Diwani ashindwa jaribio la kumchafua kwa makusudi Waziri Mstaafu Kawambwa huko Bagamoyo

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,386
24,358
Diwani mstaafu wa Kiromo anayeitwa Hassan Wembe, ambaye hana historia nzuri sana, amefanya jaribio la kihuni na kuudhi kwa kumzushia tuhuma za uongo aliyekuwa waziri Awamu ya Nne, mh. Shukuru Kawambwa.

Clip iliyorushwa mitandsoni na kusambaa kama moto wa nyika, ilikuwa ikimtuhumu ati Kawambwa ni dalali wa viwanja!

Imejulikana kuwa sababu ya mzozo ni uamuzi wa wanakijiji wa Kitopeni kuamua kufunga barabara yao kutokana na malori ya mchanga kuiharibu kabisa na kufan gari ndogo za wananchi kushindwa kupita.

Katika clip hiyo Diwani Hassan Wembe alidiriki kumvaa mwilini Kawambwa ambaye hakuonekana kubishana wala kurudisha maneno ya kuudhi ya mhuni Hassan Wembe.

Kwa tunaomfahamu Kawambwa toka alipokuwa wizarani (Miundombinu Ujenzi) huyu jamaa ni maji ya mtungi, hana presha au munkari.
Pengine kwa vile alikuwa mwalimu UDSM-Uhandisi.

Habari zilizopatikana ni kwamba katika hilo valangati la Diwani mstaafu Hassan Bwana alikuwepo jirani ya Kawambwa ambaye ni DSO mstaafu (Mkuu wa Usalama wilaya).

Na habari zinatonya kuwa huyu Wembe na grupu lake wamelala lupango.
 
Wana kesi ya kujibu maana alimtishia kumuua Kawambwa.

Halafu huyo jamaa boya sana eti yule DSO anamuitwa wewe mtu wa protokali hahaha ila namhurumia he is a deadman walking kwa sababu hahaha aliyempiga kofi Marehemu A. H. Mwinyi hahaha cheza na wastaafu.

Huyo jamaa nimemuona kwenye clip ni mjinga sana tena jinga mno. Huwezi kuwa na jazba za kijinga namna ile
 
Issue sio udalali hapa. Malori ya mchanga yanaingia kwenye eneo lenye barabara ya kuingia kwake na pia kwenda shule ya sekondari na kufanya uharibifu wa barabara. Yeye Kawambwa na huyo mwingine aliyedhalilishwa DSO Mstaafu wa Kawe na Bagamoyo Madondola waliamua kuweka vigogo vya mnazi ili malori yasipite na kuharibu barabara ndipo walipokutwa na huyo Hassan Wembe Diwani mstaafu wa Kiromo na beki ya zamani ya timu ya Malindi Zanzibar. Wembe ni mmiliki wa mashimo ya mchanga huko Kiromo kwahiyo kuzibwa Kwa barabara kunazuia malori kuingia na hivyo kukosa fedha. Mhusika huyo wlWembe na washirika wenzie walikamatwa jana na wako lokapu hadi sasa. Nadhani jambo limekuwa kubwa kwani mmoja ya waliodhalilishwa ni DSO Mstaafu na DSO Bagamoyo kasimamia zoezi zima kuhakikisha wanakamatwa!

C&P
 
Wana kesi ya kujibu maana alimtishia kumuua Kawambwa.

Halafu huyo jamaa boya sana eti yule DSO anamuitwa wewe mtu wa protokali hahaha ila namhurumia he is a deadman walking kwa sababu hahaha aliyempiga kofi Marehemu A. H. Mwinyi hahaha cheza na wastaafu.

Huyo jamaa nimemuona kwenye clip ni mjinga sana tena jinga mno. Huwezi kuwa na jazba za kijinga namna ile
Kwa tukio lile huyo diwani atakuwa ndy mpumbav na mjinga # tz

Ova
 
Huyo mwehu atajuta kujitutumua hivi unawezaje kumdhalilisha mtu kama Dr. Kawambwa? Mtu ni binamu wa JK halafu alikuwa na power kubwa sana enzi za utawala wa JK unadhani bado hana connection hata kwenye chama chake ambacho ndio kimeshika dola?

Ameenda kumharass yule DSO pale ndio ameingia choo cha kike ndio maana hii ishu DSO wa bagamoyo ndio ameishikia bango mwenyewe jamaa atafurahi eti oooh mimi kijana so whaat? Ukiwa kijana ndio ukose nidhamu kwa wakubwa zako?

Aombe Mungu Dr Kawambwa amhurumie asikomae nae otherwise ana kesi ya kudhalilisha na kujeruhi maana amempiga yule mzee kamsukumasukuma na kuwafunga kamba kama waahalifu na kuwatuhumu ni waharifu. Atafurahi.
 
Huyo mwehu atajuta kujitutumua hivi unawezaje kumdhalilisha mtu kama Dr. Kawambwa? Mtu ni binamu wa JK halafu alikuwa na power kubwa sana enzi za utawala wa JK unadhani bado hana connection hata kwenye chama chake ambacho ndio kimeshika dola?

Ameenda kumharass yule DSO pale ndio ameingia choo cha kike ndio maana hii ishu DSO wa bagamoyo ndio ameishikia bango mwenyewe jamaa atafurahi eti oooh mimi kijana so whaat? Ukiwa kijana ndio ukose nidhamu kwa wakubwa zako?

Aombe Mungu Dr Kawambwa amhurumie asikomae nae otherwise ana kesi ya kudhalilisha na kujeruhi maana amempiga yule mzee kamsukumasukuma na k kawambwa uwafunga kamba kama waahalifu na kuwatuhumu ni waharifu. Atafurahi.
Mbona kawambwa alikuwa mpole vile akifungwa Pingu na mgambo.jamani nikajua amefulia
 
Back
Top Bottom