha kuandika wala cha kuongea.

Ni mwanagenzi wa tenzi kwa enzi
Duni wa kujiruzuku, mwingi wa shauku
Tambo lilokithiri, lilovikwa ujasiri wa ufadhili
Malumbano ya hisani, yanonuka nuksani kwa waso fani ya waghani
Aso chonjo na hiyana, kwa wazee na vijana
Hakuhini takilifu, nadhama ya kamilifu
Kinaganaga husema, ya uzuzu na ya wema
Rai yangu waungwana, tujikite kwenye dhana
Hatari danger!
 
Mi nakumbuka mshua alikuwa na subsciption ya CIA World Factbook(s), Africa Event(s?), collection ya World Book Encyclopedia, Encyclopaedia Britannica, na majarida mengine mengi tu. Alikuwa na chumba alichokigeuza kikawa ofisi/ library ndogo nyumbani. Nothing surprising there, he was a university professor, after all. Vitabu vya atheism na agnosticism navyo vilikuwepo na bado tunavyo nyumbani hadi leo hii.

Hivyo tokea niko mdogo kabisa nimekuwa exposed na mambo mbalimbali ya kitaaluma. Ilikuwa nikiona na kusoma kitu halafu nisikielewe namwuliza ananieleza. Basi nilikuwa namuona anajua mambo mengi sana na kwamba ana akili nyingi sana.

Sasa nikawa najiuliza, huyu mdingi anajuaje mambo yote haya? Yaani ana majibu ya maswali yote ninayomwuliza! Hata American football ni yeye ndo alinifanya niipende kwa kunielezea rules zake na mengineyo. Mid 80s hiyo. Wabongo wangapi walikuwa wanajua hata kuna mchezo unaitwa American football enzi hizo?

Yeye kusoma ndo ilikuwa pastime yake licha ya kuwa ndo career yake pia.

Baada ya kukua na kuanza kuelewa mambo ndo nikajua kwa nini nilikuwa namwona kama mtu wa ajabu sana na ajuaye mengi sana. Kiukweli hakuwa mtu wa ajabu na wala hakujua kila kitu.

Alikuwa anapenda tu kujifunza mambo mbalimbali na yote aliyokuwa anayajua hayakuwa mambo ya ajabu wala. Yalikuwa ni mambo tu ya kawaida na yaliyokuwepo kwa yeyote yule mwenye shauku ya kutaka kujifunza.

Ndo sasa walau nimejua kwa nini enzi hizo Nyerere alionekana kama mungu mtu fulani hivi. Yule mzee naye alikuwa ni mtu mwenye kupenda sana kujifunza mambo. Anecdotes nilizopewa na washua ni kwamba alikuwa ni 'omnivorous reader'.

Humu unaweza kuzungumzia mambo ya jiujitsu au six sigma certification halafu ukarusha au kuambatanisha na bombast za hapa na pale na ukakuta labda ni watu wawili au watatu tu ndo walau wanajua hivyo vitu ni nini. Wengine jiiiii.

Hivyo tu, tayari unaweza ukapachikwa u-genius. Wakati sehemu zingine jiujitsu na six sigma ni mambo ya kawaida kabisa.

So, it really is all relative.
🙏🙏🙏
 
Asante.

Halafu kwa kuwa na mimi najua najifunza bado, siwezi kuacha kuandika kiingereza changu cha kuunga unga kwa kuhofia watu watanisema vizuri au kwa kutaka sifa. Huko nyuma sikuwa hivyo, kwa nini nianze sasa?

Nikifanya hivyo nitajinyima nafasi yangu ya kujiendeleza zaidi.

Nakumbuka tukiwa shule Tambaza tulikuwa tunaongea kiingereza na rafiki zangu mpaka kwenye mabasi, kwa kuwa tulikuwa tunajifunza. Ilikuwa kama utani lakini tulikuwa tunapata mazoezi ya kuongeleshana kiingereza bila kujali watu wengine watafikiri vipi. Wengine wakatuona tunajidai, walioelewa wakaona vijana wanaweka jitihada ya ziada nje ya madarasa kujifunza kiingereza.

Hakukuwa na cha ajabu, after all hizi habari muda huo kwa vijana fulani wa mitaa fulani zilikuwa za kawaida kama jando kwa makabila fulani. Vijana waliozibukia hip hop, sitcoms, comedies, international news, novels, non fiction books etc kuongea Kiingereza, hata kama ni cha kujifunzafunza tu, haikuwa cha ajabu sehemu fulani.

Nakumbuka kuna siku tukakutana na mzee mmoja wa wizara ya elimu alikuwa impressed na maongezi yetu mpaka akajichanganya kwenye mazungumzo yetu, kiingeteza. Mzee anashangaa nimeshika kitabu cha Carl Sagan ananiuliza kama nakielewa. Nikamwambia nakielewa vizuri na hiki cha pili sasa nasoma. Akatuambia "kila mara nasikia mambo mabaya kuhusu shule yenu lakini nyinyi mnaonekana smart tu". Tukamwambia mambo ya samaki mmoja akioza yanatuharibia wote.

Najikuta kwamba kadiri ninavyozidi kujisomea, nakusanya msamiati mkubwa zaidi, na kadiri ninavyokuwa na msamiati mkubwa zaidi, nautumia zaidi. Mara nyingine bila ya kupanga.

Natoa historia zote hizi ili wanaofikiri kuna cha kuiga wajue kufika hapa - ambapo mimi.napaona bado chini sana, lakini.wengine wanaona panatamanika sana tu- haikuwa.kazi ya mara moja. Ni utamaduni uliojengeka tangu niko mdogo naangalia comics za Archie na Tintin, najaribu muelewa story kwa kuangalia picha, halafu ukweli kwamba sijui kusoma kiingereza na nashindwa kuelewa story yote ukaniuma sana na kunisukuma kujifunza kiingereza mwa njia zote, kuanzia kamusi.mpaka kujifua kwa maongezi.

There is a point when one has to decide to be a Bodhisattva or a Buddha.

One shouldn't be blamed for either decision.
Ukiona vyaelea ujue vimeundwa🙏
 
Back
Top Bottom