Dkt. Slaa: Freeman Mbowe aachane na Maridhiano maana hayafai, Katiba sio mali yake binafsi au mali ya Rais Samia

Mkuu kwa nchi hii utawapata wapi?
Kwa Ile ya walioba ililetwa na chama Cha siasa gani?? Narudia Tena iundwe taasisi huru ya watu isiyokuwa na mhemuko wala kuongozwaa na chama chochote Cha kisiasa ijapokuwa washiriki wa mchakato huo huenda wakawa na vyama vyao wavipendavyo. Chama chochote chakisiasa kikiongoza zoezi hili haita patikana katiba ya wananchi matokeo yaki itakuwa katiba Kwa matakwa ya chama hicho. Tutakosea pakubwaa
 
Hakuna mtu kamzuia Slaa kutafuta katiba mpya, Kama Mbowe anatafuta na maridhiano, yeye atafute ya ugomvi, hakuna kupangiana, kila mtu na department yake.
Tena yeye aliunga Juhudi za Marehemu. Hayakuwa maridhiano?
 
Wananchi kut

Mpaka sasa Katiba yetu hii ya Jamhuri ya Muungano ni Katiba ya chama kimoja cha siasa(CCM) baada ya chama kushika hatamu ndipo ilipoanzishwa na misingi yake ni ya kulinda chama cha mapinduzi na viongozi wake.Ambapo Magufuri aliyumbisha nchi kwa kutumia hatamu hiyo kumweka kiongozi aliyeona anafaa yeye na si wananchi wa Tanzania kuchagua kiongozi wanayemtaka.Ambapo mwaka 2019 aliweka viongozi wa Serikali za mitaa nchi nzima wa chama chake ili aibe uchaguzi mwaka unaofuata.Pia 2020 aliweka wabunge aliowataka yeye na matokeo yake tumeyaona sasa imekuwa serikali ya kusingiziana.
Vyama vya upinzani vinapodai Katiba mpya viko sahihi kutokana na tukio la nchi kuwa ya Mfumo wa Vyama vingi.Kwa hiyo hakuna sababu ya kubishana kama tunaamini katika mfumo wa vyama vingi vya siasa,maoni yao yaheshimiwe na yatekelezwe maana hiyo ndiyo demokrasia.
Vyama vya siasa vikae kimyaa kabisa kwenye mchakato wa siasa. Kama hoja nikatiba hiii inawaonea wa vyama vya upinzani sio kweli nakukatalia kabisaa, jeee ikitokea wakashinda Kwa katiba hiiii itakuwa ushindi wao ni batiliii?? Mbona wabunge wa upinzani wako bungeni si Kwa katiba hiii hiiii???
 
Narudia Tena iundwe taasisi huru ya watu isiyokuwa na mhemuko wala kuongozwaa na chama chochote Cha kisiasa ijapokuwa washiriki wa mchakato huo huenda wakawa na vyama vyao wavipendavyo..
Kuunda taasisi siyo suluhisho. Tume ya uchaguzi ya akina MAHELA, na ile ya akina JECHA nazo ziliundwa lakini zikakosa tija kabisaa
 
Sahivi kuna udini mkali sn teuzi zote ni Tanga, Pwani na Zanzibar
Tunao uhuru wa kuongea, tunao uhuru wa kufanya nikutano ya kisiasa, hakuna cha watu wasiojulikana, .Sehemu za Ibada zimebakia kwa ajili ya ibada na sio masuala ya kuongelea siasa za chama kimoja .....
 
Akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii Aprili 20, 2023, Dkt Slaa amesema akipata nafasi ya kukutana na mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe atamshauri aachane na maridhiano kwa kuwa hayafai.

“Nikipata nafasi ya kukutana nitamwambia kwamba fuata principle za siasa safi, simamia, kwa sababu kwa sasa unatakiwa kuwapatia watanzania katiba mpya. Maridhiano hayafai” amesema

Amesisitiza, “Maridhiano hayafai kwasababu yanakaa zaidi ya mwaka, hakuna taarifa kwa wananchi. Maridhiano si mali ya Samia na ya Mbowe. Katiba inayodaiwa ni ya watanzania. Katiba si mali ya watu wawili, wala sio ya CCM na CHADEMA, ni ya watanzania. Watanzania lazima wajue wanataka katiba ya aina gani”
Dkt Slaa amesema amemsikia mara kadhaa Rais Samia akisema kuwa wataangalia katiba ya mwaka 1977 kwa kuwa Rasimu ya Warioba imepitwa na wakati, yeye anasema haya ni makosa makubwa sana.

“Someni preamble pale kwenye katiba mwanzoni imeandikwa nini, imeandikwa sisi watanzania tumeamua, kwenye katiba”

Kuhusu kusubiria uteuzi, amesema kwa umri wake hasubirii tena fursa hiyo, pia amemsfia Freeman Mbowe kuwa mwanasiasa mzuri, mkonge na mpambanaji wa siku nyingi.

Chanzo: East Africa Radio
Yeye kama mtanzania kama walivyo watanzania wengine ,ni Nini mchanga wake au mpango wake nje ya maridhiano kuhakikisha katiba mpya unapatikana?!.
 
Na Mimi naongezea kwamba, chama chochote Cha siasa kiachane na harakati za kutafuta katiba ya wananchi, kwani katiba ya wananchi itatafutwa na wananchi wasio na mlengo wowote wa kisiasa, ili iweze kusimamia vyama vyote, vya kisiasa. Labda chadema itapendeza wakisimama kutafuta katiba ya chama Chao sio katiba ya wananchi.
Hakuna mwananchi asiye na mrengo wa kisiasa..!!

Wote tuna mrengo kama sio mrengo wa kushoto basi wewe ni wa mrengo wa kulia na kama hauko kotekote huko basi wewe ni wa mrengo wa kati..!

Unaweza ukawa unaishi tu na usilijue lakini huo ndiyo uhalisia..

Na kumbuka hili:

Kila mtu anaathiriwa na siasa. Na ndiyo kusema siasa ndiyo hayo maisha unayoishi. Siasa ndiyo inayoamua upate huduma za kijamii kama maji, umeme, barabara, elimu nk za ubora au uduni wa kiwango gani..

Siasa ndiyo inayoamua wewe Ujamaa ni mhimu uwe na maisha ya kiuchumi ya namna gani. Siasa na wanasiasa ndiyo wanaamua mfumo wa maisha ya kijamii, siasa, utamaduni na uchumi wa watu katika nchi uweje..

Siasa ni mfumo wa maisha ya watu ktk nchi au taifa fulani

Kwa hiyo unaposema "chama chochote cha siasa kiachane na harakati za kutafuta katiba ya wananchi" bila shaka unakuwa hujui unasema nini..!!

Chama cha siasa siyo kitu au kiumbe fulani kisicho na uhai. Chama cha siasa ni watu. Kwa kauli yako hii Ina maana watu wote wafe na maana yake ndiyo inakuwa mwisho wa chama siasa!!!

Unataka katiba ya wananchi, ungana na wananchi wenzako waliokwisha weka wazi misimamo yao kisiasa pengine na vyama vyao vya siasa..!!
 
Wananchikaribia wote wanavyama vyao, ila tunachokataaa, wasitumie vyama vyao kudai katiba ya wananchi. Maana katiba ya wananchi ni Sheria mama, hivyo haitakiwi kubuguziwa na chama chochote Cha kisiasa. Tunavyama vingi vya siasa tukiruhusu vyama hivyo Kila kimoja kiingize umasilahi wake hatuta pata katiba ya wananchi, matokeo yake ni katiba ya matakwa ya watu na vyama vyao. Hivyo iundwe taasisi huru kama ya akina warioba ndio ichakate na kudai katiba ya wananchi, licha ya kuwa hao nao watakuwa na vyama vyao wavipendavyo. Tukirusu makundi ya vyama vya siasa kunajisi mchakato wa katiba hatutaelewana matokeo yake tutamwaga damu. Hivyo ni vyemaa iundwe time huru kabisa ichakate zoezi Hilo, vyama vya siasa vitaalikwa kama wajumbe wengine ilikuchangia maoni Yao. Lakini sio matakwa Yao, na vikubali kwamba so Kila wao wanachokitaka lazima kiwekwe, lazima wakubali kukosolewa Kwa kile wanachokiamini kingewekwa kwenye katiba ya wananchi. Hiii tunataka katiba ya wananchi sio katiba ya chama Cha siasa. Tukitengeneza katiba Kwa mihemko ya vyama vya siasa tutapigana na hatutoelewanaa. Asante.
 
Na Mimi naongezea kwamba, chama chochote Cha siasa kiachane na harakati za kutafuta katiba ya wananchi, kwani katiba ya wananchi itatafutwa na wananchi wasio na mlengo wowote wa kisiasa, ili iweze kusimamia vyama vyote, vya kisiasa. Labda chadema itapendeza wakisimama kutafuta katiba ya chama Chao sio katiba ya wananchi.
Hao wananchi hawahitaji uongozi?

Juhudi za hao wananchi hazihitaji kuratibiwa?

Wakati mwingine mnajifanya kuwa na akili kichwani kumbe ndani ni patupu kabisa!

Uliona wapi wananchi wakifanya jambo bila ya kuwepo na usimamizi wa kuratibu shughuli zao!

CHADEMA kuwepo kwenye nafasi hiyo haina maana ndiyo inayopigania katiba yao; hii itakuwa ni kazi ya wananchi wenyewe.
 
Itengenezwe tume huru, ndani yake kutakuwa na viongozi kama vile kipindi Cha akina walioba na wenzao. Hao ndio watakao ratibu zoezi, na haoviongozi wa vyama vya siasa watakuwa waalikwa kwma wajumbe wengine. Hujanielewa wapii bwasheee???
 
Ni nani atakayeweka msukumo wa kufika hatua hiyo kama siyo hao CHADEMA na makundi mengine wanaounganisha juhudi za wananchi kuishinikiza serikali iruhusu mchakato huo?
 
Huyu Mzee wa Kinyaturu ni tofauti sana na Tundu Lissu.

Huyu Mzee ni kigeugeu rahisi kuhongwa na CCM lakini hebu tumpe second chance.

Jana nilikuwa nikimsikiliza alipokuwa akifafanua upigaji wa ardhi uliofanywa na Hussein Bashe Mzee yuko vizuri labda njaa tu ndio zinazomsumbua.
 
Ni nani atakayeweka msukumo wa kufika hatua hiyo kama siyo hao CHADEMA na makundi mengine wanaounganisha juhudi za wananchi kuishinikiza serikali iruhusu mchakato huo?
Ukisha sema chadema kwenye katiba ya wananchi sio sawa nchiii sio chadema pekeee kunavyama vingi. Chadema wataalikwa kama wajumbe wengineee. Kwani tume ya warioba ilihamasishwa na chama kipiii??
 
Huyu Slaa haaminiki tena yeye alishakula mihogo wakati yupo CHADEMA aiache CHADEMA na mambo yake yeye aende Lumumba akachukue mgao wake.
 
Sasa kama Tatizo ni chama tawalaa, ndio maaana tunakemea Sanaa Kwa nguvu zote chama chochote Cha kisiasa kisiiingilie zoezi hiliiii laupatikanaji wa katiba ya wananchi, vyama vya siasa vipiganie katiba za vyama vyaooo, sio katiba ya wananchi, vyama vya siasa vinaweza viaaalikwa kwenye mchakato, lakini siokuendesha mchakatooo, na hiii nikukataa umasilahivyama usiiingilie na kunajisi katiba ya wananchiii
Unachoongea hakieleweki. Kuna aliyewazuia hao wananchi ukiwemo wewe kudai katiba mpya? Mbona hatujawaona mkidai huo mchakato? Waacheni Chadema wafanye wanavyoona inafaa. Wakati wanapitishwa kwenye moto kwa suala hilohilo si mlijificha nyuma ya keyboard kuwadhihaki? Leo pressure yao imesaidia walau, halafu mnafiki mmoja anaibuka eti "wananchi ndio wadai katiba". Muone.
 
Hivyo vyama vyenu vipiganie katiba yenu, kama mnataka kupigania katiba ya wananchi jivueni mwamvuli wa chama chenu muonekane neutral hapo mtatafuta katiba ya wananchi. Sawaaa bwasheee.
 
Back
Top Bottom