DED anapokataa kupitisha kibali cha uhamisho na kufunga datasheet

jonas255

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
222
104
Habari wanajamvi,

inapotokea mtumishi amefuata taratibu zote za kuomba uhamisho, yaani ameomba nafasi ya kuhamia sehemu kupitia kwa mwajiri na akajibiwa kupitia kwa mwajiri kuwa nafasi ipo na baadaye mwajiri huyo akakuombea kibali Tamise kupitia kwa RAS, Katibu mkuu tamisemi anatoa kibali cha uhamisho wako na baadaye DED anakataa kupitisha kibali na kukufungia data sheet bila sababu zozote za msingi na ameng'ang'ania barua yangu.

je nifate utaratibu gani ili niweze kuhama naombeni ushauri wenu... JINA NIMEONA KWENYE LIST YA MAJINA YA TAMISEMI
 
Pole sana mkuu....
Nasikitika binafsi sina namna ama jinsi ya kukusaidia upande huo.
Ebu fanya kuvuta subra, maana humu jf ni jungu kuu
 
Nenda kamshtaki Kwa DC , kama walikubali kukupitishia wakati unaomba uhamisho, haiingii akilini wakukatalie katika hatua ya mwisho.
DC asipokutatulia lalamiko lako nenda Kwa RC. Mamlaka ya juu ya malalamiko ni katibu mkuu utumishi
 
Hiyo barua yako lazima Nakala iwe kwa RAS, sasa wewe kama unaona DED anasumbua fika kwa RAS mjulishe juu ya adha unayokutana nayo kwa huyo Mkurugenzi.RAS akileta longolongo nyoosha utumishi moja kwa moja
 
Habari wanajamvi,

inapotokea mtumishi amefuata taratibu zote za kuomba uhamisho, yaani ameomba nafasi ya kuhamia sehemu kupitia kwa mwajiri na akajibiwa kupitia kwa mwajiri kuwa nafasi ipo na baadaye mwajiri huyo akakuombea kibali Tamise kupitia kwa RAS, Katibu mkuu tamisemi anatoa kibali cha uhamisho wako na baadaye DED anakataa kupitisha kibali na kukufungia data sheet bila sababu zozote za msingi na ameng'ang'ania barua yangu.

je nifate utaratibu gani ili niweze kuhama naombeni ushauri wenu... JINA NIMEONA KWENYE LIST YA MAJINA YA TAMISEMI
NENDA NGAZI YA JUU YAKE KAMA RAS mjulishe na vielelezo vyako vyote ulivo navyo utasaidiwa tu
 
Ushapokea barua yako ya uhamisho,kama bado ameishikiria nenda tamisemi kachukue copy yake,zen nenda kariport kituo chako kipya. Hayo mambo ya datasheet utayafanya baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi itakua ni Mbeya na kama ndivyo ni vema ukavuta subira kuna baadhi ya halmashauri kuna tatizo la vibali kutoka TAMISEMI,sidhani kama DED anaweza kukaa na barua yako akuzuie kuhama labda kama mna matatizo binafsi kati yenu.
 
Back
Top Bottom