Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kidney-1.jpg


Alhamisi ya pili ya Mwezi Machi kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Figo Duniani ili kutoa ufahamu na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa afya ya figo na magonjwa yanayohusiana na figo. Kupitia maadhimisho haya, watu hupata fursa ya kujifunza kuhusu njia za kuzuia magonjwa ya figo, kudhibiti magonjwa ya figo, na umuhimu wa kuwa na maisha yenye afya ya figo.

Aidha, maadhimisho haya huchangia katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu haja ya kuchangia katika juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa ya figo, pamoja na kusaidia watu wenye matatizo ya figo kupata msaada unaohitajika.

Hata hivyo, ugonjwa huu huambatana na dhana nyingi potofu zinazofifisha kasi ya kupambana nao hivyo JamiiCheck imekuandalia ufafanuzi wa Dhana hizo kama sehemu ya kuongeza ufahamu kwa Jamii.

1. Ugonjwa wa Figo hauwapati Watu wengi
Dhana hii haina ukweli.

Kwa mujibu wa International Society of Nephrology, zaidi ya watu Milioni 850 wanaishi na aina Fulani ya ugonjwa wa figo duniani.

Takwimu hizi ni mara mbili ya watu wanaoishi na Ugonjwa wa Kisukri, Mara 20 ya watu wanaoishi na Saratani na Mara 20 zaidi ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

2. Dalili za Ugonjwa wa Figo zinaonekana Kirahisi
Kwa bahati mbaya, watu wengi wenye ugonjwa wa Figo huwa hawazijui dalili zake kwasababu katika hatua za mwanzo za ugonjwa wa figo, watu wengi huwa hawaoneshi dalili yoyote.

Dalili zinaweza zisionekane hadi ugonjwa wa figo unapokuwa katika hatua za juu, na wagonjwa wengi hata Nchini Tanzania hugundulika wakiwa tayari wamefikia hatua mbaya. Njia bora ya kujua kama una ugonjwa wa figo ni kupima na mara tu unapogunduliwa kuna hatua nyingi unazoweza kuchukua ili kupunguza kuendelea kwa ugonjwa huo.

3. Upimaji wa ugonjwa wa figo ni mchakato mrefu na wa gharama kubwa.
Kupima ugonjwa wa figo ni rahisi kuliko inavyodhaniwa. Inaweza kufanywa kwa vipimo vya bei nafuu pindi mtu anapofika hospitalini, pia haichukui muda mrefu. Ugonjwa huu unaweza kupimwa kwa namna mbili rahisi;
  • Kutumia mkojo ili kuangalia kiwango chake cha Protini. Kuwa na kiasi kidogo cha protini kwenye mkojo wako inaweza kuwa ishara ya ugonjwa wa figo.
  • Kipimo cha damu cha kukadiria GFR (kiwango cha uchujaji wa figo).
4. Hauwezi kufanya chochote kujitoa katika Mazingira hatarishi ya kuugua ugonjwa wa Figo
Dhana hii haina ukweli.

Siyo kila mtu aliye kwenye mazingira hatarishi atapata ugonjwa wa figo bali jitihada binafsi zinaweza kusaidia kulinda figo zako.

Kula vizuri, fanya mazoezi ya kawaida, dhibiti shinikizo kubwa la damu na sukari ya damu, weka uzito unaofaa, acha kuvuta sigara, na usitumie ovyo dawa za maumivu kama vile ibuprofen Pamoja na kula chakula chenye chumvi nyingi kupita kiasi.

Hatua hizi zote zitakusaidia kuweka figo zako zikiwa na afya na kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa figo.

5. Sababu za kuugua Ugonjwa wa Figo hazijulikani
Hii ni dhana nyingine isiyo sahihi.

Sababu kuu mbili zinazopelekea kuugua ugonjwa wa figo ni kisukari na shinikizo kubwa la damu. Sababu zote mbili zinaweza kudhuru figo zako kwa kusababisha uharibifu wa mishipa midogo ya damu kwenye figo.

Baadhi ya sababu zingine ni Pamoja na maambukizi makubwa ya damu, kutumia dawa au sumu, magonjwa adimu kama Lupus, Glomerulonephritis ambao ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa figo.

6. Tiba pekee ya ugonjwa wa Figo ni dialysis
Siyo kila mtu aliye na ugonjwa wa figo anahitaji dialysis.

Ugonjwa wa figo ni ugonjwa unaoendelea. Katika hatua zake za mwanzo, kawaida hudhibitiwa na mazoezi, lishe, na dawa. Kwa njia hii, watu wengi wanaweza kupunguza au kuacha kuendelea kwa ugonjwa wa figo na kufurahia maisha ya kawaida.

Ndiyo maana ni muhimu sana kupata na kutibu ugonjwa wa figo mapema. Dialysis au upandikizaji wa figo inahitajika tu ikiwa ugonjwa wako wa figo unazidi kuwa mbaya na kuendelea hadi kushindwa kwa figo.
 
Waambie pia wanaume wa kimatumbi wenye dhana potofu ya kuwa ukitoa figo kumsaidia ndugu au rafiki watapungikiwa na nguvu za kiume
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom