MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 12,824
- 32,011
Huyu mzee anazeeka vibaya.
Hakuna mwananchi yeyote yule atakayempambania Katiba mpya kama hajihusishi na chama chochote cha siasa.Na hakuna nchi yoyote ile duniani iliyowahi kupata Uhuru wake bila kuwa na chama chochote cha siasa.Vilaza wengi hufikiria kuwa mtu anapokuwa kwenye chama fulani cha siasa basi huyo mtu si chochote katika jamii maana akili yake hufikiria kwenye maslahi zaidi.Huu ni upungufu wa Akili Mwilini na ni ushamba uliopitiliza.Na Mimi naongezea kwamba, chama chochote Cha siasa kiachane na harakati za kutafuta katiba ya wananchi, kwani katiba ya wananchi itatafutwa na wananchi wasio na mlengo wowote wa kisiasa, ili iweze kusimamia vyama vyote, vya kisiasa. Labda chadema itapendeza wakisimama kutafuta katiba ya chama Chao sio katiba ya wananchi.
Mariziano!Hakuna mtu kamzuia Slaa kutafuta katiba mpya, Kama Mbowe anatafuta na mariziano, yeye atafute ya ugomvi, hakuna kupangiana, kila mtu na department yake.
Viongozi wasitokane na vyama vya siasa. Kama ni wanasiasa wasitumie majukwwaa ya siasa ya vyama vyao huku wakitaka katiba ya wananchi. Viongozi wasiwe viongozi wa kisiasa, mfano eti chama flani kikiwa na mavazi ya chama Chao kusaka katiba ya wananchi.Unazani wananchi wenyewe watatafutaje katiba kama hakuna kiongozi wowote ambae atasiamia ...
Ni sawa na kusema wanafunzi waandae mitahala ya kufundishia wao wenyewe bila waalimu..
Sent from my M2010J19SI using JamiiForums mobile app
Yes hata kwa JPM tulipoenda Mwanza siku ya Uhuru ilikua ni kutafuta maridhiano haya haya tu. Sasa Leo yamepatikana tuanze tena kulumbana ya Nini?. Mbowe aachwe atafute suluhu mezani maana confrontational politics za Hawa waTZ waoga haziwezi zaa matunda. Hakuna haja ya mabavu kama mtu ni sikivu. So tuunge mkono maridhiano at least mpaka mwaka uishe tukiona hakuna jema Mnyika alisema watajitoa.Confrontational politics hazijawahi kuisaidia CDM sana sana zimewaumiza mno (Rip Mawazo, Saanane)......Mbowe apongezwe kwa hatua hii ya maridhiano angalau yataipa Chadema Uhuru wa kufanya siasa.
zitto junior
econonist zitto junior JokaKuu Tindo idawa MTAZAMO Pascal Mayalla ...nadhani ni wakati muafaka wa Chadema kumrudisha kundini Mzee Slaa asaidie kudai katiba kwa niaba ya Cdm na raia maana Mbowe hamna imani naye.
The fact is, tunahitaji Katiba Mpya sasa, sio unasubiri mpaka shangazi yako aondoke madarakani ndipo nawe uanze kupiga kelele.Yeye alipofanya maridhiano na Magufuli Nani alimpangia cha kufanya??
Huyu mzee ninamsikilizaga sana kwa kujifunzaAkihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii Aprili 20, 2023, Dkt Slaa amesema akipata nafasi ya kukutana na mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe atamshauri aachane na maridhiano kwa kuwa hayafai.
“Nikipata nafasi ya kukutana nitamwambia kwamba fuata principle za siasa safi, simamia, kwa sababu kwa sasa unatakiwa kuwapatia watanzania katiba mpya. Maridhiano hayafai” amesema
Amesisitiza, “Maridhiano hayafai kwasababu yanakaa zaidi ya mwaka, hakuna taarifa kwa wananchi. Maridhiano si mali ya Samia na ya Mbowe. Katiba inayodaiwa ni ya watanzania. Katiba si mali ya watu wawili, wala sio ya CCM na CHADEMA, ni ya watanzania. Watanzania lazima wajue wanataka katiba ya aina gani”
Dkt Slaa amesema amemsikia mara kadhaa Rais Samia akisema kuwa wataangalia katiba ya mwaka 1977 kwa kuwa Rasimu ya Warioba imepitwa na wakati, yeye anasema haya ni makosa makubwa sana.
“Someni preamble pale kwenye katiba mwanzoni imeandikwa nini, imeandikwa sisi watanzania tumeamua, kwenye katiba”
Kuhusu kusubiria uteuzi, amesema kwa umri wake hasubirii tena fursa hiyo, pia amemsfia Freeman Mbowe kuwa mwanasiasa mzuri, mkonge na mpambanaji wa siku nyingi.
Chanzo: East Africa Radio
Thubutu.Najiuliza Kwa sauti je chadema uchaguzi ukishika dola kabla katiba haijabadilushwa watataka ibadilishwe?
Jibu ni ndioNajiuliza Kwa sauti je chadema uchaguzi ukishika dola kabla katiba haijabadilushwa watataka ibadilishwe?
Uyu mzee nae atulie , na ikiwezekana aongeze mke mwingine, si ndo uyu alikejeli sana chadema kipindi kahongwa na mwendazake ubalozi, Leo anaongea nini,Akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii Aprili 20, 2023, Dkt Slaa amesema akipata nafasi ya kukutana na mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe atamshauri aachane na maridhiano kwa kuwa hayafai.
“Nikipata nafasi ya kukutana nitamwambia kwamba fuata principle za siasa safi, simamia, kwa sababu kwa sasa unatakiwa kuwapatia watanzania katiba mpya. Maridhiano hayafai” amesema
Amesisitiza, “Maridhiano hayafai kwasababu yanakaa zaidi ya mwaka, hakuna taarifa kwa wananchi. Maridhiano si mali ya Samia na ya Mbowe. Katiba inayodaiwa ni ya watanzania. Katiba si mali ya watu wawili, wala sio ya CCM na CHADEMA, ni ya watanzania. Watanzania lazima wajue wanataka katiba ya aina gani”
Dkt Slaa amesema amemsikia mara kadhaa Rais Samia akisema kuwa wataangalia katiba ya mwaka 1977 kwa kuwa Rasimu ya Warioba imepitwa na wakati, yeye anasema haya ni makosa makubwa sana.
“Someni preamble pale kwenye katiba mwanzoni imeandikwa nini, imeandikwa sisi watanzania tumeamua, kwenye katiba”
Kuhusu kusubiria uteuzi, amesema kwa umri wake hasubirii tena fursa hiyo, pia amemsfia Freeman Mbowe kuwa mwanasiasa mzuri, mkonge na mpambanaji wa siku nyingi.
Chanzo: East Africa Radio
Agenda ya KATIBA mpya ni ya wananchi.Namshauri Dr Slaa aanzishe chama ili afanye kile anachoona kinafaa kupitia chama chake mwenyewe. Huu utaratibu wa kurukia rukia ajenda za watu na kuzifanya kuwa za kwake hauleti maana yoyote kwa taifa.
Siasa za majitaka, mikiki mikiki na uongo wa mwembe yanga zimeshapitwa na wakati. Kwa sasa nchi imetulia aache watu wafanye kazi, na mambo yao kwa ueledi mkubwa na manufaa kwa taifa.
Jamaa anapiga huku na kule. Anajua moja itamuokoa.Slaa kama anataka kukumbukwa ama na CCM au CHADEMA