Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,304
- 118,547
Wanabodi!
Japo mimi ni mwanachama wa chama cha siasa na sio Chadema, ila mimi ni political advisor mzuri tuu, nimeisha wahi kuwa hired kuwa a political advisor wa taasisi mbalimbali kubwa tuu za kitaifa na kimataifa ambaye kwa sasa naendesha kipindi kiitwacho KMT kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten kila siku Jumapili saa 3:00 usiku na marudio kila siku za Jumatano saa 9:30 alasiri.
Tukubali tukatae Siasa za uchaguzi za Tanzania zinatawaliwa na chama kimoja, CCM kama Chama Dola vikishindana na vyama makapuku katika mashindano ya kugombea kisu cha makali kuwili kwa mtindo wa kunyang'anyana huku CCM imeshika kwenye mpini na kuelekezea wapinzani wake upande wa makali kuwili!.
Tena game yenyewe inachezewa katika uwanja tenge, CCM ikiwa upande wa juu palipoinuka, washindani wakiwa upande wa chini palipolala!.
Tangu tumeanza tena uchaguzi wa vyama vingi ile 1995, mazingira ya uchaguzi ni yale yale, hivyo kila uchaguzi ni vicheko kwa CCM na vilio kwa wapinzani.
Funga kazi ni uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ndipo wapinzani wakapigwa bumbuwazi na matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.
Wengi waliyapokea matokeo hayo as a surprise, lakini kuna akina sisi, we saw it coming tangu ile ile 2015 na tuliandika humu, kwa waliosoma mabandiko haya na kuyaelewa, matokeo ya uchaguzi wa 2020 was not a surprise.
30th Nov, 2015 Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
2017 Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?
2019 The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja
Chama kikuu cha upinzani, kilisusia uchaguzi ule na kuuita ni uchafuzi, hakiyatambui matokeo, hakimtambui mshindi, hakilitambui Bunge!.
Chadema wakapewa nafasi 19 za ubunge wa viti maalum, wakazigomea, kukajitokeza mashujaa 19 wakachangamkia tenda.
Machi 12 Sir Godi akafanya jambo, taifa likatangaziwa Machi 17, Rais Samia, akiwa ni mwanamke wa kwanza, akaingia madarakani kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu.
Akaamua uchaguzi wa mwaka 2025, tutasimamisha mwanamke ili Watanzania wachague mwanamke.
Hii ya kusimamisha mwanamke, 2025, hata mimi niliunga mkono. Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Kama CCM Itamsimamisha Rais Samia, kuwa Mgombea wake wa urais kwa uchaguzi mkuu wa 2025, mnaonaje kama tutamchagiza na kumshinikiza Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ndie awe mgombea wa pamoja wa umoja wa upinzani?.
Baada ya Rais Samia kupendekeza 2025 twende na Mwanamke, na Chadema wakaingia maridhiano na CCM na kukubaliana kugawana nusu mkate, niliwashauri Chadema na wapinzani Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!
Tundu Lissu alipotangaza kupitia ITV kuwa yeye atagombea urais kwa tiketi ya Chadema uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, niliogopa sana, kwasababu Lissu namjua, kwa kuzingatia maridhiano ya Chadema na CCM halafu Lissu agombee na Rais Samia, kiukweli Rais Samia angeyaoga sana, kwasababu Lissu ana uwezo fulani kumshinda hata Magufuli, ndio maana nilishauri Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!
Na aliporejea nchini na kukuta maridhiano, aliyozungumza haya, niliuliza humu Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Sasa kwa vile maridhiano yamevunjika, tunarudi kule kule kwenye politics of hostilities and confrontation, the best candidate kwa umoja wa upinzani ni Freeman Mbowe, kwasababu huyu ni a mild politician, ni muungwana, akigombea na mwanamke kampeni zitapigika, lakini Lissu ni an extremist hachelewi kumlipua mtu.
Mbowe akilikubali hili, atapiga ndege 3 kwa jiwe moja, na upinzani utavuna Wabunge wengi, madiwani wengi, vijiji, mitaa na vitongoji, ila kwenye urais, bado ni CCM, halafu upinzani uitumie hiyo miaka 5 ya 2025-2030 kujipanga kujaribu kutimiza hili neno la uzi huu, Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!
Hao ndege 3 ambao Freeman Mbowe akiamua kugombea urais wa 2025 kama mgombea wa umoja wa wapinzani
1. Kufuatia kuvunjika kwa maridhiano, kati ya CCM na Chadema, hii maana yake ni hakuna tena kugawana nusu mkate, hivyo Freeman Mbowe asipogombea urais angegombea ubunge jimbo la Hai, nusu mkate ndio ingemrudisha Mbowe bungeni, bila hiyo nusu mkate, then uchaguzi wa 2025 utakuwa kama ule wa. 2020, hivyo kugombea urais ndio the best honorable execuse ya kutogombea jimbo la Hai.
2. Freeman Mbowe na Rais Samia, wanajuana vema, Mbowe alipofutiwa kesi ya ugaidi, break yake ya kwanza ikawa ni Ikulu, na Chadema ilijuwa inakabiliwa na hali fulani, mara ghafla Chadema mambo yake yakawa super, mara wakawa na uwezo wa kufanya kikao cha Baraza Kuu, mara viongozi wakaanza kupiga trips za ulaya, Mbowe akawa haeshi Ikulu. Hivyo Freeman Mbowe akimchalleng Samia, then it's a clash of titan, hivyo Freeman Mbowe atamtikisa Samia na upinzani utavuna kura nyingi na kupata wabunge na madiwani wa kutosha.
3. Kufuatia Freeman Mbowe ku overstay kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Chadema, kugombea urais kutampa Freeman Mbowe a perfect and an honorable exit.
Paskali