DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

1. Gari chache sana saaaana mnakera. Sijui mnazipark vituoni au?

2. Kuna madereva wanajiona Miungu watu wanapita na "Out of Service" yaani.

3. Vingine mnajitahidi. Hope mtaboreka zaidi.
Tunakushukuru kwa kupitia kwenye uzi huu,

1. Suala la uchache wa Mabasi linafanyiwa kazi na katika kipindi kifupi tutakuwa tumelimaliza kabisa tatizo hilo.

2. Kuhusu madereva tunawashughulikia kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zilizopo na ikitokea umepata tatizo lolote usisite kutupigia katika namba yetu ya bure 0800110147 kwa msaada zaidi.

3.Tunaendelea kuboresha huduma zetu kila siku ndiomaana tukaamua kuja humu ili mtusaidie mawazo. Tunashukuru sana kwa mchango wako mdau.
 
Yaani ninyi ni wa kuomba maoni kweli.
Aisee hii dunia huwa haiishiwi vituko. Si mngeanza kwanza kurekebisha hali ya hovyo iliyopo ambayo hata haihitaji maoni. Baada ya hapo ndiyo mnatafuta maoni kutoka kwa watumiaji wa huduma.
Hali iliyopo haihitaji maoni ya watu sababu hali mliyo nayo inatokana na uwezo mdogo either kiutawala, kiubunifu, kiutendaji na kiuwwzo kama Kampani.
Kwa kifupi mna matatizo, malizeno kwanza matatizo yenu ndiyo mtujie wananchi tuwapatieni changamoto.
Ulitakiwa uyabainishe haya matatizo, ndiyo maana wamekuja, sasa ukiandika hivi tu, si utakua unafanana nao tu.
Sio kila kero kila mtu anakerekwa.
 
Asante kwa kuja.
Ni lini hayo mabasi mtayapeleka Mwanza pia ili wananchi wapate huduma ya usafiri..??
Sababu jiji la Mwanza limekua na tayari limechangamka na mkituletea hizo Bus zikaanzia route ya Kisesa, Igoma, Neshno, Buzuruga, Mabatini, Nata, Pepsi, Mkuyuni, Nyegezi, Buhongwa, Nyashishi hadi Usagara and Return.
Tunashukuru kwa mchango wako, kwa sasa tuko katika mchakato wa kukamilisha sheria ya DART ambayo itatupa mamlaka ya kwenda kuanzisha huduma katika miji mingine mikubwa kama , Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Tanga n.k. , kwahiyo wana Mwanza msiwe na wasi wasi tutawafikia.
 
Ulitakiwa uyabainishe haya matatizo, ndiyo maana wamekuja, sasa ukiandika hivi tu, si utakua unafanana nao tu.
Sio kila kero kila mtu anakerekwa.
Kama hawaoni basi hata nikiwapatia either hawataelewa au hawana nia bali wanatuchora tu.
Kwamba hata hili la mabasi kutotosha wanshitaji maoni yako? Hata kipindi kile mabasi ni mengi lakini usimamizi na upangiliaji wa route kuwa mbovu nalo wanahitaji maoni yako?
Kama hawawezi kuona hizi kero nyingi zilizopo, basi watoe kandarasi wafanyiwe kila kitu badala ya kutaka kwenda for cheap
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Mkiwa active mtapata mengi sana. Ila msije mkaja na mambo ya wenzenu TANESCO ya kupewa changamoto walizonazo, wao badala ya kuhangaika na changamoto hizo, wanaanza mambo ya kutaka mtu aandike namba yake ya simu, anakoishi na jina lake kamili..!!!
 
Back
Top Bottom