Polisi mkoani Pwani yawakamata Watu Wawili waliomdhalilisha Waziri Mstaafu Dkt. Kawambwa! Aliyerekodi Video atakiwa kujisalimisha!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
85,058
143,833
Jeshi la Polisi limewakamata Watu Wawili waliomdhalilisha Waziri wa zamani wa Miundombinu Dr Shukuru Kawambwa

Aidha Jeshi la Polisi limemtaka mtu aliyerekodi tukio la udhalilishaji huo na kulirusha mitandaoni ajisalimishe mara Moja.
---
Polisi Mkoani Pwani imewakamata watu wawili waliomdhalilisha Waziri wa zamani wa Miundombinu na Mbunge wa Bagamoyo Shukuru Kawambwa na limemtaka aliyesambaza video ya kudhalilishwa kwa Waziri huyo kujisalimisha.

Kwa mujibu wa Polisi aliyekamatwa ni Hassan Wembe ambaye anaonekana kwenye clip hiyo akimpa vitisho Waziri huyo na Mbunge wa zamani wa Bagamoyo.

Source: Kitenge Tv

Pia Soma: Shukuru Kawambwa kwenye Kashfa ya Udalali wa Viwanja
 
Jeshi la Polisi limewakamata Watu Wawili waliomdhalilisha Waziri wa zamani wa Miundombinu Dr Shukuru Kawambwa

Aidha Jeshi la Polisi limemtaka mtu aliyerekodi tukio la udhalilishaji huo na kulirusha mitandaoni ajisalimishe mara Moja

Source: Kitenge Tv
Safi sana, yule kijana abinywe hadi atapike damu! Jamii isiyoheshimu wazee ni ya hovyo. Nilipoona ile video nilijua fika ile ni siasa!
 
Nilimshangaa sana huyo jamaa. Hajitambui na nilijua tu atajutia alichofanya. Achilia mbali waziri mstaafu huyo ni mtu mzima kama baba yake heshima kitu cha bure.
Wacha jamhuri imfunze adabu.
Yule kijana ndiyo wanaitwa MTU MZIMA OVYO. Makelele kibao eti katafute Kamba nimfunge wa ovyo Sana jamaa. Kawambwa katulia mzee wa watu, kitendo kikemewe kabisa kile. yule ni mzee kuna namna ya kum handle kama alikosea mahali
 
Back
Top Bottom